Baraza la Mawaziri la Misri ni mshiriki na mfadhili rasmi wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Baraza la Mawaziri la Misri ndilo taasisi kuu ya kiutekelezaji ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na linajumuisha Waziri Mkuu na mawaziri,nao ni sehemu ya serikali, inayozingatiwa chombo cha juu cha utendaji na utawala nchini.
Majukumu makuu ya Waziri Mkuu ni kutoa kanuni muhimu za utekelezaji wa sheria, ikiwa ni bila kucheleweshwa, kurekebisha, au kutotekeleza kwake, na anaweza kumwakilisha mwingine kuyatoa, ila Sheria imetoa nani maalum mhusika mwenye jukumu la kuyatoa, pia Waziri Mkuu anatoa maamuzi maalum yanayohitajika kujenga mahali na vituo vya umma, kuyataratibu baada ya ruhusa ya Baraza la Mawaziri, pamoja na kupitisha maazimio ya kanuni za udhibiti baada ya ruhusa Baraza la Mawaziri pia.
Waziri aweka sera ya wizara yake akipanga na mamlaka husika, na kufuatilia utekelezaji, mwelekeo na udhibiti wake, ndani ya mfumo wa sera kuu ya nchi.Nafasi za uongozi wa juu wa kila wizara zajumuisha nafasi ya Naibu wa kudumu, linalohakikisha utulivu wa taasisi na kuinua kiwango cha ufanisi katika kutekeleza sera yake.
Pia majukumu ya serikali ni pamoja na kushiriki na Rais wa Jamhuri katika kuweka sera kuu ya nchi na kusimamia utekelezaji wake, kulinda usalama wa nchi, kulinda haki za raia na maslahi ya nchi, kusimamia kazi za wizara, mashirika na taasisi za umma zinazohusiana nayo, kuyaratibu na kuyafuatilia, pamoja na kuandaa mipango ya sheria na maamuzi, na kutoa maamuzi ya kiutawala kwa mujibu wa sheria, kufuatilia utekelezaji wake, kuandaa mpango mkuu wa nchi; kuandaa rasimu ya bajeti kuu ya serikali, kutayarisha na utoaji wa mikopo kwa mujibu wa masharti ya katiba, na utekelezaji wa sheria.