Kumbukumbu  ya kutimiza kwa ujenzi wa Mnara wa Kairo (Aprili 11, 1961)

Kumbukumbu  ya kutimiza kwa ujenzi wa Mnara wa Kairo (Aprili 11, 1961)
Kumbukumbu  ya kutimiza kwa ujenzi wa Mnara wa Kairo (Aprili 11, 1961)
Kumbukumbu  ya kutimiza kwa ujenzi wa Mnara wa Kairo (Aprili 11, 1961)
Kumbukumbu  ya kutimiza kwa ujenzi wa Mnara wa Kairo (Aprili 11, 1961)

Mnara wa Kairo ... hadithi ya ushikamanifu  wa Nasser na changamoto kwa kiburi cha ncha  kubwa zaidi ulimwenguni.

Katikati ya miaka ya hamsini ya karne iliyopita, hasa mnamo 1956, Marekani ilimtoa Rais Gamal Abd El Nasser "Dola milioni za kimarekani" - kama Rushwa - ikidai kuwa ni hiba ya kuunga mkono miundombinu ya kimisri, lakini lengo lilikuwa kutafutia kusimamisha jukumu la kitaifa la Misri , uungaji  mkono wa Nasser kwa harakati za uhuru na mapinduzi yanayopambana ukoloni katika nchi za Kiarabu na Kiafrika, hasa mapinduzi ya Algeria - yaliyoongozwa na Ahmed bin Bella - dhidi ya ukoloni wa Ufaransa wakati huo, lakini utaifa wa Misri wa Abd El Nasser uliamua kutoa funzo la kuhimili kwa wale wanaofikiria siku moja kununua Dhima za watoto wake au kuvunja utashi wake, wakati ambapo Abd El Nasser aliamua kutumia Fedha za kimarekani kujenga ishara ya uthabiti, changamoto na heshima "Mnara wa Kairo " na wamarekani wameuitwa "Mwiba wa Abd El Nasser,"  ama wamisri  wameutoa jina la «Urithi wa Roosevelt» kama ushahidi wa Ujasiri wa Misri mbele ya Marekani na kushikamana kwake kwa mahusiano  pamoja na Algeria.

Mhandisi  Noam Shabib, aliunda Mnara wa Kairo kwa namna ya "Ua la lotus", lililoshikiliwa nyuma ya ustaarabu wa zamani wa Farao na linaashiria milele. 

Wafanyikazi 500 walishiriki katika ujenzi wake, ambao una ghorofa 16, na unafikia urefu wa mita 187, kuwa mnara wa pili mrefu zaidi ulimwenguni wakati huo baada ya Mnara wa Evial, na urefu wake unazidi urefu wa Piramidi uKubwa kwa karibu na mita 40. Kujengwa kwa Mnara wa Kairo kumechukua miaka mitano (kutoka 1956 hadi 1961) kwa gharama ya paundi milioni 6 za kimisri wakati huo.

Kuhusu Noam Shabib :

Yeye ni msanifu majengo na mbuni  mmisri wa kizazi cha waanzilishi - kizazi cha kwanza cha wasanifu wa asili katika kizazi cha ishirini - alizaliwa Novemba 28, 1915 mjini Kairo, alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kairo na akapata digrii ya ubora katika usanifu majengo mnamo 1937, kisha akapata shahada mbili za  kwanza za uhandisi wa udongo na Ujenzi, naye ni  mmiliki wa Kampuni ya Shabib kwa majengo, na shughuli  zake zikitegemea utengenezaji wa saruji thabiti , naye akapata leseni yake, na shughuli  zake maarufu zaidi ni kama (Mnara wa Kairo – ujenzi wa Gazeti la Al Ahram- Jengo la Kairo Motor-  Jengo la Kanisa la Mtakatifu Katrine -  Sinema ya Ali Baba), pamoja na minara kadhaa huko Kairo, Noam Shabib alikufa nchini Canada mnamo 1985.