Chuo cha Polisi chapokea Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Chuo cha Polisi chapokea Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Chuo cha Polisi kilipokea kikundi cha Viongozi  Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne, ulioandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri kwa kauli mbiu "Vijana wa Nchi za kutofungamana kwa upande wowote na Kuamsha Ushirikiano wa Kusini-Kusini", pamoja na Ufadhili wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.

Ujumbe wa Vijana walioshiriki katika Udhamini huo ulipokelewa na Meja Jenerali Hani Abu Al-Makarem, Waziri Msaidizi wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Chuo cha Polisi, na viongozi kadhaa wa Chuo, ambapo aliwakaribisha Viongozi Vijana na kuwafikishia salamu za Meja Jenerali Mahmoud Tawfiq, Waziri wa Mambo ya Ndani.

Kwa upande wake, Meja Jenerali Ismail Al-Far, Katibu Mkuu wa Kwanza wa Wizara ya Vijana na Michezo na Mkuu wa Sekta ya Vijana, alitoa shukrani zake za dhati kwa Wizara ya Mambo ya Ndani inayowakilishwa na Chuo cha Polisi, akisisitiza nia yake ya kurudia ziara hiyo, inayochangia maendeleo na uboreshaji wa utaalamu na kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Shughuli za ziara hiyo zilianza kwa kutazama filamu ya maandishi inayoelezea shughuli mbalimbali za Chuo ili kuandaa na kuhitimu polisi, ikifuatiwa na ziara ya ukaguzi wa vyombo vya Chuo, ambayo ni pamoja na Kituo cha Usalama na Mafunzo ya Mkakati katika Kituo cha Utafiti wa Polisi, wakati ambapo walijifunza juu ya uwezo wa vifaa na jukumu la Kituo katika kufuzu na kuandaa makada wa usalama kutoka nchi za Afrika na Jumuiya ya Madola ndani ya muktadha wa itifaki ya ushirikiano iliyohitimishwa kati ya Kituo na Shirika la Ushirikiano wa Misri kwa Maendeleo katika Wizara ya Mambo ya Nje katika maeneo yanayowakilisha hitaji la kimataifa kama vile kupambana na ugaidi na uhalifu. Uwasilishaji wa Shirika pia ulitazamwa ambao unajumuisha shughuli za Kituo katika kukuza kanuni za haki za binadamu na kusaidia uhuru wa msingi katika ngazi mbalimbali za kitaifa, kikanda na kimataifa.

Hiyo ilifuatiwa na ziara ya makao makuu ya Kitivo cha Mafunzo ya Uzamili na Kituo cha Misri cha Mafunzo katika Operesheni za Kulinda Amani, ambayo huandaa makada wa usalama wa "kitaifa na kigeni", pamoja na kushiriki katika ujumbe wa kulinda amani katika Umoja wa Mataifa, ikifuatiwa na kwenda Chuo cha Polisi na kutazama mawasilisho ya mafunzo kwa wanafunzi wa Kitivo.  

Kwa upande wao, washiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walionesha shukrani zao za dhati kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, iliyowakilishwa na Chuo cha Polisi, kwa mapokezi mema, ikionsha jukumu lake la kihistoria na la kipekee, ambalo sio tu kwa kuandaa na kufuzu maafisa katika ngazi ya kitaifa, lakini inaenea kujumuisha makada wa usalama kutoka nchi za Kiarabu na Afrika.