Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni Mjumbe kwa Kamati ya Uhakiki wa Shindano la Kuchagua Waigizaji katika Taasisi za Elimu
Imetafsiriwa na: Rwan Abdel El-Naby
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Klabu ya Senima ya Taasisi ya Al-Thanawi nchini Urusi ilifanya majaribio ya utendaji kuchagua waombaji kushiriki katika filamu fupi iliyoandaliwa na klabu na ushiriki wa mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Kundi la tatu, Yassine Fathali, Mjumbe kwa Kamati ya Uhakiki, kwa uzoefu wake tajiri na tofauti katika uwanja wa utamaduni, hasa katika uwanja wa uigizaji wa maonesho, na kushughulikia mada kadhaa za kupendeza kwa vijana na maisha ya shule, na hii inakuja ndani ya muktadha wa maandalizi ya kushiriki katika Jukwaa la Mkoa wa Sinema na Picha nchini Tunisia.
Inatajwa kuwa "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" unalenga kujenga kizazi kipya cha viongozi wa mabadiliko ya vijana na maono kulingana na mwelekeo wa urais wa Misri katika nchi mbalimbali kupitia ushirikiano, pamoja na kuunganisha viongozi wa vijana wenye ushawishi mkubwa duniani na mafunzo, ujuzi muhimu na maono ya kimkakati.