Serikali ya Libya yampa heshima Mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana pembezoni mwa mkutano wa "Locomotive of Social Peace and Ensuring Peace" huko mji mkuu Tripoli

Serikali ya Libya yampa heshima Mwanachama wa Harakati  ya Nasser kwa Vijana pembezoni mwa mkutano wa "Locomotive of Social Peace and Ensuring Peace" huko mji mkuu Tripoli

Imefasiriwa na / Mervat Sakr

Serikali ya Libya ilimheshimu Mhandisi Mohamed Haroun, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na Mwanachama wa Harakati ya  Nasser kwa Vijana  huko Chad kwa kutambua juhudi zake katika nyanja za maendeleo, utatuzi wa migogoro na ujenzi wa amani katika jamii za Kiafrika ndani ya mfumo wa jukumu lake kama Mwenyekiti wa Rasilimali Watu na Mamlaka ya Sayansi ya Teknolojia ya Kisasa ya Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Afrika, na hii ilikuja wakati wa kuhitimisha Mkutano wa Asasi za Kiraia uliofanyika katika mji mkuu Tripoli kutoka 6 hadi 9 Machi, ukiwa na kichwa cha "Locomotive of Social Peace and Ensuring Peace".

Kwa upande wake, Mohamed Haroun alisema kuwa Baraza ni chombo cha ushauri kwa Muungano, na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika, na linalenga kuwekeza utaalamu wa asasi za kiraia na kutetea sauti yake kwa kutoa ushauri ndani ya taasisi za Umoja wa Afrika na michakato ya kufanya maamuzi, ili kujadili taratibu za kutafsiri malengo, kanuni na sera za Muungano katika mipango bora na inayoonekana katika nchi zote za bara hilo, akieleza kuwa Mamlaka ya Rasilimali Watu na Sayansi ya Teknolojia ya Habari ya Kisasa inazingatia masuala manne ya kimsingi nayo ni : Sayansi za Teknolojia ya Habari, Nyanja za Ukuaji na Elimu, pamoja na kuimarisha jukumu la vijana, na kuwekeza katika rasilimali watu.

Katika muktadha unaohusiana, Hassan Ghazaly, Mwanzilishi na Mratibu Mkuu wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, alisisitiza uongozi wa jukumu lililotekelezwa na wanachama wa Harakati ya Nasser  kwa Vijana nchini Chad katika ngazi za kitaifa, kikanda na kimataifa katika nyanja za mafunzo, ukarabati na ujasiriamali, kupambana na rushwa, na kuimarisha jukumu la vijana na wanawake katika nyanja za Amani na Usalama, akieleza kuwa juhudi hizo zimepata mwangwi wa kimataifa na kufikia kilele cha tuzo na heshima kadhaa ndani na kimataifa.