Harakati ya Nasser kwa Vijana katika Jamhuri ya Tunisia yakutana na profesa katika Chuo Kikuu cha Harvard

Imetafsiriwa na: Rahma Magdy Mahmoud 
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

Yassine Fathali, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na Mjumbe wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, alishiriki katika mkutano wa kisayansi na profesa wa chuo kikuu cha Marekani Marshall Ganz katika Chuo Kikuu cha Harvard, ulioandaliwa na timu ya "LCN", ambapo mkutano huo ulileta pamoja viongozi wa vijana kumi na tano nchini Tunisia, na wahitimu wa kozi ya shirika la Kiarabu wakiongozwa na timu ya "Ahl Ahl", na mtandao wa waandaaji wa Kiarabu,na kando ya warsha na miradi mbalimbali ya kozi, viongozi wa Tunisia walishiriki hadithi za kuhamasisha na kuchunguza jinsi ya kuunda mipango endelevu ya ujenzi wa vijana, na kujitolea kwao kufanya mabadiliko wakati wa miaka kumi ngumu ya mpito ya Tunisia ilihamasisha timu ya LCN.

Katika muktadha unaohusiana, Mwanaharakati kijana «Yassine Fathali», Mratibu wa Harakati ya Vijana wa Tasir nchini Tunisia, alishiriki wakati wa mkutano katika kuwasilisha uzoefu wake kupitia shughuli za mpango wa Umoja wa Vijana huko Sidi Hussein kujitolea, akielezea furaha yake na kiburi katika timu yake ya kazi, kwani alifanikiwa kuendeleza mpango wa kuwa leo chama cha vijana wa ndani, ambacho kwa upande wake kinachangia maendeleo ya ushawishi wake.

Kwa upande wake, Harakati ya Nasser kwa Vijana inajivunia mafanikio na athari za kijamii za wanachama wake wote, haswa uwazi wake kwa mashirika ya kimataifa na mitandao na ulimwengu, ambapo malengo yake muhimu zaidi ni kukusanya viongozi wa vijana wenye ushawishi mkubwa ndani ya nchi, kikanda, na kimataifa katika meza moja ya mazungumzo, wanayobadilishana mawazo na uzoefu, na kujadili njia za ushirikiano kati yao, katika uanzishaji wa kina wa jukumu la diplomasia ya vijana katika nyanja za maendeleo endelevu.