Uratibu wa Afro-European... Wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wazindua mfululizo wa vikao vya kutambulisha Udhamini huo
Wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walitangaza kuanza kwa mfululizo wa vikao vya utangulizi kwa Udhamini huo, utakaoanza kikao chake cha kwanza kwa Kiarabu mnamo Jumapili, Aprili 2, saa tatu na nusu usiku kwa wakati wa Kairo, na ushiriki wa nchi kadhaa za Afro-Arabo, ikiwa ni pamoja na Morocco, Algeria, Yemen, Libya, Palestina na Misri, ambapo mtafiti wa diplomasia ya utamaduni wa Morocco Amir Hamza, mwanaharakati wa Algeria Nassima Benyousi, na Yemeni Mohammed Al-Jabri, na mhandisi Nariman Al-Sahati, na mwanaharakati wa jamii Ghada Raslan, watashiriki kama wazungumzaji wakuu, na Suzanne Saadeh wa Palestina kama Msimamizi wa Kikao,na vikao hivyo vinatarajiwa kuendelea hadi katikati ya Aprili kwa wiki mbili kwa lugha tofauti nazo ni : Kiingereza ,Kifaransa, Kiswahili, Kihispania, na KIarabu, vinavyoratibiwa na Mhandisi Al-Zubair Al-Burki kutoka Libya na mwanaharakati wa Urusi Vera Kamenskaya, na kuwalenga vijana wanaotaka kujiunga Udhamini huo kutoka mabara mbalimbali Duniani.
Prof.Ashraf Sobhy, alisema kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa uko na ujali mkubwa kutoka kwa uongozi wa kisiasa, na hilo ndilo lililoufikisha kupata Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi kwa mara ya tatu mfululizo, akiashiria kuwa Udhamini huo unawalenga viongozi vijana wenye ushawishi katika nyanja mbalimbali kutoka mabara yote ya Dunia, huko akieleza kuwa Udhamini huo unawapa washiriki fursa ya kukutana na baadhi ya watoa maamuzi na wanadiplomasia, pamoja na kuandaa ziara kadhaa za nyanjani kwa taasisi mashuhuri na muhimu zaidi za kitaifa nchini humo; kufahamiana kwa karibu na sera za taifa la Misri na uzoefu wake wa mwanzo katika uwezeshaji wa vijana, na toleo lake la nne limepangwa kuzinduliwa mnamo Juni hii ya 2023.
Kwa upande wake, mwanaanthropolojia Hassan Ghazali, Mwanzilishi na Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alisifu jukumu kubwa linalotekelezwa na vikao vya utangulizi kwa njia huru na yenye madaraka, iliyoandaliwa na wahitimu wa Udhamini wa Nasser na wanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana wakati kama huo kila mwaka, akiashiria nia yao kuhusu utofauti wa kiutamaduni na utofauti wa mataifa na mabara yanayoshiriki na hata utofauti wa kijinsia wa wazungumzaji katika kila kikao, kwani wanaunda maeneo mengi ya majadiliano, maswali na majadiliano kati ya vijana kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu na kutoka nyanja tofauti na makundi ya jamii kati ya viongozi watendaji, viongozi vijana katika asasi za kiraia, wasomi, vyombo vya habari na wengineo, akisisitiza kuwa vikao hivyo ni fursa halisi ya kujua Udhamini huo kwa karibu kupitia viongozi vijana walioishi uzoefu na kufuatilia athari zake.
Mwanaharakati wa Libya, Mhandisi Al-Zubair Al-Burki, Mratibu Mkuu wa vikao vya utangulizi vya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alisema kuwa vikao hivyo ni mpango huru wa wahitimu wa Udhamini kutoka kwa makundi yaliyopita na hutokea kwa kutambua tofauti iliyofanywa na Udhamini katika njia zao za kazi na hamu ya wahitimu kushiriki maelezo ya uzoefu wenye thamani - kama alivyoiweka - na wenzao wanaotaka kushiriki katika matoleo yajayo ili kuongeza faida yao kutoka kwa Udhamini wa Nasser, akielezea fursa za mshikamano zenye nguvu na zenye matunda iliyotokana na matoleo ya zamani kati ya wahitimu wachanga, na inayoongezeka kwa kiasi kikubwa kila mwaka, akisisitiza jukumu kubwa la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa pamoja na Ufadhili wa Urais wa Misri katika kuimarisha jukumu na sauti ya vijana katika kuweka maamuzi, iwe katika ngazi za kitaifa, kikanda au kimataifa.