Wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa Wazindua Vipindi vya Utangulizi vya Kuvuka Mabara
Imetafsiriwa na: Shams Adel
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, umeaondaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri tangu kuanza kwa usajili wa udhamini, waliandaa vikao vitatu vya utangulizi na ushiriki wa kikundi cha viongozi wa vijana kutoka mabara matatu ya Asia, Afrika, na Amerika ya Kusini, ambapo vikao hivi vilijumuisha vikao viwili kwa Kiarabu, ambapo wasemaji kutoka nchi nyingi za Kiarabu na Afrika walishiriki, ikiwa ni pamoja na: Sudan, Tunisia, Libya, Moroko, Iraq, Jordan, Chad, Saudi Arabia na Misri, na Kikao kingine kwa Kiingereza, kilichojumuisha wasemaji kutoka Afghanistan, Colombia, Brazil, Pakistan na Côte d'Ivoire.
Mratibu wa vikao vya maarifa na mwanachama wa timu ya vyombo vya habari vya kimataifa kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Libya Al-Zubair Al-Burki, alielezea kiburi chake katika ushiriki mkubwa wa udhamini, na athari kali na za kuhamasisha kuhusu mfumo na teknolojia za kitaaluma na za juu, ambazo udhamini unafuata wakati wa maandalizi yake ya kupokea kundi la tatu, na majibu ya haraka kwa maswali ya waombaji, kuwasilisha mapendekezo yao kwa kutoa fursa kwa vijana kuchukua idadi kubwa ya Udhamini mwaka huu, Mbali na matarajio yao ya kupanua kipindi cha usajili kwa kundi la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, iliyopokea ulinzi wa Mheshimiwa Rais.
Wazungumzaji wa nchi zinazoshiriki katika vikao vya utangulizi kutoka kwa wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walipongeza kiwango kikubwa ambacho Misri inafurahia kutoka kwa jengo la taasisi la muda mrefu, na uongozi wa kisiasa na wa akili na wa kidiplomasia, wenye uwezo wa kuuza nje picha ya nchi yao kitaaluma, wakisisitiza kwamba walipata uzoefu huu kwa karibu kupitia mikutano yao mingi na wanadiplomasia, watoa maamuzi, na mawaziri ndani ya mfumo wa ushiriki wao katika udhamini, na kwamba hawakutarajia kwamba Misri inafurahiya kiwango hiki cha maendeleo, taaluma na shirika.
Ni vyema kutajwa kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unakuja kama mojawapo ya utaratibu wa utendaji wa kuwasilisha uzoefu wa Misri katika kujenga taasisi za kitaifa, kama mfano wa kufuatwa, kama toleo la kwanza la ilizinduliwa mnamo mwezi Juni 2019, kuwa udhamini wa Afrika-Afrika unaohusiana na urais wa Misri wa Umoja wa Afrika, chini ya ufadhili wa Urais wa Baraza la Mawaziri, na kisha kupanua katika toleo lake la pili ili kujumuisha mabara matatu Afrika, Asia na Amerika ya Kusini, Chini ya kaulimbiu "Ushirikiano wa Kusini-Kusini" na kushinda ulinzi wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi mnamo tarehe Juni 2021, na sasa iko katika mchakato wa kuzindua toleo lake la tatu chini ya kauli mbiu "Vijana wasio na Uadilifu na Kuhamasisha Ushirikiano wa Kusini-Kusini" mnamo tarehe Juni ijayo 2022 chini ya ufadhili wa Rais wa Jamhuri kwa mara ya pili mfululizo.