Kampuni ya Uzalishaji wa Coke ya El-Nasr

Imetafsiriwa na/ Hasnaa Hosny
Imeharirwa na/ Mervat Sakr

Kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1968, na Amri ya Rais Na. 2383 ya 1960, iliyotolewa na Rais Gamal Abdel Nasser wakati aliona kuongezeka kwa Uagizaji wa makaa ya mawe, kwa hivyo Dkt. Aziz Sedky, aliyepewa jina la Utani "Baba wa Viwanda vya Misri", alielekeza kuanzishwa kwa kampuni hiyo kuongeza sekta ya chuma. Kampuni hiyo ilianza Uzalishaji wake mwaka 1964, ikiwa na betri moja yenye tanuru 57 zenye Uwezo wa Uzalishaji wa tani elfu 328 za madini ya Coke, na tarehe 11 Mei 1966, Rais Gamal Abdel Nasser na Alexi Kosygin, Waziri Mkuu wa Umoja wa Sioufiti wakati huo, walitembelea viwanda vya Kampuni ya Uzalishaji wa Coke ya El-Nasr huko Helwan.

Mwaka 1974, betri ya pili ilianzishwa na Uzalishaji ulianza na tanuru 50 zenye Uwezo wa Uzalishaji wa tani elfu 328, na kufikia mwaka 1979 betri ya tatu ilianzishwa na tanuru 65 zenye Uwezo wa Uzalishaji wa tani elfu 560 za coke, na mwaka 1993, betri ya nne ilianzishwa na tanuru 65 zenye Uwezo wa Uzalishaji wa tani elfu 560 kwa mwaka, hivyo Uwezo wa Uzalishaji wa betri nne ulikuwa tani milioni 1.6 kwa mwaka. Betri ya kwanza ilijengwa Upya mnamo 2000 na ya pili mnamo 2006.

Kampuni hiyo ina viwanda vinne:

Kiwanda cha Coke

Kiwanda cha lami (Tar Distillery)

Kiwanda cha Nitrate

Multi-Purpose Logistics Module (Kitengo cha Kusudi Nyingi)

Pia ina matawi matatu:

Gati kwenye bandari ya Alexandria kwa kusafirisha Coke nje ya nchi, na kupakua makaa ya mawe, malighafi kwa coke, kwa kiwango cha kila siku cha tani elfu 4 / siku na uwezo wa tani elfu 45.

Gati kwenye Bandari ya Dekheila huko Alexandria kupakua makaa ya mawe kwa kiwango cha kila siku cha tani elfu 3 na Uwezo wa tani elfu 100.

Gati kwenye Nile kupokea mashua kusafirisha coke na makaa ya mawe kwa kiwango cha Upakiaji na Upakuaji wa tani 4000 / siku.

Bidhaa muhimu zaidi za kampuni:

Kampuni hiyo hutoa bidhaa mbalimbali kuanzia Coke ya Ukubwa mbalimbali na benzol, ammonium sulphate 20.6% nitrojeni, nitrate safi ya ammonium, lami ya electrode, naphthalene, sulfonate ya rangi ya sodiamu, tar mbichi, mafuta ya chrysote, na bidhaa zingine nyingi zinazotumiwa katika kilimo, viwanda, madini, kemikali, Ujenzi, chakula, Uzalishaji wa kijeshi, na Utafiti wa kisayansi.

Kampuni hiyo pia inashughulikia mahitaji mengi ya viwanda vya kimkakati vya kitaifa na kusafirisha bidhaa zake kwa Ulaya, Asia, Amerika na nchi za Kiarabu.

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy