Kituo cha Kiislamu cha Misri nchini Tanzania ni jengo la Kiislamu na jukwaa la wito wa Kiislamu wenye uvumilivu

Kituo cha Kiislamu cha Misri nchini Tanzania ni jengo la Kiislamu na jukwaa la wito wa Kiislamu wenye uvumilivu

Imetafsiriwa na: Basmala Hisham 
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

 Ndani ya muktadha wa umakini wa kuimarisha uhusiano wa mawasiliano na ndugu wa Kiafrika, na kwa kuzingatia jukumu la Misri katika kueneza mawazo ya wastani katika nchi mbalimbali za ulimwengu na maslahi yake katika kina cha Afrika, na chini ya maagizo ya Rais Gamal Abdel Nasser na Rais wa Tanzania Julius Nyerere, Kituo cha Kiislamu cha Misri kilianzishwa katika Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania mnamo mwaka 1968, kwenye eneo kubwa la hekta 12, katika maandalizi ya upanuzi wake wa baadaye katika vitongoji vya kifahari zaidi vya mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam, kwa ufadhili wa Misri, kutekeleza majukumu ya kumwita Mwenyezi Mungu na kueneza mafundisho ya dini ya Kiislamu yenye uvumilivu na kama hatua ya kwanza kwa maandalizi ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Misri jijini Dar es Salaam.

Kituo hiki kinajishughulisha na shughuli za utetezi na elimu nchini Tanzania na nchi zote za Afrika Mashariki, na kazi katika kituo hicho imeandaliwa kwa makubaliano kati ya pande za Misri na Tanzania zilizosainiwa mnamo mwaka 2003, ambapo kinatokana na kundi la wajumbe waliochaguliwa kwa uangalifu wa Wizara ya Misri ya Awqaf, lenye wajumbe kumi na moja, pamoja na walimu saba wa Kitanzania wanaofundisha masomo yaliyoagizwa kwa wanafunzi wa taasisi za Al-Azhar Al-Sharif, na wizara inabeba mishahara ya wote, pamoja na kubeba mishahara ya walimu wa Tanzania, na wizara pia hutumia shughuli zote na vifaa vya kituo hicho, ambacho kwa sasa kinafundishwa Takribani wanafunzi elfu moja wa Kitanzania katika hatua mbalimbali za elimu kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari, pamoja na shughuli za Msikiti wa Kituo.

Kituo hicho kinajumuisha kliniki ya matibabu ili kutoa huduma za matibabu kwa watu wa Tanzania kwa bei ya chini, na kuifanya kuwa nguzo ya utetezi, elimu, mafunzo na matibabu, mnara wa Misri nje ya nchi na njia ya kujenga madaraja ya mawasiliano na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, na hata bara la Afrika.