Mhanga wa Ukumbi wa Michezo Nihad Saliha

Mhanga wa Ukumbi wa Michezo Nihad Saliha
Mhanga wa Ukumbi wa Michezo Nihad Saliha

Imetafsiriwa na/ Rahma Ragab 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled  


"Nini yaliyobaki kutoka binadamu baada ya kifo chake?...si chochote kilichoonekana...bali ni kitu kisichoonekana na maneno yaliyotuliza ugumu wa siku na yanatufanya kufikiria kwa muda chache kwamba tumepita nyakati, tumeweza kudhibiti matukio mengi ya siku yanatofichwa"
Kitabu cha maelekezo ya jukwaa kilichoandikwa na Nahid Saliha 

Saliha ni mmojawapo wa wataalamu wa uhakiki wa tamthilia nchini Misiri na ulimwengu wa kiarabu, alikuwa na bado ni bibi wa kwanza wa uhakiki, anapenda jukwaa kwa hali ya pekee ikiwa hapati fursa ya kuigiza kwenye jukwaa, lakini ameweza kujali mambo yake na amestahiki sana lakabu ya " MTAWA wa JUKWAA" kwa roho ya uhuru na akili mzuri inayopendelea uwazi, uzuri, uhuru na maisha

Nahid Salih ni mhakiki na mtafiti wa tamthilia, amezaliwa mwaka 1945, mtaani mwa shobra hapa kairo, masomoni mwake, hamu yake ya jukwaa ilizidishwa na tamthilia za Shakespeare , kwa hivyo alichagua kusoma fasihi ya kiingereza ili kuendelea hamu yake ya  tamthilia, amehitimu Kitivo cha fasihi, kitengo cha lugha ya kiingereza, chuoni mwa Kairo, baadaye alihamia uingereza ili kuendelea masomo yake, ambapo alipata uzamili na uzamivu katika uwanja wa riwaya ya kisasa kutoka Chuo kikuu cha Susse, na alifanya kazi kama mwalimu wa tamthilia na uhakiki wa kifani kwenye taasisi kuu ya uhakiki wa kifani mnamo mwaka 1984 baadaye amekuwa mkuu wa taasisi kati ya 2001 hadi 2003, pamoja na hayo akafanya kazi kama mwangalizi wa kitengo cha uhakiki wa tamthilia kwenye gazeti la  "Al-ahram weekly" kuanzia 1989 hadi kifo chake mnamo mwaka 2017.

Utungaji wa Saliha umetofautisha kati ya wazo, jukwaa, fasihi, uwazi na masuala ya wanawake, utungaji huo umekuwa unaonesha mtazamo wake mkubwa wa uhakika na miongoni mwake ni " mikondo ya kisasa ya tamthilia" na " usasa baadaye na Sanaa za kucheza" , pia " mwanamke kati ya sanaa, upendo na ndoa" na kitabu cha " wameniulizia kuhusu uzoefu" na " jukwaa imepita mipaka" kupitia hayo, mwandishi wetu ametoa uhakiki unaoendana na uhalisia, na anapata kina na nguvu yake kupitia kuelewa kwa kina vipengele vya ustaarabu wa kimagharibi, na hakusahau vipengele vya utamaduni wa kimisri na wa kiarabu.

Saliha alijali kuhamisha harakati ya jukwaa ya kimisri kwa viwango vya ulimwengu, na kwa mtazamo wake sanaa haitokei pekee yake bali ina uhusiano wa kina na maisha ya binadamu, alikuwa anaona kwamba maandishi ya tamthilia si maonesho ya kucheza tu bali ni kuonesha hali ya kisiasa, ya kijamii, na ya kiuchumi kwa onesho zima, kwenye muktadha huo, aliandika maandishi kadhaa kwa kiingereza miongoni mwao ni " jukwaa ya kimisri: mikondo mipya" na mengine kwa anwani ya " jukwaa ya Lord Bairun: kusoma kwa sasa" na " tamthilia na wanatamthilia(watendaji)" na kitabu chake cha anwani ya "matarajio ya tamthilia" kinachojumuisha makala yake katika kipindi cha kati ya ( 1994:2009), kinaonesha urahisi wa simulizi lake na uhamu yake mkubwa kwa jukwaa.

Mwandishi na mhakiki mkuu "Saliha" alipata tuzo nyingi kutoka matamasha mengi ya kiarabu na ya kimataifa miongoni mwake ni tuzo ya tamasha la ( Al-sharka), (Carthage) na tuzo ya tamasha la tamthilia la Damascus mnamo 2008, kwa heshima ya juhudi za wana wake wenye dhati,MISRI imemheshimu mara kadhaa , heshima kubwa zaidi ilikuwa kumtoa tuzo ya shukurani ya nchi ya sanaa kwa uhakiki wa kifani na mnamo 2013, ili kudumisha jina la  "Nahid Saliha", jukwaa isiyofunika kwenye taasisi ya sanaa imeitwa kwa jina hilo, na iliyofunguliwa mnamo Novemba, 2021 ili kudumisha, kuthamini michango yake katika nyanja za sanaa na utamaduni.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy