Dkt. Yamana Abdulrahman, Profesa wa Usalama wa Mtandaoni, Kwenye Kitivo cha Kijeshi cha Ujerumani

Dkt. Yamana Abdulrahman, Profesa wa Usalama wa Mtandaoni, Kwenye Kitivo cha Kijeshi cha Ujerumani

Imetafsiriwa na/ Malak Hazem
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

Youmna Ali Abdel Rahman amezaliwa mwaka 1989 mjini Kairo. Alijiunga na Kitivo cha Uhandisi kwenye Chuo Kikuu cha Ujerumani huko Kairo na alipata Shahada yake ya Uhandisi wa Kompyuta mnamo 2010.

Dkt. Youmna Abdulrahman alisafiri kwenda Ujerumani kufanya kazi katika Kitivo cha Uhandisi, Chuo Kikuu cha Stuttgart, huko Ujerumani, na kisha alipata shahada ya uzamili katika uhandisi wa kompyuta na programu kutoka Chuo Kikuu cha Stuttgart, Ujerumani mnamo mwaka 2013. Kisha alipata shahada ya uzamivu katika sayansi ya kompyuta kutoka chuo kikuu hicho hicho mnamo mwaka 2014, kabla ya kuanzisha safari yake ya sasa katika Chuo cha Kijeshi, na Dkt. Youmna anasimamia masomo ya uzamili na udaktari kwa wanafunzi wa kiraia na kijeshi pia.

Youmna alifanya kazi kama mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Bundeswehr, kwenye Munich, huko Ujerumani, wakati wa 2019 na 2020. Yeye ni mhadhirialiyekabidhiwa katika Chuo Kikuu cha Ujerumani mjini Kairo.  

"Abdulrahman" alitengeneza kamera za joto zilizokuwa za jeshi la Ujerumani hapo zamani, zilizoona vitu gizani, ili kuzifanya zipatikane kwa kila mtu katika huduma ya sayansi, haswa kwa kuwa kamera hizi za joto hazikupatikana kwa mtu yeyote kuzinunua miaka 20 iliyopita, na kufuata tu jeshi la Ujerumani wakati huo. Kamera hizi za hali ya juu zinaweza kupima mabadiliko katika mwili wa binadamu, na kutabiri mabadiliko kabla ya kutokea, kulingana na vipimo wanavyofanya kupitia kamera hizi, kwa kuchambua data ya picha. Kamera pia ina "software" yenye rangi kadhaa, kila rangi inahusika na kubadilisha na kupima joto la ndani la mwili, na saizi ya kamera ni ndogo sana, inaweza kufichwa mfukoni. Inaweza kutumika kwa matibabu katika kutambua hali ya afya ya mtu, na data ya joto lake na mabadiliko yanayotokea ndani, hasa katika vyumba vya huduma kubwa, na pia katika shughuli za usalama, hivyo kesi za ukweli na uongo zinaweza kujulikana kupitia mabadiliko haya mbalimbali, pamoja na kutambua takwimu za kigaidi katika uvamizi, kupitia ishara zake za mafadhaiko, kamera inazoweza pia kupima, na pia wakati wa kazi katika viwanja vya ndege, walanguzi na wengine wanaweza kugunduliwa.

Kamera pia inaweza kupima vigeu vya uso, na inaweza kujua kinachotokea ndani, na ikiwa mtu huyo ana furaha, ana shida, hatia au afueni.

Dkt. Youmna alifanya kazi kwa miaka mitatu na Idara ya Moto ya Ujerumani kuunganisha na kuendeleza matumizi ya kamera ya joto ili kuokoa maisha ya binadamu, ili uweze kujua mahali pa moto zaidi, pamoja na kujua maeneo ya watu kuwaokoa, wakati ambapo alifanikiwa kuunganisha kamera hiyo kwa njia ya juu kwenye kofia yake.

Dkt. Youmna alishiriki katika vikao vingi vya kimataifa, mikutano na mashindano hadi utafiti wake ulichaguliwa kati ya karatasi tano za juu za utafiti ulimwenguni katika uwanja wa teknolojia. Alichaguliwa na Taasisi ya MIT, ni taasisi kubwa zaidi ya teknolojia duniani, na nafasi kama shule ya kwanza ya teknolojia duniani kati ya watafiti wa juu wa wanawake wa 70 duniani katika uwanja wa uhandisi wa elektroniki.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy