Siku ya Vijana Duniani... Njia za Vijana wa Digital kwa Maendeleo Endelevu

Siku ya Vijana Duniani... Njia za Vijana wa Digital kwa Maendeleo Endelevu

Imetafsiriwa na: Basmala Nagy na Hager Moslleh
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Imeandikwa na: Rehab Ayman Hussein 

Mtafiti anayevutiwa na masuala ya kisiasa mnamo 
tarehe Agosti 12, dunia inaadhimisha Siku ya Vijana Duniani kwa lengo la kukumbusha ulimwengu jukumu la vijana na majukumu ya nchi kwao kama nguzo ya mataifa na msingi wa miradi yao ya kitamaduni na kijamii, pamoja na kuwa kundi linalohitaji umakini zaidi kwa unyeti wa hatua wanayoishi, imeyojaa nishati, ambayo, ikiwa imetumiwa vizuri, ingechangia katika ufufuaji wa mataifa.

Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani:

Mnamo mwaka 1999, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliteua tarehe Agosti 12 kuwa Siku ya Vijana Duniani kama sherehe ya kila mwaka ya jukumu la wanawake na wanaume kama washirika muhimu katika mabadiliko, pamoja na fursa ya kuongeza ufahamu wa changamoto na matatizo yanayowakabili vijana duniani.

Kauli mbiu ya Siku ya Vijana Duniani 2024

Siku ya Vijana Duniani mwaka huu itashughulikia mada ya kubonyeza maendeleo: njia za vijana wa digital kwa maendeleo endelevu inabadilisha ulimwengu wetu, kutoa fursa zisizo za kawaida za kuharakisha maendeleo endelevu. Teknolojia za kidijitali kama vile vifaa vya simu, huduma, na akili bandia ni zana muhimu katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). 

Ukweli wa Vijana na Takwimu

• Nusu ya idadi ya watu wa sayari yetu ni umri wa miaka 30 au mdogo, na asilimia hii inatarajiwa kufikia 57% ifikapo mwisho wa 2030.
• Utafiti unaonyesha kuwa 67% ya watu wanaamini katika maisha bora ya baadaye, na kwamba wale wenye umri wa miaka 15-17 ndio wenye matumaini zaidi.
• Watu wengi wanakubaliana kwamba uwiano wa umri katika siasa ni makosa.

Zaidi ya theluthi mbili (69%) ya watu katika makundi yote ya umri wanakubaliana kwamba fursa zaidi kwa vijana kuwa na usemi katika maendeleo na mabadiliko ya sera zitafanya mifumo ya kisiasa kuwa bora.

Duniani kote, idadi ya wabunge walio chini ya umri wa miaka 30 imefikia asilimia 2.6 tu, huku wanawake wakichukua chini ya asilimia 1 ya wabunge wote katika kitengo hiki.

Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani

Umoja wa Mataifa umeitangaza Siku ya Vijana Duniani Agosti 12 kuwa ni Siku ya Vijana Duniani hasa kwa sababu vijana ndio nguzo ya jamii katika nchi yoyote duniani, na ni sehemu muhimu ya maendeleo na maendeleo, na leo hii inashuhudia mpangilio wa shughuli nyingi za burudani, utamaduni na sanaa zinazoashiria nguvu na vipaji vingi katika jamii ambavyo lazima vitumike vizuri.

Kupitia Siku ya Vijana Duniani, Umoja wa Mataifa ulitoa wito kwa mashirika katika kila nchi duniani, iwe serikali, asasi za kiraia au hata watu wa kawaida, kusaidia shughuli katika ngazi mbalimbali, na kusherehekea vijana siku hii, kwa mujibu wa tovuti ya Umoja wa Mataifa. 

Kutoka Malengo ya Siku ya Vijana Duniani

• Kuendeleza sera za vijana, kuhimiza serikali na mashirika ya kimataifa kuendeleza sera za vijana zinazokidhi mahitaji ya vijana na kusaidia ushiriki wao.
• Uwezeshaji wa vijana, ambao husaidia kuwawezesha vijana kupata elimu na mafunzo yanayohitajika ili kujenga maisha yao ya baadaye.
• Kukuza mazungumzo ya kizazi, ambayo husaidia kuhamasisha mazungumzo na uelewa kati ya vizazi tofauti.
• Kupambana na ubaguzi, kwa kupambana na aina zote za ubaguzi dhidi ya vijana, ikiwa ni pamoja na ubaguzi kwa misingi ya jinsia, umri na dini.

Zaidi ya miongo 3 iliyopita, wazo la Siku ya Vijana Duniani, hasa mwaka 1991, lilipendekezwa na baadhi ya vijana huko Vienna na Austria, kuhudhuria kikao cha kwanza cha Jukwaa la Vijana Duniani la mfumo wa Umoja wa Mataifa, na Baraza lilipendekeza kutangazwa kwa siku ya vijana ya kimataifa.

Mnamo mwaka 1998, Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa mawaziri walio na jukumu la vijana, ulioandaliwa na serikali ya Ureno kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa, ulipitisha azimio lililotangaza mnamo tarehe Agosti 12 kuwa Siku ya Vijana Duniani.