Mfasiri Fukuzawa Youkitshi...Ni Mojawapo wa Waanzishi wa Mwamsho wa Japani Mpya “

Mfasiri Fukuzawa Youkitshi...Ni Mojawapo wa Waanzishi wa Mwamsho wa Japani Mpya “

Imetafsiriwa na/ Tuka Ashraf 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled  


"linasemwa kwamba mbingu haiwaumbi watu zaidi ya waliopo, na haiwaumbi watu chini ya waliopo"

   Fukuzawa Youkitshi amezaliwa mnano mwaka  wa 1835  huko mjini Ausaka jimboni Nakatsu wilayani Bozin, aliyekuwa mtoto wa pili katika familia ya Samurai iliokuwa ikifanya kazi katika ghala ya mazao, Wakati wa utoto wake, Fukuzawa alipata elimu ya Ukonfusio huko jimboni Nakatsu, na mnami mwaka wa 1854, amemaliza misingi ya masomo ya sayansi ya nchi za magharibi pamoja na kuongea lugha ya Kiholanzi kwa ufasaha sana hukomjini Nagazaki ulioko kwenye pwani ya kusini ya magharibi ya kisiwa cha Kiosho cha kijapani, na kilichokuwa chini ya utawala ya ukoloni wa Kiholanzi wakati huo,  mnamo mwaka wa 1855, Youkitshi alirudi kwa “Ausaka” ili kujiunga shule ya kisayansi ya magharibi iliyokuwa Inasimamiwa  na Daktari na Mwalimu Ogata Kwan, Daktari wa Matibabu ya Magharibi.

  Ama mnamo  mwaka wa 1855, Youkitshi alihamia mjini Idu (ambayo kwa sasa ni  mji mkuu Tokyo) alikuwa Mwalimu katika Shule ya Kisayansi ya Magharibi (  baadaye imekuwa Kiuu Ghigoko) katika jimbo la Nakatsu, Japan ilikuwa imefungua  bandari tatu za meli za Marekani na Ulaya kwenye ghuba ya Tokyo, hivyo Youkitshi alikwenda mji wa Kanagao ili kukutana na wagen, lakini alishtukwa alipogundua kwamba wafanyabishara wa Ulaya waliongea lugha ya kingereza sio lugha ya Kiholanzi, kwa hivyo alichukua uamuzi wa kujifunza lugha ya kiingereza licha ya ukosefu wa kamusi, na wafasiri wa lugha za kiingereza- kijapani wakati huo.

     Shughon “kiongozi ya kijeshi ya Japan” alipoamua kutuma mjumbe kwa Marekani, Fukuzawa alijitolea ili kusaidia mjumbe kwenye meli ya kijeshi ya Kanrinmaru yaliokuwa yanamilikiwa na serikali ya Ido. wakati wa ujumbe ulifikia San Francisco mnamo  mwaka wa 1860, ulibaki kwa mwezi, hii ilimsaidia Youkitshi ili kupata kamusi ya ‘Webster’  na alianza kufanya juu chini ili kujifunza lugha ya kiingereza,  Baada ya kurudi Japani, cheo chake kilibadilika na kuwa mfasiri katika huduma ya usafiri wa kigeni. Baada ya muda mfupi aliandika kitabu chake ya kwanza; kamusi ya kiingereza iliopewa jina la “ Kaya Tsogho” iliofasiriwa kutoka kwa kamusi ya Kiichina-Kiingereza. 


     Mnamo mwaka wa 1862 , Youkitshi alikwenda kwa baadhi ya nchi za magharibi kama  Uingereza, Ufaransa, Uholanzi, Ujerumani  na Urusi. Aligusia nchi hizo akisema:"  kupitia maoni yangu juu ya  ustaarabu wa Magharibi na Mashariki  , ninaona kwamba kila ustaarabu una  nguvu na udhaifu,  ndani ya  mafundisho yake ya kimaadili, na nadharia za kisayansi. Lakini ninapolinganisha baina ya ustaarabu mbili kwa ujumla, kwa upande wa utajiri, ngovu, na kuhakikisha furaha kwa watu wengi, nitaweka Mashariki katika daraja ya chini kuliko Magharibi.


    Youkitshi alipokuwa katika Ulaya, haivutiwa na kisayansi, uhandisi, na umeme…, alieleza hayo akisema:  kwa hivyo nilipokuwa barani Ulaya, nilikuwa na hamu kwa mambo yanayonivuta zaidi. Kwa mfano, niliona hospitali na nilitaka kujua namna inasimamiwa na nani anayelipa gharama inayoendelea, na nilipokwenda benki, nilitaka kujua namna ya kutoa na kulipa pesa, na kulingana na maswali ya moja kwa moja, ninapata baadhi ya maelezo kuhusu mfumo wa posta na (chango- uandikishji ) unaotumika wakati huo nchini Ufaransa.
     Youkitshi alifahamu mahusiano baina ya tabia ya mfumo wa utawala unaozingatia dhuluma na kuwazuia wanawake kupata elimu, na alisisitiza katika maandishi yake kwa dharura ya kumkomboa mjapani kutoka kwa vikwazo vilivyopunguza uwezo wa kufanyikia katika maendeleo na kiutamaduni – kwa maoni yake- na haya ni maoni ambayo yamekua kwa sababu ya kujua majaribio ya kimagharibi ya kifalsafa, kijamii, na kiudhibiti.


    Alianzisha gazeti la”Jiji Shinbo” na magazeti mengine ya Kijapani, na yeye ni mjapani ya kwanza anayetoa wito kwa marekebisho ya kielimu, kisayansi na  ya kimarifa akiomba serikali kudhibiti (au kuunda) taasisi za kijamii. Mawazo yake juu ya utawala na kisiasa yalikuwa yenye athari kubwa kwa maendeleo ya Japani .


    Fukuzawa Youkitshi ni mwanzishi wa chuo kikuu cha Kiuu, kinacho ni ya kwanza na ya kale zaidi nchini Japani, na pia ni moja ya vyuo vikuu bora zaidi nchini Japani، kilianzishwa na Fukuzawa Youkitshi kama shule ya masomo ya kigeni huko mjini Idu mnamo mwaka wa 1858,  na wakati wa ufunguzi, alisema neno yake maarufu: “Ninazingatia kusoma kama sanaa ya vitendo, mara baada ya kuondoka, weka akilini mwenu kile kilichojifunza. Na kuanza kufanya kazi yenu katika jamii. Jiungene na jichanganye na watu, hii itayabadilisha mawazo yao na kuwasaidia nyinyi kupanua elimu zenu.”.
  Fukuzawa alikabiliwa na  matatizo mengi sababu ya  mila inayokuwa  inazuia uwezo na fursa za elimu za wanawake; wakati mahitaji ya shule za kibinafsi ya wasichana yalipungua,  yeye aliwajibika kuwafunza wasichana wake nyumbani mwake na walimu binafsi..
Mwaka 1866, alichapisha kitabu chake “Hali ya Magharibi” alieleza ndani yake muundo wa kisiasa na kiuchumi kwa kila nchi za magharibi, akitegemea maelezo yaliyoyapata pale . Na alisafiri tena Marekani mwaka 1876, na alikwenda mji mkuu Washington na mji wa New York.    


        Fukuzawa alijaribu kwa bidii ili kuchapisha masharti sita ya kisiasa ya kiustaarabu yanayopo mwanzoni mwa shehemu ya kwanza katika kitabu chake “ Hali ya Magharibi” nchini Japani na nchi za Asia. Na masharti yale ni: 

-Kuheshimu uhuru wa kibinafsi na kutoruhusu sheria kuzuia wananchi.
-Kudhamini uhuru wa kidini
-Kuunga mkono na maendeleo kisayansi na kiteknolojia
-Kuboresha elimu ya shule
-Kuboresha viwanda kupitia sera thabiti inayotegemea sheria zinazofaa.
-Kuboresha maisha ya wananchi


    Fukuzawa aliaga dunia kwa sababu ya kiharusi chake katika Tarehe 3, mwezi wa Februari , mwaka 1901, katika umri wa 66, Picha yake iliwekwa kwenye 10000 sarufu ya yen ya kijapani ili kuwa kumbukumbu yake.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy