Harakati ya Vijana wa Kutofungamana kwa upande wowote

Harakati ya Vijana wa Kutofungamana kwa upande wowote

Imefasiriwa na / Zeinab Abd ElMohsen Mekky 

Shirika la Vijana wa Harakati  ya Kutofungamana kwa upande wowote limeanzishwa rasmi mjini Shusha, siku ya Ijumaa,   Julai 29, mnamo mwaka  2022, na hivyo kwa mara ya kwanza kupitia miaka 61 tangu kuanzishwa kwa harakati hiyo, ambayo kulingana naye wakala ya "AZERTAC" imeriopti kwamba hati hiyo ambayo huitwa " Mkataba wa Shusha" inasema kuanzisha Shirikia la Vijana wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote, na imerekodi jina la Shusha, mji mkuu wa utamaduni wa kiazabajani katika Historia ya Shirika hilo la kimataifa.

Hiyo ilikuja wakati mkutano wa Vijana  wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote, uliofanyika mjini mkuu wa Azabajani, Baku, mnamo kipindi cha Julai 25 hadi 29,  mwaka 2022,  ulipitisha uamuzi wa kubadilisha Mtandao wa Vijana  wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote ambayo imeanzishwa mwaka 2019, kwa Shirika la Vijana la kimataifa hupitisha mawazo ya harakati, kanuni na malengo yake, na kukuza na kuimarisha vijana katika nchi 120 wanachama wa harakati.

Kuanzishwa kwa Mtandao wa Vijana wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote ni mpango wa pili baada ya kuanzishwa kwa Mtandao wa Bunge wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote pamoja na uongozi wa Rais wa Azabajan kwa Shirika hilo, kisha shirika hilo la vijana limechukua "Baku" Makao yake Makuu, na Mwakilishi wa Azabajan amechukua urais wake kwa kipindi cha miaka 3 kama muhula wa kwanza, pamoja na kuanzishwa kwa ofisi wa kikanda katika nchi wanachama.

Wazo la kuanzisha Shirika hilo lililotolewa kwa mpango wa Azabajani mnamo Oktoba 4,2021, liliungwa mkono na kukaribishwa kwa wawakilishi wa nchi wanachama wanaoshiriki katika mkutano wa Vijana huko Baku, hivyo kwa kubadilisha Mtandao wa VIjana wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote kwa Shirika la Vijana wa Harakati ya Kutofungamana, kulingana na hayo kutoa nafasi bora kwa vijana ili kushirika katika majukwaa ya kimataifa.

Ikumbukwe kwamba Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote ni Shirika la pili kwa ukubwa baada ya Umoja wa Mataifa, hiyo inamaanisha kwamba Shirika hilo la vijana litakusanya pamoja wawakilishi kutoka nchi wanachama 120, na inatarajiwa kwamba Shirika la vijana litakuwa na athari chanya kwa maendeleo ya vijana.