Misri yaendelee na Afrika yaendelee .. Mwaka mmoja wa kazi madhubuti

Misri yaendelee na Afrika yaendelee .. Mwaka mmoja wa kazi madhubuti

Imeundwa na / Kitengo cha Tafiti za Ofisi ya Vijana wa Afrika-Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri

Imefasiriwa na / Ali Mahmoud

Utangulizi:

Kulingana na ujihusishaji wa Misri kwa mazingira yake ya kiafrika, na kuamini kwake kwamba utulivu wa Bara la Afrika uko miongoni mwa vipaumbele vya sera za kigeni za Misri, Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika ulikuja, kuelezea mambo yale ya kudumu yaliyounda sera ya kigeni ya Misri kuelekea Bara la Afrika, kwa njia inayoongeza hadhi kubwa ya Kairo kati ya ndugu wa Afrika,  iliyoongezeka sana wakati wa Rais El-Sisi aliposhika madaraka, mwaka mzima umepita tangu Rais Abdel Fattah El-Sisi aliposhika Urais wa Umoja wa Afrika katika Mkutano wa Kilele wa Addis Ababa, mnamo  Februari 2019, na kupitia Urais wake wa Umoja wa Afrika, Misri imeshughulikia na jukumu hili kama Imani kwamba inathamini viongozi wa nchi za Afrika nchini Misri na uongozi wake, wakati huo huo, kama jukumu ambalo inapaswa kutimiza kuelekea Bara na watu wake, na hii ni mara ya nne katika historia ambapo Misri imebeba bendera ya Bara la Afrika, na ya kwanza kwa jina jipya la Shirika kubwa zaidi Barani Afrika, "Umoja wa Afrika", ambapo Misri imechukua kiti cha uongozi mara tatu hapo awali, zote zilikuwa baada ya Umoja wa Afrika kuitwa Shirika la "Umoja wa Afrika".

Katika muktadha huu, na mnamo kipindi cha mwaka huu, uongozi wa Misri umetenda kwa zaidi ya ngazi moja kwa maslahi ya watu wa Afrika, na kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano kati ya Misri na nchi za Afrika, na kati ya watu wa Afrika pomoja.

Misri ilichukua Urais wa Umoja wa Afrika mnamo Februari 10, 2019 kwa mara ya nne katika historia yake, na ya kwanza kwake kwa jina jipya "Umoja wa Afrika", ambapo Misri imechukua kiti cha uongozi mara tatu kabla, kama Misri inazingatiwa moja ya nchi zilizoanzisha Shirika la Umoja wa Afrika, Rais Abdel Fattah El-Sisi, katika hotuba yake katika Mkutano wa Kilele wa Afrika, uliofanyika katika Mji Mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, kwamba Misri itafanya kazi kwa bidii ili kuendelea na njia kwa ajili ya mageuzi ya kimuundo na kifedha ya Umoja huo na kukamilisha mafanikio yaliyotimizwa ili kuunganisha umiliki wa nchi wanachama wa Shirika lao la bara na kujitahidi kuendeleza zana na uwezo wa Umoja huo na kamisheni zake kukidhi matarajio ya watu wa Afrika.

Tangu kushika Urais wa Umoja wa Afrika, Rais Abdel Fattah El-Sisi ameshiriki katika mikutano na makongamano mengi ya kilele ya kimataifa, ambayo aliongoza baadhi ya mikutano hiyo kwa ushiriki wa viongozi wa ulimwengu huko mabara 4 nayo ni Ulaya, Asia, Afrika na Marekani ya Kaskazini, na katika mikutano hii yote alikuwa mtetezi hodari na wazi katika kudai haki za watu wa Afrika kwa amani, utulivu, maendeleo na ustawi, ambapo alisema kuwa  mnam 2019  watashughulikia zaidi kuimarisha mifumo ya maendeleo endelevu kutoa fursa zaidi za kazi kwa vijana wa Afrika, akisema kwamba Bara la Afrika linaahidi fursa nyingi, na mapato ya Maendeleo lazima yafikie sehemu zote za Bara kwa njia ya haki.

Kwa hivyo, Baada ya Mkutano wa Kilele wa Afrika, Rais Abdel Fattah El-Sisi alikuwa kwenye jukwaa la Mkutano wa Usalama wa Munich huko Ujerumani kwa ajili ya Amani Barani Afrika, kisha kwenye Mkutano wa Kilele wa Afrika-Ulaya huko Austria, kisha kwenye Jukwaa la China-Afrika huko Beijing, kisha kwenye Mkutano wa Kilele wa Japan-Afrika (TICAD) huko Tokyo, Mkutano wa Kilele wa Nchi Saba za Viwanda huko Paris, Mkutano wa Kilele wa Kundi la Nchi Ishirini Kubwa huko Osaka, Japan, kisha katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kisha Mkutano wa Kilele wa Ushirikiano kati ya Kundi la Ishirini na Afrika nchini Ujerumani, kisha Mkutano wa Kilele wa Afrika - Urusi huko Sochi, kisha Mkutano wa Kilele wa Uingereza - Afrika wa Uwekezaji huko London (Januari 2020) na kwa hivyo, katika vikao hivi vyote na vingine vya kimataifa, Rais Abdel Fattah El-Sisi alikuwa msemaji bora wa masuala ya Bara la Afrika na mtetezi wa haki zake na masilahi zake.

Kwa hiyo, jukumu la Misri linaweza kuangaziwa kupitia Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika kupitia mada tatu:

Mada ya kwanza: kuimarisha Amani na Usalama Barani Afrika.

Mada ya pili: katika ngazi ya Kiafrika-Kiafrika

Mada ya tatu: Mahusiano kati ya Misri na Watu wa Afrika

{Mada ya Kwanza}: kuimarisha Amani na Usalama Barani Afrika:

Rais alifanya juhudi wakati wa mikutano ya nchi mbili na ya Pamoja za Afrika, ikiwa ni pamoja na Jukumu la Misri katika kuunganisha Kenya na Somalia, na vile vile msaada wa Rais El-Sisi kwa mpango wa kunyamazisha bunduki katika Bara la Afrika (2020), pamoja na Jukumu lenye manufaa la Misri katika maendeleo yaliyoshuhudiwa na Sudan, na vile vile juhudi za Misri za utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa sasa Nchini Libya, inaweza kuangazia jukumu la Misri katika kukuza Amani na Usalama Barani Afrika kupitia:

Mkutano wa Usalama wa Munich mnamo Februari 15, 2019:

Rais El-Sisi alitoa hotuba wakati wa kikao kikuu cha mkutano huo na ushiriki wa Kansela wa Ujerumani, kuwa Rais wa kwanza wa Nchi isiyo ya Ulaya anayeshiriki katika kikao kikuu tangu kuanzishwa kwa mkutano huo mnamo mwaka wa 1963, na Rais aliwasilisha maoni ya Misri ya kuimarisha hatua za kiafrika katika hatua inayofuata, kwa kuzingatia Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika, kupitia kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda katika ngazi ya Bara, kuwezesha harakati za biashara za ndani, ndani ya mfumo wa Ajenda ya Afrika ya 2063 kwa maendeleo ya kina na endelevu pamoja na kuimarisha juhudi za ujenzi upya na maendeleo baada ya migogoro.

Mkutano wa Wawakilishi wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini:

Misri ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa Manaibu Wakuu katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika kipindi cha kuanzia Februari 20 hadi 23, Rais Abdel Fattah El-Sisi alisisitiza umuhimu wa jukumu la Jumuiya ya Wawakilishi wa Afrika katika kufanya kazi ili kuongeza ufanisi wa huduma za mashtaka katika Bara na kujenga uwezo wa wanachama wake, akiashiria uungaji mkono wa Misri kwa jukumu la Jumuiya hiyo chini ya Urais wa Sasa wa Misri wa Umoja wa Afrika, kwa kuzingatia kwamba kukuza hatua ya Pamoja ya Afrika ni moja ya vipaumbele vya Urais wa Misri wa Umoja huo.

Katika muktadha huu, Rais alipitisha maoni ya Misri ya kupambana na ugaidi,  inayotegemea kushughulikia hali hii katika nyanja zake zote, zikiwemo za kiusalama, kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiakili na kidini, pamoja na kupambana na taratibu za ufadhili na msaada wa kisiasa na vyombo vya habari kwa makundi ya kigaidi, akisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi za Jumuiya ya kimataifa kuzuia unyonyaji wa ugaidi kwa maendeleo ya habari na kiteknolojia.

Mkutano wa Kilele wa Troika na “Kamati ya Libya” Aprili 23, 2019:

Mkutano huo wa Kilele ulijadili maendeleo ya hivi karibuni katika uwanja wa Libya na njia za kudhibiti mgogoro huo, kufufua mchakato wa kisiasa Nchini Libya na kuondoa ugaidi, na hili kwa ushiriki wa marais wa Rwanda na Afrika Kusini, wanachama wawili wa Troika ya Utawala wa Umoja, Rais wa Congo kama Mwenyekiti wa Kamati ya Libya katika Umoja huo, pamoja na ushiriki wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Mkutano wa Kilele wa Mashauriano wa washirika wa Kikanda kwa Sudan Aprili 23:

Nchi zinazoshiriki zilithibitisha tena kanuni na malengo ya Umoja wa Afrika kuelekea kuimarisha Amani, Usalama na Utulivu Barani, pia zilithibitisha kujitolea kwao kwa umoja, uhuru, uadilifu na mshikamano wa Sudan na usalama wa ardhi yake na zilielezea msaada wao kamili kwa jukumu la Umoja wa Afrika,”IGAD” na nchi jirani katika kuunga mkono Juhudi za Sudan kushinda changamoto za kisiasa, kiusalama na kiuchumi inayokabiliwa nazo, nchi zinazoshiriki pia zilimhimiza Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja kuendelea na mazungumzo na mamlaka ya Sudan na vyama vya Sudan na ziliita Sudan kuendana na ushirikiano wake wenye manufaa na Umoja wa Afrika na Kamisheni yake, nchi zinazoshiriki pia zilihimiza jumuiya ya kimataifa kuendelea na msaada wake na kutoa misaada ya haraka ya kiuchumi kwa Sudan kutokana na kuzorota kwa hali za kiuchumi, na zilisisitiza umuhimu wa msamaha wa haraka kwa madeni ya Sudan.

Mkutano wa Kilele wa Ukanda na Barabara jijini Beijing katika Aprili 24, 2019 nchini Uchina:

Rais aliongea kwa niaba ya Afrika, akitaka ushirikiano zaidi katika nyanja za miundombinu na maendeleo ya kiuchumi.

Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo wa Maendeleo ya Afrika "TICAD":

Japan imeandaa mkutano wa kilele wa ngazi ya juu kusaidia Afrika na matarajio yake ya maendeleo, kikao cha saba cha Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo ya Maendeleo ya Afrika “TICAD” ulifanyika katika Mji wa Kijapani wa Yokohama kutoka katika kipindi cha kuanzia Agosti 28 hadi 30, 2019 chini ya uenyekiti wa pamoja wa Japan na Misri, Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, na kwa ushiriki wa marais wa nchi za Afrika, idadi ya mashirika na taasisi za kimataifa, zikiongozwa na Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia.

Katika muktadha huu, lengo linalotarajiwa kutoka kufanyika kwa mkutano huu wa kilele ni kuimarisha mazungumzo ya kisiasa kati ya Afrika na washirika wake wa maendeleo.

Mkutano wa Kilele wa 14 wa Kundi la Nchi Ishirini:

Rais El-Sisi alishiriki katika shughuli za Mkutano wa Kilele wa 14 wa Kundi la Nchi Ishirini huko jijini Osaka, Japan, uliofanyika mnamo Juni 28 na 29, baada ya mwaliko ulitolewa kwa Misri kutoka kwa Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, kushiriki katika mkutano huo wa kilele, kulingana na nafasi ya Misri katika Afrika, na Urais wake wa Umoja wa Afrika, Rais El-Sisi pia alishiriki katika mkutano mdogo wa uratibu wa Afrika pembezoni mwa shughuli za Mkutano wa Kilele wa Kundi la Ishirini, uliojumuisha Rais wa Afrika Kusini "Cyril Ramaphosa" na Rais wa Senegal "Macky Sall" imekubaliwa, wakati wa mkutano mdogo huo wa kilele, kufanya kazi kuangazia vipaumbele vya maendeleo ya nchi za Afrika mbele ya washirika wakati wa mikutano ya Kundi la Ishirini, na kuzingatia katika mfumo huu juu ya Malengo yaliyojumuishwa katika Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063.

{Mada ya Pili}: katika ngazi ya Kiafrika-Kiafrika

Uzinduzi wa Eneo la Mkataba Mkubwa wa Biashara Huria Barani Afrika, ambao ni msukumo mkubwa zaidi wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za Bara hilo, ambapo Mkutano wa Kilele wa Kipekee wa Afrika wa 12, ukiongozwa na Rais Abdel Fattah El-Sisi, ulifanyika katika Mji Mkuu wa Niger, Niamey, mnamo Julai 7 na 8, 2019, na mkutano huo wa kilele ulishuhudia uzinduzi wa Eneo la Mkataba wa Biashara Huria Barani Afrika, Baada ya kukamilisha akidi ya uidhinishaji wa nchi za Afrika, na kuanza kutumika kwa makubaliano hayo.

Jukwaa la Kwanza la Afrika la Kupambana na Ufisadi:

Mnamo Juni 12, 2019, Misri ilikaribisha Jukwaa la Kwanza la Afrika la Kupambana na Ufisadi Barani Afrika chini ya Urais wake wa Umoja wa Afrika, kwa kuzingatia mpango uliozinduliwa na Rais El-Sisi mnamo Januari 2018 wakati wa ushiriki wake katika Mkutano wa Kilele wa kila mwaka wa Viongozi wa Afrika.

Nchi 55 za Afrika na maafisa 200 wa Afrika wa ngazi ya juu, walishiriki katika kongamano hilo, na  hilo lilijadili masuala muhimu, haswa mapitio ya juhudi za kitaifa za kupambana na ufisadi za nchi kadhaa za kiafrika katika utekelezaji wa ahadi za bara na kimataifa, jukumu la kupambana na ufisadi katika maendeleo ya Bara la Afrika, taratibu za kupambana na ufisadi katika ngazi ya Bara na maendeleo ya uwezo wa rasilimali za watu katika nyanja mbalimbali za kupambana na ufisadi katika Bara la Afrika, msaada wa uratibu wa serikali ya ndani ya Afrika katika kupambana na ufisadi, na jukumu la utashi wa kisiasa katika kufanikisha juhudi za kupambana na ufisadi katika Bara la Afrika.

Maadhimisho ya Siku ya Afrika:

Rais El-Sisi alitoa hotuba mnamo Mei 25 kwa kuadhimisha Siku ya Afrika kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuwawezesha vijana wa bara hili kuendana na maendeleo ya nyakati na kutekeleza majukumu yao katika kuongoza mustakabali wa Afrika, pamoja na kuendelea kuimarisha jukumu la mwanamake wa kiafrika kama moyo wa kupiga kwa jamii zao na mwanga wa mabadiliko yao ya kiuchumi na utulivu wao pamoja na kuimarisha mahusiano ya kitamaduni na ustaarabu kati ya watu wake, kuimarisha utambulisho wa kiafrika na kuzingatia misingi ya mshikamano wa Afrika, Rais alionesha katika hotuba yake kuwa hakuna njia yoyote kwetu isipokuwa kufanya juhudi na kushikilia umoja wetu ili kufikia ndoto ya waasisi na matarajio ya watu wakuu wa Afrika katika kuunda Bara thabiti na lenye ustawi ambalo linahakikisha maisha ya staha kwa watoto wake wote, na inatangaza mwanga wa ustaarabu na utamaduni wa uvumilivu na upendo kwa ulimwengu wote.

{Mada ya Tatu}: Mahusiano kati ya Misri na watu wa Afrika:

Misri imefanya juhudi kubwa katika mwelekeo huu, Misri iliandaa Jukwaa la Uwekezaji Barani Afrika, Jukwaa la Uchumi la Kiarabu-Kiafrika, na Aswan ikawa Mji Mkuu wa vijana wa Afrika, na kutoa maagizo kwa mashirika yote ya Serikali ya Misri ili kuimarisha ushirikiano na nchi za kiafrika katika nyanja zote, zilizotekeleza mipango mingi ya ushirikiano katika nyanja zote za uchumi, biashara, kilimo, umwagiliaji, diplomasia, mazingira, vijana, michezo, viwanda, kujenga kada na uwezo wa binadamu, na nyingine.

Misri yaandaa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Soka:
Misri, chini ya Urais wake wa Umoja wa Afrika, iliandaa Kombe la Mataifa ya Afrika, ambalo Cameroon ilipangwa kulikaribisha katikati mwa Bara la Afrika, lakini kutokamilika kwa maandalizi ya Cameroon kuandaa tukio kubwa zaidi la michezo katika Bara la Afrika, lilisababisha Shirikisho la Soka la Afrika "CAF" kuondoa maandalizi haya kutoka kwake, na kuiridhisha kwa kuandaa toleo linalofuata la 2021, na uhamisho wa maandalizi yaliyopangwa hapo awali huko Cote d’Ivoire na Guinea hadi miaka miwili ya 2023 na 2025.
 
Katika muktadha huu, Misri imeandaa Mashindano ya Mataifa ya Afrika katika mara nne zilizopita, kuanzia Mwaka wa 1959 kupitia matoleo mawili ya 1974 na 1986 kuishia na mashindano ya Mwaka wa 2006, maandalizi ya Misri kwa mashindano haya hayajawahi kukutana na Urais wa Umoja wa Afrika, lakini hii ni mara ya kwanza katika historia, ambapo Misri ilichanganya maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika na Urais wa shirika la Umoja wa Afrika, ili Misri ichukue nafasi ya kuongoza katika ngazi ya kisiasa na pia kuongeza kwake uwanja wa michezo.

Kuandaa mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 23, Misri ilikuwa na uwezo na jukumu na ilishangaza dunia tena, kwa maandalizi mazuri ya mashindano ambayo Mafarao walipata taji lake, ambapo Timu ya Taifa ya Olimpiki ya Misri ilitimiza mafanikio ya kihistoria mnamo mwaka wa 2019, baada ya kufanikiwa kushinda taji la Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 kwa mara ya kwanza katika historia yake, na ilifikia kwa Michezo ya Olimpiki (Tokyo 2020) kwa mara ya 12 katika historia yake, na ya kwanza tangu toleo la mashindano huko London 2012.

Jukwaa la Aswan la Amani na Maendeleo Endelevu:

Rais Abdel Fattah El-Sisi alizindua katika Mkutano wa Kilele wa Sochi nchi ya Shirikisho ya Urusi kufanya toleo la kwanza la Jukwaa la Aswan la Amani na Maendeleo Endelevu, ndani ya mfumo wa Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika 2019, kufungua peo mpya kuelekea kufikia Amani na Maendeleo Endelevu katika Bara la Afrika.

Jukwaa hilo lilifanyika mnamo Desemba 11, kwa lengo la kutoa wito kwa uwekezaji wa rasilimali nyingi za Bara la Afrika na kuzibadilisha kuwa thamani ya ziada sambamba na maendeleo ya miundombinu yake, ambayo inamaanisha kutengeneza njia ya kufikia maendeleo endelevu, na lengo la kuunganisha Amani na kufikia Maendeleo Endelevu ni kuhimiza na kuhamasisha Taasisi za Fedha za Kimataifa kusaidia na kufadhili miradi ya maendeleo barani Afrika na kuvutia uwekezaji kwake, na hii ni kwa maslahi ya umma ya Bara kupitia ufikiaji wa bidhaa zake kwa Ulaya na kinyume chake kupitia Lango la Misri.

Mkutano wa Vijana wa Kiarabu na Kiafrika:

Mkutano wa Vijana wa Kiarabu na Kiafrika, ulioandaliwa na Aswan mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 16 hadi 18 Machi 2019 ulizinduliwa pamoja na uangalizi wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, kwa ushiriki wa zaidi ya Vijana 1,500 wa Kiafrika na Kiarabu kujadili masuala na changamoto za Bara la Afrika na Eneo la kiarabu, Rais alithibitisha wakati wa mkutano huo kwamba wazo la Jukwaa la Vijana Ulimwenguni lilikuja kuwasiliana na aina zote za vijana ili tusikie na kuzungumza sisi kwa sisi, akisisitiza umuhimu wa kuendelea na mikutano hii na kwamba ziwe katika vipindi vya karibu ili lengo linalotarajiwa liweze kuamuliwa.

Jukwaa hilo lilijumuisha shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kikao cha majadiliano "Mustakabali wa Utafiti wa Kisayansi na Huduma za Afya", kikao cha meza ya pande zote na kichwa cha "Bonde la Nile ni Njia ya Ujumuishaji wa Kiafrika na Kiarabu", mkutano huo pia ulijumuisha semina juu ya "Maendeleo ya Eneo la Pwani ya Afrika”, pamoja na kufanya semina mbili za ujasiriamali, moja yao ni yenye kichwa "Jinsi ya kuwa Mjasiriamali aliyefanikiwa", na nyingine yenye kichwa "Ujasiriamali wa Jamii kutoka kwa Mtazamo wa Kiafrika".

Katika uwanja wa Miundombinu, Usafiri na Mawasiliano
Miradi ya kuunganisha Misri na nchi za Bara la Afrika ilikuja na juu ya miradi ya miundombinu (Mradi wa Kairo – Cape Town), pamoja na Mradi wa Uunganisho wa Umeme kati ya Misri na nchi za mabara mawili ya Afrika na Ulaya, kwa kusambaza umeme kwa nchi za mabara mawili kupitia minara ya chuma inayovuka mipaka, na Mradi wa Uunganisho wa Maji (Alexandria – Victoria) nao ni mradi wa kuunganisha maji kati ya Ziwa la Victoria lililopo Afrika na maji ya Bahari ya Mediterania huko Misri, na mradi huo unachangia kwa kazi ya ufufuo wa kikanda kwa nchi zote za Bonde la Mto Nile.

Katika muktadha huu, Misri imechangia kuanzishwa kwa Mfuko wa Uwekezaji wa Miundombinu ya Habari kwa lengo la kusaidia maendeleo ya kiteknolojia na mabadiliko ya kidijitali katika Bara, ili kujenga uchumi wa kisasa kulingana na mifumo ya hivi karibuni ya kiteknolojia, na Mamlaka Kuu ya uwekezaji na Maeneo Huria na Tume ya Uwekezaji ya Ethiopia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia zilisaini mkataba wa makubaliano katika uwanja wa kuimarisha uhusiano wa uwekezaji wa nchi mbili.

Katika Ngazi ya Afya :
Misri imechukua uenyekiti wa Kamati Maalum ya Kiufundi ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya katika Umoja wa Afrika, sambamba na mipango iliyozinduliwa na Rais Abdel Fattah El-Sisi katika uwanja wa Afya inayolenga kupambana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, haswa Mpango wa "Afya Milioni 100", uliojumuisha uchunguzi wa wakaazi wasio Wamisri, Misri pia inakusudia kuanzisha kituo cha kikanda kusaidia mipango ya afya ya umma kitakachopatikana Kairo, ili kuamsha mipango ya afya ya umma katika nchi za kiafrika; kuondoa magonjwa na magonjwa ya milipuko ambayo yanaleta mzigo mkubwa kwa nchi ndugu za kiafrika.

Mikutano na Viongozi wa Afrika:

Rais El-Sisi alianza ziara zake kwa Nchi za Afrika mnamo tarehe ya Februari 9, kwa ziara ya kihistoria kwa Mji Mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ambapo ulishuhudia kupokea kwake kwa Urais wa Umoja wa Afrika, Urais wake wa kazi za kikao cha kawaida cha 32 cha mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi na serikali za Afrika za Umoja wa Afrika, na katika muktadha huu, Rais El-Sisi alianza katika tarehe ya Aprili 7 ziara ya kigeni ambayo ilijumuisha ziara ya Guinea, Cote d’Ivoire na Senegal, ndani ya mfumo wa nia ya Misri ya kuimarisha mawasiliano na uratibu na ndugu zake wa Afrika, kuendelea kuimarisha mahusiano yake na nchi za Bara katika nyanja mbalimbali.

Pembezoni mwa ushiriki wake katika shughuli za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo mwezi wa Septemba, Rais El-Sisi alishiriki katika Mkutano wa Kilele wa pande tatu ambao ulijumuisha Mohamed Abdullah Farmajo, Rais wa Jamhuri ya Somalia, na Uhuru Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya, kujadili baadhi ya masuala yenye utata kati ya pande hizo mbili.
Mnamo Juni 9, Rais El-Sisi alimpokea Rais Isaias Afwerki, Rais wa nchi ya Eritrea, kwa nia ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Eritrea, Rais alisisitiza umuhimu wa kusonga mbele katika kuunda mipango maalum ya maendeleo ya miradi ya ushirikiano wa nchi mbili kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali na kushinda vikwazo vyote, haswa katika sekta za miundombinu, umeme, afya, biashara, uwekezaji, kilimo, mifugo na uvuvi, pamoja na kuimarisha mipango ya msaada wa kiufundi iliyotolewa kwa upande wa Eritrea kupitia Shirika la Misri la Ushirikiano kwa Ajili ya Maendeleo.

Pamoja na mikutano na idadi ya marais na viongozi wa Bara la Afrika, wakiwemo Felipe Jacinto Nyusi, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini, Rais wa Chad, na Rais wa Jamhuri ya Comoro, kujadili njia za kuimarisha ushirikiano, mashauriano na uratibu kuelekea njia za masuala ya Afrika yenye maslahi ya pamoja na juhudi za kupambana na ugaidi, na njia za kuimarisha mahusiano ya nchi mbili katika ngazi mbalimbali.

Kutokana na Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika, viongozi na marais wengi wa Nchi za Afrika walitembelea Kairo, akiwemo Moussa Fakih, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, ambaye alikutana na Rais El-Sisi pembezoni mwa kufanyika kwa Jukwaa la Vijana wa Kiarabu na Kiafrika huko Aswan, kwa kuthibitisha umuhimu wa Shirika la Umoja wa Afrika la Maendeleo “NEPAD”, na kutoka kwwa kuzingatia ukweli wa kwamba Misri ni moja ya nchi zilizoanzilisha mpango huo, Rais El-Sisi alipokea katika tarehe Mei 8, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, na mkutano huo ulishuhudia makubaliano juu ya kuimarisha Ushirikiano kati ya pande hizo mbili kusaidia mipango ya NEPAD inayolenga kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na ushirikiano wa kikanda barani Afrika.

Hitimisho:

Misri imetimiza kile ambacho Rais Abdel Fattah El-Sisi aliahidi katika hotuba yake katika Mkutano wa Kilele wa Afrika, uliofanyika katika Mji Mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ambapo Misri ilichukua Urais wa Umoja, itafanya kazi kwa bidii ili kuendelea na njia kwa ajili ya mageuzi ya kimuundo na kifedha ya Umoja na kukamilisha mafanikio yaliyopatikana ili kuimarisha umiliki wa nchi wanachama wa shirika lao la bara na kuelekea kuendeleza zana na uwezo wa Umoja na kamisheni zake ili kukidhi matarajio ya watu wa Afrika, na kuimarisha mifumo ya Maendeleo Endelevu kutoa fursa zaidi za ajira kwa vijana wa Afrika.

Misri imepata matokeo mengi ya kuvutia katika ngazi za kikanda na kimataifa, ambalo lilisifiwa na nchi wanachama wa Umoja na maafisa wakuu wa muundo wake wa kiutawala, ambapo Misri ilithibitisha tena kanuni na malengo ya Umoja wa Afrika kuelekea kuimarisha amani, usalama na utulivu katika Bara, Rais El-Sisi hakuondoka kwenye jukwaa lolote la kimataifa bila kushiriki katika jukwaa hili na alishiriki akibeba wasiwasi na matumaini ya watu wa Bara kwa maisha mema, na kupata haki yao katika maendeleo endelevu na fursa za kazi, pamoja na mwaliko wake kwa wafanyabiashara na makampuni makubwa ya kimataifa kuwekeza katika Afrika, kwa sababu ya fursa na faida nyingi zinazopatikana huko, ikiwa ni pamoja na maliasili na wafanyakazi.

Mbali na kuendelea kuimarisha jukumu la mwanamke wa kiafrika kama moyo unaopiga kwa jamii zao na mwanga wa mabadiliko yao ya kiuchumi na utulivu wao, pamoja na kuimarisha mahusiano ya kiutamaduni na ustaarabu kati ya watu wao, kuimarisha utambulisho wa kiafrika na kudumisha kanuni za mshikamano wa Afrika.

Orodha ya Marejeleo ya Mwisho:

Kwanza: Marejeleo katika Kiarabu:

Fatma Hassan, “ Mavuno ya 2019..Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika”, Mamlaka ya Taifa ya Vyombo vya Habari, inapatikana katika kiungo kifuatacho www.maspero.eg

“Urais wa Umoja wa Afrika”, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, inapatikana katika kiungo kifuatacho www.mfa.gov.eg

“Urais wa Umoja wa Afrika unahamia Misri kwa mara ya kwanza katika historia ya Shirika”, inapatikana katika kiungo kifuatacho: www.france24.com

“Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika 2019”, Taasisi  Kuu ya Habari, inapatikana kwenye kiungo kifuatacho: www.sis.gov.eg

Pili: Marejeleo katika Kiingereza:

Diaa Rashwan, "Egypt president of the African Union .. the possible and hoped” (Issue47,2018), Available at: www.africa.sis.gov.eg

“Egypt to Hand African Union Presidency to South Africa in February”, Asharq Al-Awsat, Available at: https://aawsat.com

Christin Roby, “What will Egypt focus on as African Union chair?”, Available at: www.devex.com/new

Amr Mohamed Kandil, “Sisi hands over African Union presidency to South Africa”, Available at: www.egypttoday.com