Abdulrazak Gurnah
Ni mwandishi wa riwaya kutoka Tanzania anayeishi nchini Uingereza. Amezaliwa tarehe 20 Desemba, mwaka 1948 katika visiwa vya Zanzibar.
Alisafiri kwenda Uingereza mwaka 1968, miaka saba baada ya nchi yake ya Tanzania kupata uhuru, na mpaka sasa anaendelea kuishi Uingereza, ambako hivi karibuni amestaafu kama Profesa wa Fasihi katika Chuo Kikuu cha Kent.
Mbali na kufundisha, Gurnah amekuwa pia akifanya kazi za uhariri wa nyaraka mbalimbali, vitabu na majarida, na kwa sasa ni mhariri wa jarida maarufu la Wasafiri.
Mbali na Tuzo ya Nobel, pia amewahi kushinda Tuzo ya Booker Prize for Fiction mwaka 1994, Times Book Prize (Fiction) mjini Los Angeles mwaka 2001, na Commonwealth Writers’ Prize (Eurasia Region, Best Book) mwaka 2006.
Abdulrazak Gurnah ni mmoja wa Waafrika wachache waliowahi kushinda Tuzo ya Nobel katika historia tangu kuanzishwa kwake mwaka 1901.
Hadi sasa amechapisha riwaya 10 ambazo ni:
The Last Gift (2011),
The Cambridge Companion to Salman Rushdie (2007),
Desertion (2005),
By the Sea (2001),
Admiring Silence (1996),
Paradise (1994),
Essays in African Literature: A Re-evaluation (1993),
Dottie (1990),
Pilgrim’s Way (1988),
Memory of Departure (1987).