Mohamed Wardi..  Misri iwe huru daima na Sudan

Mohamed Wardi..  Misri iwe huru daima na Sudan

 kufuatilia habari zote ulimwenguni , kwa kadiri nilivyoweza, ni mojawapo ya tabia zangu muhimu sana tangu  utotoni na hazijaisha kwa mapitio ya  umri ,bali imekuwa yenye kina na uchambuzi  zaidi pamoja na imekuwa tofauti   katika nyanja na upande wa kijiografia.. Leo, ninapofanya kawaida yangu ya kila siku kuangalia habari, nimepata habari ya kutangazia Serikali ya Sudan, ikiwakilishwa na Baraza la Mpito linaloongozwa na  Jenerali Al-Burhan, kuwa 2022 kama mwaka wa kiutamaduni kwa kumheshimu mwimbaji marehemu wa Sudan "Mohamed Wardi." wakati umesitisha kitambo , kabla ya wakati kunichukua zamani kama miaka thelathini iliyopita, nilikuta kipindi cha utoto wangu ambacho nilikiishi tangu siku ya kuzaliwa katika mji mkuu wa Sudan hadi kipindi cha shule ya upili, kurudi kufikiri siku hizi kulikuwa kuzuri ambazo zilishuhudia  mwanzo ya utoto na athari za malezi, na kurudi kulikuwa na furaha na thamani kama siku hizo, nilipojifunza kuwa nchi ni kubwa, na kwamba ushirikiano kati yao ni  lengo kubwa mno..

Wakati nyumba ya babu yangu kutoka upande wa mama yangu - Mwenyezi Mungu amrehemu - katikati ya  Khartoum ilikuwa ikishuhudia mikutano ya Jumuiya ya Misri, Jumuiya za Kiarabu na jumbe za kidiplomasia na majadiliano yalikuwa yenye masuala ya kina, mpana wa upeo, yenye  athari inayoendelea bila ya  mabishano, upumbavu, au uvunjaji wa mipaka, yenye tamaduni mbalimbali, ustaarabu unaopatana.. hakuna usaliti, kashfa,  wala msimamo mkali, au udanganyifu. Nilipokuwa nikiimba kila asubuhi katika uwanja wa Shule ya Kiinjili ya Misri huko Sudan, na wenzangu kutoka Sudan, Iraki, Ufalme  wa Oman na Palestina, pamoja na baadhi ya mataifa ya Ulaya wanaimba, “ Misri  idumu  huru na  Sudan..  idumu nchi ya Bonde la Mto Nile wa Usalama.” Tukihitimisha kuimba kwetu kwa asubuhi Katika kipande cha wimbo ambacho ni  bora zaidi, “Sudan kwa Misri.. na Misri kwa Sudan.”.. siku hizo nilipokuwa nikisali magharibi na Ishaa   kwenye Kanisa la Bikira Maria kwenye pwani ya  Mto wa Nile linalokudumu huko Khartoum  na hii kwa sababu ya ushirikiano wangu  kwa mafunzo ya kila wiki ya  kambi ndani yake.. .. Siku zile ambazo ninazidaiwa na mapenzi yangu  kwa nchi ya kuzaliwa  kutokana na imani   kwa athari yake na uwepo wake, na upanuzi wa athari hii hadi mbali zaidi ya vile wanawe wengi wanavyofikiria.

Labda jambo zuri zaidi ambalo Sudan  ilitofautisha  nayo siku hizi ni Kiwango cha tafauti za kiutamaduni na upanuzi wa kisanaa ikiwa ni pamoja na kuimba  ,fasihi , sanaa za watu na makongamano ya kiutamaduni ambayo " ukumbi wa urafiki " uliyoyashuhudia   na ambao uko mbele ya  kisiwa cha " Toty " ambapo Mto Nile mweupe ulikutana na Nile ya buluu , ikijitayarisha  kuzindua pamoja ili kufika mwisho ya  safari huko Misri .. Msanii marehemu "  Muhammed Wardi " alikuwa miongoni mwa wasanii maarufu zaidi wa uimbaji wa Sudan wa kinubi kwani anazingatiwa Mmoja wa watu wasudan wa kasikazini ambao ni karibu nasi zaidi kwa upande wa Utamaduni pamoja na mila na desturi   . Inawezekana Kiwango cha kuimba kwake ambacho kimefikia takribani nyimbo 250 ، kilikuwa juu zaidi kulingana na wasanii  wasudan wa kizazi  sawa sawa .  " Muhammed wardi " aliwaongoza wasanii kadha kutoka Sudan , Misri , Ethiopia , Uganda na Kenya ambapo nyimbo zake zimekuwa desturi na njia zinazoigiwa . Vilevile , Msanii Mmisri mzuri mno Muhammed Mounir  aliimba wimbo wake " Katikati ya Duara " ambao mwenye maneno na Toni nzuri mno . Lingine nililolikumbuka pia  wakati wa safari yangu pamoja na chombo cha wakati ni  ushikamano wa  harakati ya raia wa Sudan  mnamo kipindi cha sitini dhidi  ya Jenerali "Ibrahim Abud " kupitia wimbo maarufu wa " Wardi "  ambao ulitungwa na Mshairi msudan Bw. " Muhammed El-Fetury "  na maneno yake yanasema " Asubuhi imechomoza .. Gereza wala mlinzi hawapo  .. hapo Alfajiri kama ina mabawa mawili  yanaruka .. na hapo huzuni iliyochora macho  na iliyotukaza  .. na iliyotutawanya kwa kila bonde ikawa  furaha inayotolewa mioyoni  ewe nchi yangu "  na wimbo huo ulielezea pendeleo za kitaifa wa " Wardi "  zenye upendeleo wa kushoto haba  ambazo zilimfanyia miongoni mwa wale wa kwanza waliopinga utawala wa " ukombozi " wenye msimamo wa kulia wa  ikhwani  ambapo alihamia Misri mnamo mwaka 1989 anapokaa kama mzalendo kwa nchi  , msimamo na sanaa yake  na  Misri ilimkaribisha vizuri ambapo alipata heshima katika pande mbili wa watu na kirasmi . Na Ardhi ya Misri ilikuwa yenye ukarimu kwake kama  hali ilivyo katika nchi yake ambapo aliheshimiwa na Waziri Mmisri wa Vyombo vya Habari  mnamo 2008   "  

Kwako  raia wanasogea mbele , wanajikusanaya pamoja na kujiandaa wakasema acha ، acha  na hujaacha badio

  Acha buibui zetu na kanzu zetu, Qurani zetu, misikiti na makanisa yetu, urithi wa mababu zetu , akili za watoto wetu ” Kwa maneno haya, “Mohamed Wardi” alikabiliana na utawala wa khwan wa itikadi kali, akiita  roho wa taifa la Sudan ili kuwakabili wale waliotaka kuunyang'anya Uraia wake, athari yake ya kiutamaduni  na urithi wa ustaarabu wake .. kama kwamba Anaimba kwa sauti ya wanadamu wote dhidi ya wale wanaouza nchi na kununua kwa bei ndogo dini ya Mwenyezi  Mungu. 

Muhammad Wardi aliaga Dunia mnamo 2012 baada ya maisha yalidumu miaka themanini iliyojaa kwa upendo wa nchi , sanaa na maisha, vilevile , alituachia urithi wa kumbukumbu nzuri, kama vile ardhi yake na kama Nile uliokusanyika kusini mwa bonde pamoja na kaskazini .

 chombo cha wakati kilinirudisha  nikajikuta kutamka Ewe eneo  letu .. Ewe zuri zaidi  wacha mioyo yetu ipeperuke..na utuhamishe kati ya kipepeo anayependeza...kati ya Zeinat na Abeer.”..na nikarudi uhalisia, nikimuombea   " Waridi"  Dua  kwa Rehema, nikiwashukuru wale walioamua kumheshimu.