Mawasiliano ya Siku nyuma na Siku zijazo

Mawasiliano ya Siku nyuma na Siku zijazo

Imefasiriwa na / Mervat Sakr

«Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa» wachukua ishara na maadili ya "Ma'et" kama kauli mbiu ya Udhamini wa Nasser kwa mwaka 2023 

«Uwiano - Hekima - Maarifa - Ukweli - Haki - Utaratibu» Maadili ya Ma'et wa Misri tangu alfajiri ya historia 

Udhamini wa Nasser umechukua mfano wa "Ma'et" kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kwa mwaka 2023, utakaoanza Juni ijayo, kwa ushiriki wa viongozi Vijana 150 Duniani kote. 

Ma'et anajulikana, kiishara, haki na utaratibu katika ulimwengu, akiwakilishwa kama mwanamke mwenye manyoya ya mbuni juu ya kichwa chake, ishara ya haki, akishikilia kwa upande mmoja ufunguo wa maisha "Ankh" na kushikilia kwa upande wake mwingine fimbo ya utawala, ambapo Mmisri wa kale alichukua kutoka «Ma'et» kanuni za maisha yake, ambapo aliona katika utaratibu wake, usawa, mwanzo, mwisho, dali(ghaya) na kamilifu, iliyoashiriwa na mwanamke mwenye mabawa mawili - ni siri ya Uwiano wake - na usawa wa uthabiti wa kitu chochote na mfumo wa ulimwengu, na Ma'et ni ishara ya ukweli, haki na uadilifu, ambayo ni kauli mbiu ya mahakama katika Misri ya kale.

Sheria za Ma'et zilijumuisha maadili ya kibinadamu katika sura zake zote za juu, na zilionesha wazi ufahamu wa Misri ya kale juu ya ulimwengu, kwani ni ishara ya ukweli, haki na utaratibu katika ulimwengu, hivyo kanuni za Ma'et zilikuwa mwongozo wa kuishi katika jamii na zilitiiwa na kila mtu. 

Kwa upande wake, Hassan Ghazaly, Mwanzilishi na mratibu mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alisema kuwa sheria za mfano za Ma'et zinaungana na kanuni na nyaraka nyingi za Udhamini huo unazotegemea, unaotaka kutafuta taratibu za kuziamsha, miongoni mwao, akionesha kuwa muhimu zaidi, kwa ujumla na kina kanuni hizo ndizo zilizoelezwa katika sheria za Ma'et, kama inavyosema:  

1- Sikuwaibia wengine mali zao kwa ugomvi.

2. Sijafunga masikio yangu kutokana na kusikia maneno ya ukweli.

3- Sijamudhia mtu yeyote.

4- Sijaumiza hisia za wengine.

5- Sijabaka ardhi ya mtu yeyote.

6- Sijamtisha mtu yeyote.

7- Sijatishia Amani. 

8. Sijatoa mawazo/maneno/au vitendo vibaya.

9- Sijanyakua chakula na mdomo wa mtoto.

10- Sijaharibu majengo ya dini (mahekalu) 

Ghazaly aliongeza, akieleza kuwa Udhamini wa Nasser ni moja ya mipango ya Wizara ya Vijana na Michezo na moja ya mifumo ya kiutendaji ya mapendekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na unafanya kazi kuwawezesha vijana kwa utambuzi na kuwawezesha kujenga maoni kamili na muhimu yanayohusiana na masuala ya kimataifa na mipango ya maendeleo endelevu na matokeo ya kihistoria, akielezea kuwa inakuja ndani ya mfumo wa kutekeleza maoni ya Misri ya malengo ya maendeleo endelevu 2030 na ajenda ya Afrika 2063, na ushirikiano wa Kusini - Kusini.

Katika muktadha unaohusiana, Hassan Ghazaly alisisitiza kuwa wazo la ishara ya kihistoria ya Udhamini mwaka huu linahusishwa sana na kulingana na maoni ya serikali ya Misri katika kuendeleza utambulisho wa kitaifa, na mipasho yake ya ustaarabu inayoenea na kuingia ndani kabisa ya historia, kuanzia na Wamisri wa kale, wakipitia Kigiriki na Kirumi, kisha polar, Islamic, Mediterranean na African, ambao sifa na tamaa zao zilionekana kwa ulimwengu wakati wa sherehe ya kusafirisha mama wa kifalme «Safari ya Dhahabu» wakati wa ufunguzi wa Makumbusho ya Ustaarabu wa Misri.