Dkt. Yasmine Fouad, Waziri wa Mazingira wa Misri

Imefasiriwa na / Alaa Zaki
Amezaliwa mnamo Machi 24,1975.
Shahada za Kielimu:
Alisoma katika Shule ya Lugha ya Port Said, kisha akajiunga na sehemu ya Fasihi ya Kiingereza, Kitivo cha Sanaa, Chuo Kikuu cha Kairo, ili kupata Shahada ya kwanza mnamo mwaka wa 1997.
Alipata Uzamili wa Sayansi ya Mazingira, "Jukumu la Usaidizi wa Maendeleo ili Kupunguza Umaskini na Kulinda Mazingira. Uchunguzi wa Miradi ya Maendeleo katika Eneo la Mijini nchini Misri", Taasisi ya Mafunzo na Utafiti wa Mazingira (Chuo Kikuu cha Ain Shams), mwaka wa 2010.
Shahada ya Uzamivu katika Siasa za Kimataifa (Masomo ya Euro-Mediterranean) kutoka Kitivo cha Uchumi na Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Kairo, kuhusu "Athari za Misaada ya Maendeleo wa Uingereza kwa Ushiriki wa Mashirika ya jamii ya kiraia katika Utafiti wa Bonde la Mto Nile, Uchunguzi kutoka Misri."
Pia, Dkt. Yasmine alihudhuria kozi kadhaa za mafunzo, zikiwemo:
Diploma katika tafsiri ya Kiarabu-Kiingereza / Kiingereza-Kiarabu (Chuo Kikuu cha Kairo) mwaka wa 2000.
Kozi ya Upangaji wa Mkakati, Msaada wa Marekani, mwaka wa 2001.
Kozi ya uchambuzi wa mfumo wa kimantiki, Msaada wa Marekani, mwaka wa 2001.
Kozi ya Usimamizi wa Mradi, Msaada wa Marekani, mwaka wa 2001.
Kozi ya ufuatiliaji na tathmini, Msaada wa Marekani, mwaka wa 2001.
Ziara ya mafunzo kuhusu mifumo ya usimamizi wa mazingira iliyogatuliwa nchini Marekani kwa muda wa miezi 3 - mwaka wa 2001.
Mfumo wa usimamizi kwa matokeo, wa awali na ulioendelezwa, kipindi cha 2005-2007.
Tathmini ya misaada ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kupitia viashiria, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa 2009.
Mfumo wa usimamizi kwa matokeo, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa mwaka wa 2009.
Mifumo ya Usimamizi Jumuishi wa Majanga Asilia Septemba, Mfuko wa Kimataifa wa Kupunguza Majanga, Oktoba, mwaka wa 2010.
Kozi ya mafunzo kwa maeneo ya kitaifa ya Kituo cha Mazingira cha Ulimwenguni ili kuandaa miradi ya kupata ufadhili, Washington, mwaka wa 2012.
Kozi ya mafunzo juu ya maendeleo endelevu, Chuo Kikuu cha Colombia, Marekani (Januari-Aprili 2014).
Kozi ya mafunzo kwa wanafunzi kuhusu kuandaa mipango ya kitaifa ya kufanyika, Bangkok, Machi, mwaka wa 2018.
Pia alitoa Maonesho kadha na tafiti nyingi, zikiwemo:
Ugatuaji wa usimamizi na uwezeshaji wa wanawake huko Minya, mradi wa Benki ya Dunia mwaka wa 2003.
Jukumu la misaada ya maendeleo katika kupunguza umaskini na kuhifadhi mazingira nchini Misri, katika Taasisi ya Mazingira ya Chuo Kikuu cha Ain Shams.
Matarajio ya Maendeleo Endelevu, Kitivo cha Uchumi na Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Kairo, mwaka wa 2006.
Ukuzaji wa Uwezo kwa Mabadiliko ya Tabianchi Masomo yaliyopatikana kutoka kwa Mradi wa Kitaifa wa Kukuza Uwezo nchini Misri, Bonn, Ujerumani mwaka wa 2010.
Ujumuishaji wa jinsia katika usimamizi wa Bonde la Mto Nile, katika Kongamano la Kimataifa la Bonde la Mto Nile mwaka wa 2012.
Hadithi za mafanikio kuhusu kusaidia jumuiya za watu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ya kitaifa, katika Kongamano la Kimataifa la Bonde la Mto Nile 2012.
Changamoto za Kitaasisi za Mazingira nchini Misri, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Ripoti ya Changamoto za Maendeleo nchini Misri, Baraza la Mawaziri, mwaka wa 2012.
Utetezi wa manufaa ya kitaifa ya pamoja ya eneo la Bonde la Mto Nile na mipango ya kupunguza mvutano katika Kongamano la Kimataifa la Bonde la Mto Nile, mwaka wa 2013.
Kuunganishwa kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika Bonde la Mto Nile - katika Kongamano la Kimataifa la Bonde la Mto Nile, mwaka wa 2013.
Kusaidia maendeleo endelevu katika eneo la Kiarabu, Chuo Kikuu cha Colombia, na New York mwaka wa 2014.
Mwenendo wa kazi:-
Dkt. Yasmine alifanya kazi katika Wizara ya Mazingira tangu mwaka wa 1997, ili kutoa msaada wa kiufundi kwa ushirikiano wa pande mbili na wa kimataifa pamoja na na wafadhili, kuchambua sera za mazingira, kuandaa mapendekezo ya miradi ya kitaifa na kikanda kwa ufadhili kutoka kwa wafadhili, inayozingatia miradi ya mazingira ya kimataifa, ambayo ni mabadiliko ya tabianchi, bioanuwai, kuenea kwa jangwa, na usimamizi wa kemikali na maji kimataifa.
Wakati wa kazi yake na Umoja wa Mataifa, alifanikiwa kuvutia zaidi ya dola milioni 32 za kimarekani kutoka kwa Mfuko wa Mazingira wa Kimataifa, unaohusika na kutoa misaada kwa nchi zinazoendelea ili kutekeleza majukumu yao ya kimataifa, pamoja na kuhamasisha karibu dola milioni 350 kwa ajili ya miradi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi kupitia kazi yake kama kituo cha mawasiliano ya Mfuko wa Tabianchi ya Kijani kwa Misri, na kwamba katika mwaka mmoja na nusu mnamo akifanya kazi na Waziri wa Mazingira kama msaidizi wake kwa maendeleo endelevu na uhusiano wa nje.
Alisimamia faili la Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira Waafrika chini ya usimamizi wa Waziri wa Mazingira katika wadhifa wake kama Rais wa Mkutano huo, kwa kipindi cha miaka miwili.
Dkt. Yasmine aliwakilisha Misri katika majukwaa mengi ya kimataifa kama vile Baraza la Kituo cha Mazingira Duniani huko Washington, mikutano ya mawaziri ya Kituo cha Mazingira cha Kimataifa nchini Afrika Kusini, mikutano inayohusiana na Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika huko Cote de Varolema, Mikutano ya Sera ya Ujirani huko Brussels, mikutano ya uwezo wa kitaifa wa mabadiliko ya tabianchi nchini Ujerumani, na mikutano ya Gavana wa Baraza la Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa na Maendeleo ya Vijiji vya Kitaifa vya Nchi za Afrika huko Nairobi, ili kuvutia vyanzo vingi vya ufadhili kwa miradi ya kitaifa na kikanda, na kufungua maeneo ya ushirikiano na nchi za Kiafrika na Kiarabu katika nyanja ya miradi ya kimataifa ya mazingira mafanikio kupitia Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa wa kikanda.
Pia, alifanya kazi kama mtaalamu wa kimataifa kutetea ushirikiano katika Bonde la Mto Nile na Jukwaa la Kimataifa la Bonde la Mto Nile, mtandao wa mashirika ya kiraia yanayochangia kukuza dhana ya Nile moja, familia moja. Usawa kati ya Misri, Sudan na Ethiopia, athari za mabadiliko ya tabianchi kwa jamii za wenyeji katika nchi za bonde hilo, ujumuishaji wa jinsia katika usimamizi wa Bonde la Mto Nile, mipango ya utekelezaji ya vikao vya kitaifa na kimkoa ili kuchochea ushirikiano kati ya nchi za Bonde hilo.
Alishiriki katika mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu mjini New York, na alichangia katika uteuzi wa Mtandao wa Waarabu wa Mazingira na Maendeleo kama mwanachama wa kwanza Mwarabu wa Mtandao wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo Endelevu. Na aliandaa pendekezo la kusaidia maendeleo endelevu katika eneo la Kiarabu kupitia kazi yake kama mtafiti mgeni katika Taasisi ya Ardhi katika Chuo Kikuu cha Colombia huko New York, na kuchangia Ufunguzi wa matarajio ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Dunia na Wizara ya Mazingira kuanza kuandaa mradi wa kuanzisha kituo cha kitaifa cha mabadiliko ya tabianchi nchini Misri.
Mnamo kipindi cha Novemba, mwaka wa 2014 hadi Agosti, mwaka wa 2017, Dkt. Yasmine alifanya kazi kama msaidizi wap Waziri wa Mazingira kwa Maendel Endelvna Uhusiano wa Kimataifa na Kikanda, kisha kama mshauri wa Waziri wa Mazingira kwa makubaliano ya kimataifa ya mazingira, na pia alifanya kazi katika kutoa msaada wa kiufundi kwa kusimamia faili za Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi na kushiriki Misri wa Kongamano la kumi na nne la Bioanwani, pamoja na kuwa kituo cha kitaifa cha mawasiliano cha Mfuko wa Tabianchi ya Kijani nchini Misri.
Na mnamo mwaka wa 2017, alichaguliwa kama mhariri mkuu wa ripoti ya mabadiliko ya tabianchi na kuenea kwa jangwa na Kamati ya Kisayansi ya Mabadiliko ya Tabianchi, ambacho kitengo cha kisayansi cha Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi nchini Ujerumani.
Mnamo Juni mwaka wa 2018, Dkt. Yasmine Fouad alishika cheo cha Waziri wa Mazingira. Tangu wakati huo, alikuwa na jukumu muhimu katika kuendeleza ajenda ya bioanuwai na kuandaa mfumo wa bioanuwai wa kimataifa baada ya mwaka wa 2020, kama Mwenyekiti wa Mkutano wa Kumi na nne wa Wanachama wa Mkataba wa Bioanwani (CBD COP14) tangu Novemba 2018. Na alisimamia kushiriki na kuandaa kwa Misri na kuandaa mkutano wa tabianchi wa COP27 mnamo mwaka jana.
Pia alisimamia kubuni, maandalizi na uzinduzi wa mipango kadhaa ya mazingira inayolenga kuongeza mwamko wa mazingira na kuhakikisha ushiriki wa vijana, kama vile mpango wa rais "tayari kwa kijani" kwa kipindi cha miaka mitatu (2020-2023).
Vyanzo
Tovuti ya Wizara ya Mazingira ya Misri.
Gazeti la Al-Ahram ya Misri.