Sikukuu ya machipuko ni Sikukuu ya kitaifa inayounganisha Wamisri wote

Imefasiriwa na / Fatma Mahmoud
Sikukuu ya machipuko inakuja kutangaza mwanzo wa majira ya kuchipuka, nalo ni tamasha la kimisri na la kitaifa linalosherehekwa na Wamisri wakiwamo Waislamu na Wakristo. nayo ni sikukuu ya kitaifa inayowaunganishana na kuwashikamana tena, kwa hiyo mara nyingi iko kama mapumziko na inabahatika iwe siku ya pili ya Pasaka yaani siku inayofuata Sikukuu ya Pasaka na historia yake ilianzia tangu zama za kale za kimisri pamoja na kuhusishwa na uwanja wa Kilimo nchini Misri.
Ambapo Tarehe yake ilihesabiwa na Wamisri wa kale bila kuhesabu Pasaka, mnamo siku ya kwanza ya Pentekoste, iliyoambatana na siku iliyofuata Pasaka moja kwa moja .
Kulingana na rekodi zilizoandikwa na Plutarch wakati wa karne ya kwanza, ambapo Wamisri wa kale walisherehekea Sikukuu ya pasaka wakati wa enzi ya Mafarao (takribani 2700 ) na sherehe hiyo iliendelea wakati wa enzi ya Ptolemies na Warumi hadi Enzi za Kati, na baada ya Misri kujiunga katika Kikristo, tamasha hilo liliambatanishwa na tamasha lingine la machipuko la Kikristo, ambayo ni Jumapili inayoitwa Pasaka, na kwa hiyo Jumatatu ya Pasaka ambayo ni Sikukuu ya machipuko na hivyo kulingana na mtindo wa Kikristo ya Mashariki kwa takwimu inayotumiwa na Kanisa la Coptic Orthodox, ambalo ni madhehebu makubwa zaidi ya Kikristo nchini .
kwa kufikia wakati wa ushindi wa Kiislamu nchini Misri, Waislamu walitafutia kwa kina tarehe ya Sikukuu ya Pasaka kihistoria, na imeshahakikishwa kutoka kwa tarehe yake, ambayo ni kama tulivyotaja, siku iliyofuata Siku ya pasaka na kwa wakati, imekuwa sikukuu ya kitaifa inayotuunganisha kama wamisri sawa ni wakiristo au waislamu, na njia za kusherehekea zilikuwa tofauti hadi zikafanana kwa jinsi tunavyosherehekea hivi karibuni .
Sisi sote tulikulia kati ya mila kadha za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, kama ilivyotujia kutoka kwa Wamisri wa kale, waliokuwa wakizoea kupika samaki wenye chumvi, lettuce na vitunguu ili kuvikula wakati wa Sikukuu ya Pasaka inayojulikana kama "Shem El-Nasim ", au ( harufu ya kutoa pumzi ), ambapo ilionekana mnamo siku ya kwanza ya miaka ya 50 na mwanzo mapema ya asubuhi hii, watu wengi, haswa wanawake, huvunja vitunguu na kunusa harufu yake, kisha kipindi cha asubuhi, wakazi wengi wa Kairo kwa ujumla hupanda boti kuelekea kaskazini ili kujiburudisha kwa hewa safi, ambapo wanaamini kuwa siku hiyo ina athari ya manufaa.
Vilevile ,kuna idadi kubwa ya watu hula chakula mbele ya ufukwe wa mto, kinachojumuisha mayai ya rangi ambapo Wamisri wa kale walikuwa wa kwanza kupaka mayai ya kuchemsha kwa rangi tofauti na yenye furaha,zikionesha uzuri wa machipuko na zinapendeza.
Mpaka wakati huu, bado tunafuata matendo ya wahenga wetu wamisri na mila zao za Sham El-Nasim kwa shughuli za sherehe zile zile. ambapo watu hushinda siku kwa kutembelea bustani au Mto Nile au kutembelea ndugu, au kwenda vijijini na mashamba ya kilimo ili kupumua hewa safi ,Kula vyakula vya asili kama kawaida, ambapo kuliwa siku hii, sill, dagaa, salinity, kila aina ya samaki, lettuce, vitunguu kijani, na lupine, pamoja na tabia ya kupaka na kula mayai ya kuchemsha, ambayo bado ni mojawapo ya desturi muhimu zaidi ya kusherehekea Sham El-Nessim.