Siku ya Kusherehekea
Imeandikwa na/ Shahd Ahmed
Lugha zinaongezeka duniani kote. Kuna lugha mbalimbali zaidi ya 6900 ulimwenguni. Lugha ina jukumu muhimu katika kuunda jamii na kuziendeleza, na hiyo ni kwa sababu ina umuhimu mkubwa; ambapo inasaidia mawasiliano na ukaribu wa kiakili na kitamaduni kati ya watu, na kuongezeka kwa ufahamu na ujuzi wa mambo mbalimbali, jambo linaloruhusu kushirikiana na ulimwengu wa nje.
Bara la Afrika lina zaidi ya lugha 3000 za asili, ambapo lugha ya Kiswahili ni mojawapo ya lugha muhimu zaidi za Afrika Mashariki. Shirika la UNESCO lilitangaza rasmi tarehe saba Julai kuwa Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili, jambo linaloifanya kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kuadhimishwa na Umoja wa Mataifa. Lugha ya Kiswahili inatumika katika nchi za vyanzo vya mto Nile zinazojumuisha nchi 14 ambapo inatumika kama lugha rasmi ya kwanza nchini Tanzania na lugha rasmi ya pili nchini Kenya, na pia inatumika nchini Rwanda, Burundi, Visiwa vya Komori, Kusini mwa Somalia na Uganda. Lugha ya Kiswahili ina jukumu muhimu katika kuimarisha utofauti wa kitamaduni, kuunda ufahamu na kukuza mawasiliano na muunganiko kati ya watu.
Lugha ya Kiswahili ina umuhimu mkubwa, ambapo zaidi ya watu milioni 200 wanazungumza lugha ya Kiswahili barani Afrika, na pia ina jukumu kubwa katika ukuaji wa elimu, ambapo inafundishwa katika nchi nyingi jambo linasaidia kuieneza na kuitumia. Lugha ya Kiswahili inatumika pia katika biashara na utalii; na hiyo inasababisha ukuaji katika uchumi wa kitaifa kwa nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili. Lugha ya Kiswahili ina umuhimu mkubwa katika kuhifadhi utamaduni na urithi wa kitamaduni na urithi wa kisanii na kifasihi kupitia riwaya, michezo na ushairi wa mdomo na maandishi. Lugha ya Kiswahili ina jukumu muhimu katika majukwaa ya kimataifa na kisiasa kupitia mashirika ya kikanda na kimataifa kama vile Umoja wa Afrika ambapo lugha ya Kiswahili ni moja ya lugha rasmi ya Umoja wa Afrika jambo linaloimarisha jukumu lake la kisiasa na kidiplomasia katika bara la Afrika.
Shirika la UNESCO linaweka tarehe ya kusherehekea Siku ya Kiswahili Duniani kuwa Julai 7 kila mwaka kuanzia mwaka 2022. Kusherehekea siku hiyo ni muhimu sana katika nyanja mbalimbali na kuimarisha nafasi yake kama lugha muhimu katika jamii ya kimataifa. Siku ya Kiswahili Duniani inasaidia kuimarisha utofauti wa lugha na kitamaduni kwani inabainisha umuhimu wa lugha ya Kiswahili kama sehemu ya urithi wa kitamaduni na lugha ya bara la Afrika, na pia kusaidia kuthibitisha umuhimu wa lugha na kuimarisha kuitumia katika maisha ya kila siku. Maadhimisho ya siku hii yanakuza ushirikiano kati ya nchi za Afrika katika nyanja ya elimu na utamaduni, na kuongeza uelewano kati ya tamaduni tofauti. Kuongezeka kwa hamasa ya Kiswahili kunaweza kuongeza utalii katika nchi zinazozungumza na kuwezesha biashara na ubadilishanaji wa utamaduni.
Ulimwengu husherehekea Siku ya Kiswahili Duniani mnamo tarehe Julai 7 ya kila mwaka, na miongoni mwa sherehe hizi ni matukio ya kitamaduni na kisanaa ambapo maonesho ya sanaa na muziki na maonesho ya michezo yanakazia urithi wa Kiafrika kupitia Kiswahili. Sherehe hizi zinajumuisha mashairi, nyimbo na dansi za kitamaduni pamoja na warsha za elimu na semina zinazofanyika shuleni au katika vituo vya kitamaduni; ili kufundisha lugha ya Kiswahili na kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wake. Vyombo vya habari vinaonesha programu maalumu kusherehekea siku hiyo kwa Kiswahili kama vile filamu za kumbukumbu, mahojiano, na programu za kielimu. Pia, taasisi za kitaaluma na kitamaduni zinaandaa semina na mikutano kujadili changamoto na fursa zinazohusiana na usambazaji na uendelezaji wa matumizi ya lugha.
Siku ya Kiswahili Duniani ni sehemu ya mashindano ya uandishi na hotuba kwa lugha ya Kiswahili ili kuhamasisha vijana kujifunza Kiswahili. Maadhimisho ya siku hiyo yanaendelezwa katika mitandao ya kijamii kupitia usambazaji wa taarifa na vifaa vya elimu ili kuhamasisha ujifunzaji na matumizi ya lugha ya Kiswahili.Katika siku hii, vyakula vya asili vinavyoonesha utamaduni wa nchi zinazozungumza Kiswahili vinahudumiwa. Pia huandaa maonesho ya sanaa yanayoonesha kazi za sanaa zinazoelezea utamaduni na urithi wa Kiswahili. Shughuli hizi zinaoneshwa kusaidia kukuza uelewa wa kimataifa kuhusu umuhimu wa Kiswahili na kukuza juhudi za kukisambaza kwa wingi, na hivyo kuimarisha utofauti wa lugha na utamaduni miongoni mwa Mataifa.
Umoja wa Afrika unalenga kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha inayounganisha watu wa Afrika, kukuza utambulisho wa pamoja wa Kiafrika, na kuimarisha mawasiliano kati ya nchi za Afrika, kupitia ushiriki wake katika shughuli za siku hii kupitia shughuli kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano na matukio rasmi mbele ya wawakilishi kutoka nchi wanachama, ili kuonesha umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika kukuza umoja na uelewa miongoni mwa watu wa Afrika. Umoja wa Afrika unashirikiana na mashirika ya kitamaduni ya ndani na kikanda kuandaa hafla za kitamaduni kusherehekea lugha na utamaduni wa Kiswahili.
Umoja wa Afrika unakuza siku hii kwa kuandaa kampeni za habari ili kuongeza ufahamu wa umuhimu wa lugha na kukuza matumizi yake, na Umoja wa Afrika pia unaunga mkono mipango ya elimu inayolenga kufundisha lugha ya Kiswahili shuleni na vyuo vikuu, na kukuza matumizi yake katika utafiti wa kitaaluma, Umoja wa Afrika hutoa fedha kusaidia miradi inayolenga kukuza lugha ya Kiswahili na matumizi yake katika maisha ya kila siku.
Kiswahili ni miongoni mwa lugha muhimu sana kwenye nchi za Afrika Mashariki na kina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na utamaduni wa nchi zinazozungumza Kiswahili. Imekuwa mojawapo ya lugha zinazoadhimishwa na Umoja wa Mataifa. Kutokana na hamasa kubwa ya uenezaji na uendelezaji wa lugha ya Kiswahili, watu wengi wana shauku ya kujifunza na kujifunza kuhusu utamaduni na ustaarabu wa watu wa nchi zinazozungumza Kiswahili Afrika.
