Waziri Amr Moussa

Mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Misri, alishika madaraka ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri kuanzia mwaka 1991 hadi 2001. pia alikuwa katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu kuanzia 2001 hadi 2011.
Amr Moussa alipata Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Kairo mwakani 1957, kisha akajiunga na kikosi cha kidiplomasia katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri mwakani 1958, na alipitia vyeo kadha ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, ambapo alifanya kazi katika idara na jumbe kadhaa za kimisri. na kushika nyadhifa kuu kadhaa , zikiwemo " Balozi wa Misri katika Umoja wa Mataifa. na aliteuliwa na Katibu Mkuu wa “Umoja wa Mataifa” katika kundi la Umoja wa Mataifa inayohusika na hatari, machangamoto na mabadiliko, pamoja na kuwa Balozi wa Misri nchini India , akakuwa mshauri wa Waziri Mmisri wa Mambo ya Nje kwenye Wizara ya Mambo ya Nje mnamo mwaka 1977.
Moussa alitumia muda mrefu wa miaka yake ya kazi yake nchini Marekani, ambapo alikuwa mwakilishi wa kudumu wa nchi yake ya Misri katika Umoja wa Mataifa kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri mwakani 1991, na mnamo 2001 alishika cheo cha Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, na kupitia nafasi yake alizindua mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kiarabu kwa Amani kwa ajili ya kujadiliana na kutatua mzozo wa Waarabu na Israeli, na akabaki kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa ya Kiarabu hadi 2011, ambapo alijiuzulu baada ya kujizulu kwa Rais wa zamani Mubarak kwa siku moja tu, kisha akagombea katika uchaguzi wa Urais wa Misri mwakani 2012.
Amr Moussa alishika cheo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Hamsini ya Kurekebisha Katiba mwakani 2013 katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, ambapo aliteuliwa kuwa mwanachama wa Kamati ya Hamsini iliyoteuliwa ili kurekebisha Katiba ya Misri, kisha wanachama wa Kamati hiyo walimchagua kuwa Mwenyekiti kwake.
Wakati wa kazi yake ya kidiplomasia, mwanadiplomasia wa Misri (Amr Moussa ) alipokea tuzo kadha, ikiwa ni pamoja na Mkufu wa Nile kutoka Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mnamo Mei 2001, na Mkufu wa Nile mbili kutoka Jamhuri ya Sudan mnamo Juni 2001, pamoja na nishani kadhaa ya kiwango cha juu kutoka Ecuador , Brazili, Argentina, Ujerumani, Chile, Qatar, Jordan, na Sudan.