Hapa Misri, Twahisi undugu wa Uarabuni na Lebanon Ndugu
Imefasiriwa na / Alaa Zaki
Nafurahi sana kwa fursa hii inayowakusanya vijana wa Misri na vijana wa Lebanon na washauri wa vijana wa Lebanon, ili wahisi undugu unaowaunganisha watu wa Lebanon na ndugu zao miongoni mwa watu wa Misri, na ninafurahi kuwa ziara hizi zinaendelea na zinalenga manufaa ya pamoja ya ulimwengu wa Kiarabu.
Ujumbe unaokuwa jukumu lenu ni mkuu kuliko ujumbe wetu, kwa sababu mnahisi hisia halisi zinazotoka kwa watu wa Misri, hivyo mnarudi mkibeba undugu wa kweli ulioupata Misri na wana wa Misri, na hili litakuwa jambo kuu zaidi katika kuimarisha muungano wa moyo na kiroho. Muungano huo ni uzio wetu ambapo nguvu zetu na msaada wetu kwa kila mmoja dhidi ya matarajio ya ulimwengu unawakilishwa.
Hapa Misri, Twahisi undugu wa Uarabuni na Lebanon ndugu yetu, na tuko hapa kama maafisa nchini Misri tunafanya kazi ili kuimarisha uhusiano huo, kwa njia ya kuwapeleka ndugu zenu kutoka hapa ili wakujue huko Lebanon. Na tunatumaini kuwa ziara hizi zitarudiwa na mnaiita, kwa sababu inalinda ulimwengu wa Kiarabu kutokana na utawala wa kigeni, inaimarisha ulimwengu wa Kiarabu na kuongeza viungo vyake vyote.
Ziara zenu za mara kwa mara zinaimarisha Lebanon na Misri, na hilo ndilo kusudi la juu kabisa ambalo nyote mnaweza kulifanyia kazi. Natumaini kuwa idadi yenu itaongezeka katika ziara zijazo. Mpaka athari za undugu huu na uunganishaji zionekane katika ulimwengu wa Kiarabu, vipengele vya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni vinavyosaidia katika kuanzisha ulimwengu mkubwa wa Kiarabu vitaongezeka.
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika ujumbe wa walimu wa Lebanon.
Mnamo Machi 4, 1956.