Antonio de Aguirre Patriota... Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Brazil mjini Kairo

Antonio de Aguirre Patriota... Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Brazil mjini Kairo

Imefasiriwa na / Zeinab Mekky


Balozi Antonio de Aguiar Patriota amezaliwa mnamo Aprili 1954 katika jiji la Rio de Janeiro. 


Sifa za kitaaluma:

•Alihitimu kutoka Taasisi ya Rio Branco, Chuo cha Diplomasia cha Brazil mnamo 1979, baada ya kusoma falsafa katika Chuo Kikuu cha Geneva.

 •Alitunukiwa Uzamivu wa heshima katika utumishi wa umma kutoka Chuo Kikuu cha Chatham mnamo 2008.

•Miongoni mwa tafiti zake zilizochapishwa ni tasnifu ya kozi ya Masomo ya juu ya Taasisi ya Rio Branco iliyopewa jina la "Baraza la Usalama baada ya Vita vya Ghuba: Kuunda Mtazamo Mpya wa Usalama wa Pamoja" na juzuu mbili za "Hotuba, Makala na Mahojiano" ya idara hiyo katika uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje. Makala “Je, Ulimwengu Uko Tayari kwa Ushirikiano wa Wingi?” Iliyochapishwa hivi karibuni na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Brazili (CEBRI). 

Uzoefu wa kazi:

 ▪︎Mwanadiplomasia katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Brasilia (1979-1982).

 ▪︎Mwanadiplomasia huko Geneva (1983-1987 na 1999-2003), huko New York (1994-1999), Beijing (1987-1988) na Caracas (1988-1990).

 ▪︎Mwanadiplomasia katika Sekretarieti ya Sera ya Mambo ya Nje katika Wizara ya Mahusiano ya Nje (1990-1992) 

▪︎Mshauri wa Kidiplomasia kwa Urais wa Jamhuri kutoka (1992-1994)

 ▪︎Mshauri wa Kidiplomasia kwa Ujumbe wa Kudumu wa Brazil katika Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani (1994-1999)

 ▪︎Waziri katika Ujumbe wa Kudumu wa Brazil katika Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi (1999-2003)

 ▪︎Katibu wa Mipango ya Kidiplomasia katika Wizara ya Mahusiano ya Nje (2003-2004) 

▪︎Balozi wa Brazil nchini Marekani (2007-2009), Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje (2009-2010), kisha Waziri wa Mambo ya Nje (2011-2013) 

▪︎Mwakilishi wa Kudumu wa Brazil katika Umoja wa Mataifa (2013-2016)

 ▪︎Wakati wa kipindi  cha uongozi  wake wa Ujumbe wa Brazil katika Umoja wa Mataifa, aliongoza vikao vya 61 na 62 vya Kamati ya Hali ya Wanawake na Kamati ya Kujenga Amani (2013-2014).

 ▪︎Mwanachama wa mpango wa "Viongozi kwa Amani", unaoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Ufaransa Raffarin.

▪︎Mwanachama wa kamati la waamuzi wa tuzo ya kimataifa ya "Binti Sabeeka Bint Ibrahim Al Khalifa kwa Uwezeshaji wa Wanawake" tangu 2018.

 ▪︎Balozi wa Brazil nchini Italia, Malta na San Marino kuanzia (2016-2019).

 ▪︎Antonio de Aguiar Patriota ameteuliwa kuwa Balozi wa Brazil katika Jamhuri ya Misri ya Kiarabu  na   Eritrea tangu 2019. 


Vyanzo

Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazil. 

(Haki Miliki ya picha : Jukwaa la Amani la Aswan).