Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa akutana na Balozi wa Jamhuri ya Malawi nchini Misri

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa akutana na Balozi wa Jamhuri ya Malawi nchini Misri

Balozi wa Jamhuri ya Malawi nchini Misri, Bi.Catherin Kongi amempokea Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, toleo la tatu, Godfrey Jenner Malungu, aliyeshiriki kwa njia bora zaidi na maarufu wakati wa shughuli za Udhamini huo, mkutano huo ulishughulikia kuelezea Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, na kujadili na kutafuta uwezekano wa kuanzisha na kutekeleza programu wa kubadilishana kati ya vijana wa Misri na Malawi, ili kuimarisha mahusiano ya nchi mbili kati ya Misri na Malawi kupitia viongozi  vijana na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.

Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri imepanga shughuli za Udhamini huo pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na viongozi wa vijana 150 kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki walishirika katika mpangilio huo mnamo kipindi cha kuanzia 31 Mei hadi 17 Juni, 2022 katika Shirika la Uhandisi huko Kairo.

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuhamisha uzoefu mkale wa kimisri katika kuanzishwa na kujenga taasisi za kitaifa, pamoja na kuunda kizazi cha viongozi wa vijana kutoka Nchi Zisizofungamana kwa upande wowote wenye maoni yanayolingana na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza ufahamu kwa jukumu la Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote kihistoria na jukumu lake mnamo siku zijazo, pamoja na kuamsha jukumu la Mtandao wa Vijana wa Nchi Wanachama Pamoja na Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote NYM, na kuunganisha viongozi wa vijana wenye athari kubwa katika kiwango cha nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki.

Pamoja na kutoa fursa sawa kwa jinsia zote mbili kama lengo la tano la malengo ya Maendeleo endelevu linavyoainishwa hivyo 2030, pia unatoa fursa kwa watenda kwa bidii kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni kuchangamana na kufanya mashirikiano katika nyanja mbalimbali, si tu Barani , bali pia kiwango cha kimataifa, kama lengo la kumi na saba la malengo ya Maendeleo Endelevu linavyoainishwa hivyo.