Al-Tigani Al-Mahi .. Msudan aliyejitolea kama daktari mkuu kwa madaktari wa akili kwenye Silaha ya matibabu ya kimisri

Al-Tigani Al-Mahi .. Msudan aliyejitolea kama daktari mkuu kwa madaktari wa akili kwenye Silaha ya matibabu ya kimisri
Al-Tigani Al-Mahi .. Msudan aliyejitolea kama daktari mkuu kwa madaktari wa akili kwenye Silaha ya matibabu ya kimisri
Al-Tigani Al-Mahi .. Msudan aliyejitolea kama daktari mkuu kwa madaktari wa akili kwenye Silaha ya matibabu ya kimisri
Al-Tigani Al-Mahi .. Msudan aliyejitolea kama daktari mkuu kwa madaktari wa akili kwenye Silaha ya matibabu ya kimisri
Daktari Al-Tigani Al-Mahi anachukuliwa kuwa baba wa madaktari wa kisaijolojia barani Afrika na mmoja wa waanzilishi mashuhuri wa Chama cha Saikolojia cha Kiafrika, alizaliwa Aprili 1911, huko Al-Kawa katika eneo la Nile nyeupe huko Sudan, na alihitimu kutoka Shule ya Matibabu ya Kitchener huko Khartoum mnamo 1935, kisha akelekea Uingereza mnamo 1947, na akapata diploma ya juu katika taaluma ya Tiba ya kisaikolojia mnamo 1949, kisha akarudi nyumbani kwake na alijiunga na Wizara ya Afya ya Sudan, na alianzisha kliniki ya magonjwa ya neva huko Khartoum, na kuwa Msudan na Mwafrika wa kwanza anayehusika katika Taalum ya tiba ya kisaikolojia.
Mnamo kipindi cha kuanzia 1959-1969, Shirika la Afya la kimataifa lilimchagua Daktari Al-Mahi kuwa mshauri wa kikanda kwa shirika hilo kwa eneo la Mashariki ya bahari ya katikati kuhusu tiba ya Saikolojia, na mnamo 1969 alichukua nafasi ya Mkuu wa Idara ya Saikolojia katika Kitivo cha Tiba katika Chuo Kikuu cha Khartoum, na utafiti na masomo yake yakawa ya marejeo ya kisayansi ya kuaminika, ambapo hufundishwa katika sehemu za Saikolojia katika nchi nyingi za ulimwengu. Pia Daktari Al-Tijani alishiriki katika mikutano kadhaa ya kisayansi kote ulimwenguni, na akaongoza mkutano wa kwanza uliokuwa ukisimamiwa na Umoja wa Mataifa katika elimu na saikolojia huko Geneva. Pia alitoa mihadhara kadhaa katika vyuo vikuu vingi vya kimarekani kuhusu Tiba ya kisaikolojia.
Alikuwa na jukumu kubwa katika maisha ya kisiasa huko Sudan baada ya mapinduzi ya Oktoba 21, 1964, ambapo alichaguliwa kama mbunge na rais mbadala katika Baraza Kuu, na akashika nafasi ya rais katika baraza lile lile mnamo 1965, na alipendezwa sana na wasomi wengi na wanasiasa kote ulimwenguni , ambapo mwanahistoria na mtaalam mkubwa mfaransa anayehusika mambo ya kiafrika "Jack Burke" alimtembelea huko Khartoum, alishangaa na kushangilia maarifa na utamaduni wake, kama alivyosifiwa na Malkia wa Uingereza "Elizabeth wa pili " wakati wa alipotembelea Sudan mnamo 1965 kulingana na maarifa yake ya kiutamaduni.
Kuhusu nafasi yake na Misri , Daktari Al-Mahi alijitolea huko Misri wakati wa uchokozi wa mara tatu nchini Misri mnamo 1956. Ambapo alijiunga na akawa mkuu wa madaktari wa kisaikolojia - Silaha ya matibabu ya kimisri, na akaenda Misri mnamo Disemba 1964, ili kushiriki katika sikukuu za ushindi zilizofanyika katika mji huo Port Said na alikutana na Rais Gamal Abd El Nasser, na hapo awali Rais Abd El Nasser alikuwa alipeleka naye hotuba mnamo siku ya kwanza ya Machi 1960, na hii ni sehemu ya hotuba ya Rais Abd El Nasser na Daktari El Mahi :-
"Daktari Al-Tijani Al-Maji ... Al salamu Alaikum w Rahmat Allah w Barakatu... nilikipokea kitabu chako cha (Utangulizi wa Historia ya Tiba ya kiarabu) ambacho ulinipa, na nilikipenda kama kielezo cha kihistoria kinachosajili Uarabu iliyochangia ustaarabu tangu mwanzo wake, na Waarabu walikuwa kutoka waanzalishi wa wazo hilo na walitoa huduma nzuri zaidi kwa ubinadamu".
Kazi yake haikujiwekea hadi suala la Tiba na uandishi katika uwanja wa afya ya kisaikolojia , lakini alikuwa akivutiwa na ubinadamu na sayansi za kijamii, falsafa, historia, sayansi za ustaarabu na asili na historia ya Tiba ya kisaikolojia.
Kwa hivyo, Al Mahi alihusika sana katika utafiti wa matibabu ya kisaikolojia katika muktadha kamili wa kijamii na kiutamaduni, na katika utafiti wake juu ya utamaduni wa Kiafrika alisoma akiolojia ya zamani na ustaarabu mkale wa Kiafrika, na alikuwa na ufahamu wa lugha kale ya hieroglyphiki, pia alikuwa akicheza Kinanda na alikuwa na hamu ya sanaa kwa aina zake tofauti.
Katika hotuba yake ya ufunguzi katika Mkutano wa kwanza wa Saikolojia ya Kiafrika alisema: "Katika Tiba ya kisaikolojia ya Kiafrika mtu anaweza kufuatilia mwanzo, mabadiliko, ukomavu na kuenea kwa ulimwengu wa Tiba ya kisaikolojia leo. Kwa hivyo, katika mkutano huo, mazungumzo yetu ndani bara kubwa hili yatatupeleka kwenye mitazamo mipya ya uelewa, ambapo vyanzo vya kihistoria, kijamii, kiuchumi na kitamaduni huunganisha na kuingiliana na kuibuka kama sehemu muhimu ya dhana ya afya ya kisaikolojia".
Kabla ya kifo chake, Daktari Al-Tijani Al-Mahi aliondoka maktaba kubwa, inayokusanya jumla ya karibu na vitabu vikubwa elfu ishirini, kati ya hizo elfu sita ni nakala ya maandishi ya akiolojia na seti ya barua rasmi, na sasa ni sehemu ya maktaba ya Chuo Kikuu cha Khartoum, na ana masomo ya upainia na mashuhuri katika uwanja wa afya ya kisaikolojia , na Daktari Al-Mahi alikufa huko Mnamo tarehe nane ya Januari 1970, jina lake lilipewaa kwa hospitali ya kwanza iliyoanzishwa katika Afya ya Neva na Saikolojia huko Sudan ambayo ni Hospitali maarufu (Al-Tigani Al-Mahy), na inachukuliwa kuwa moja ya hospitali maarufu zaidi barani Afrika.