Anis Sayigh.. Mlinzi wa kumbukumbu za Palestina

Anis Sayigh.. Mlinzi wa kumbukumbu za Palestina

Sayigh aliishi akiwa na ndoto za kurejea Tiberias, ambako alikozaliwa Palestina, na alieleza msimamo wake kuhusu suala la Palestina akisema, akishutumu msimamo wa Jumuiya ya kimataifa kuhusu kesi hiyo, "Si mgongano wa kuwepo au mipaka, bali ni mgongano wa ustaarabu. Kuwepo kwa Israel ni kosa kubwa, kosa la kihistoria, na kosa lisiloendani na kanuni za nchi za Magharibi".
   
Mwanafikra mkubwa wa Kiarabu "Anis Sayigh" alizaliwa katika mji wa Tiberias, kaskazini mwa Palestina, mnamo Novemba 3, mwaka wa 1931. Alijulikana kama Mlinzi wa Kumbukumbu ya Palestina, naye ni Mpalestina mwenye asili ya Syria na ana uraia wa Lebanon. Alipata elimu yake huko Tiberias, kisha akajiunga na Chuo Kikuu cha Al-Quds, na baada ya mwaka wake wa kwanza huko, vita vilianza huko Palestina, kwa hivyo Sayigh alisafiri ili kumaliza masomo yake katika Shule ya Sanaa ya Kiinjili huko Sidon, kusini mwa Lebanon, kisha akajiunga na Chuo Kikuu cha Amerika huko Beirut na alihitimu katika mwaka wa 1953, kwa shahada ya kwanza katika Sayansi za Kisiasa, kisha akafanya kazi kama mwalimu wa historia ya Kiarabu katika idara ya Kifaransa katika Chuo Kikuu cha Marekani hadi mwaka wa 1957, baada ya hapo, alifanya kazi kama mshauri katika Shirika la Dunia la Uhuru wa Utamaduni kwa miaka miwili, kisha akajiunga na Chuo Kikuu cha Cambridge ili kupata uzamivu mnamo mwaka wa 1964, katika masomo ya Mashariki ya Kati, na kipindi hicho hicho, alikuwa profesa msaidizi katika Idara ya Mafunzo ya Mashariki, katika chuo kikuu hicho.

Al-Sayigh alihamia ili kufanya kazi kwa miaka kumi kutoka kipindi cha (1966-1976) kama mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Shirika la Ukombozi wa Palestina huko Beirut, ambapo alifanya kazi ya kuanzisha maktaba yenye vitabu zaidi ya elfu 13, pamoja na hati na nyaraka, na aliendelea juhudi zake za kutoa jarida la "Mambo ya Palestina" lililochapishwa kila mwezi, kisha likafuatwa na mfululizo wa "Masomo ya Palestina", na pia Kituo hicho kikiongozwa naye kilitoa, kipindi cha "Ufuatiliaji wa Redio ya Israel".

Katika kipindi hicho hicho kilichotajwa, "Al-Sayigh" pia alishika wadhifa wa Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kiarabu na Mafunzo ya Umoja wa Nchi za Kiarabu huko Kairo, ambapo alisimamia zaidi ya uzamili na uzamivu thelathini, huko Beirut na Kairo. Pia alifanya kazi kama mwenyekiti wa kiti cha Palastina katika Umoja wa Kiarabu katika kipindi cha (1977-1987), kisha kama mshauri wa usalama wake katika mwaka wa 1980, na kama mkuu wa kitengo cha magazeti, na alitoa gazeti la "mambo ya kiarabu" na alishika uhariri wake, na akaendelea na kazi yake katika chuo kikuu hadi mwaka wa 1982.

Al-Sayigh alikuwa na jukumu kubwa katika kutoa "Ensaiklopidia ya Palestina", wazo lililopitishwa na Shirika la Kiarabu la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa ya Kiarabu, na alishika uhariri wake. Na pia, alichaguliwa kama mwandishi wa ensaiklopidia na mshauri wa bodi yake ya wakurugenzi katika mwaka wa 1983.

Miongoni mwa vitabu vyake mashuhuri zaidi ni kitabu chake "Madhehebu ya Lebanon" na somo lake maarufu "Kutoka Faysel wa kwanza kuelekea Gamal Abdel Nasser: usomaji wa dhana ya uongozi wa kisiasa", ambacho alikichapisha katika mwaka wa 1965, na kitabu chake "ujinga wa kesi la Palestina: Utafiti katika Taarifa za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kiarabu juu ya Kesi la Palestina" ililochapishwa katika mwaka wa 1970, pamoja na utafiti wa "Syria katika fasihi ya Mmisri wa zamani", "wazo la kiarabu nchini Misri", pamoja na kitabu chake "Maendeleo ya Dhana ya Kitaifa kwa maoni ya Waarabu" na vingine.

Mwanahistoria mashuhuri "Anis Al-Sayigh" hakuwa mbali na mbinu za ukandamizaji na ukiukaji mbaya ambao Ukoloni ulifanya dhidi ya watu wote wenye heshima, wapiganaji na watetezi wa suala la Palestina. Mwanahistoria wetu alikandamizwa zaidi ya mara moja kwa kalamu yake ya heshima. Ambapo katika mwaka wa 1966 aliombwa kutia saini kwa ahadi ya kutoandika makala za kisiasa hata kidogo. Pia alikabiliwa na jaribio la mauaji zaidi ya mara moja, hata katika mwaka wa 1972, palikuwa na kifurushi chenye bomu kiliipuka mikononi mwake, jambo linalosababisha mikono yake kukatwa. Ukiukaji huo pia uliathiri kitovu cha Beirut, na mnamo mwaka wa 1974 ilifanyiwa operesheni ya mabomu iliyosababisha hasara kubwa.