Balozi Christine Burger.. Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Misri

Balozi Christine Burger.. Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Misri

Imefasiriwa na / Ali Mahmoud

Bwana Christian Burger alizaliwa huko Austria.

Sifa za Elimu :

Ana digrii za kisayansi na kitaaluma katika sheria kutoka Vyuo Vikuu vya Vienna na London (Kitivo cha Uchumi cha London).

Uzoefu wa Kazi:

Christian Burger alijiunga na taasisi za Ulaya mnamo Mwaka wa 1997; Alifanya kazi katika usimamizi wa mahusiano na Syria, kisha mshauri wa kisiasa katika masuala ya Mashariki ya Kati. Alifanya kazi katika nyadhifa za awali na Shirika la Usalama na Ushirikiano la Ulaya huko Vienna, Umoja wa Mataifa nchini Syria (UNDOF), na Gaza na Yerusalemu (UNRWA).

Kati ya Miaka ya 2005 na 2006, alifanya kazi kama mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kwa Mjumbe Maalum wa kamati ya pande nne kwa Mashariki ya Kati (James Wolfensohn); ambapo alifanya kazi kimsingi kwenye Mkataba wa Rafah (kivuko cha mipaka kati ya Misri na Gaza).

Mnamo miaka ya 2006 na 2008, alishikilia wadhifa wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Majibu ya Migogoro na Kujenga Amani katika kimisheni ya Ulaya.

Kipindi cha kuanzia Mwaka wa 2008 hadi 2011, alikuwa Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya / Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya huko Yerusalemu.

Kipindi cha kuanzia Mwaka wa 2011 hadi 2016, alishikilia wadhifa wa Mkurugenzi/ Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ya Huduma ya Utekelezaji wa Nje ya Ulaya huko Brussels.

Kipindi cha kuanzia Mwaka wa 2016 hadi 2020, alifanya kazi kama Balozi na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Uturuki na Balozi nchini Turkmenistan.

Tangu Mwaka wa 2020, Christian amekuwa akifanya kazi kama Balozi wa nchi za Umoja wa Ulaya nchini Misri.

Chanzo:

Tovuti ya Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Misri (EEAS).