Balozi Nabil Ismail Fahmy

Balozi Nabil Ismail Fahmy

 Mwanadiplomasia mmisri,aliyefanya kazi hapo awali kama Waziri wa Mambo ya Nje, naye ni mwana wa Ismail Fahmy, Waziri wa zamani sana wa Mambo ya Nje wa Misri ambaye alijiuzulu wakati wa mahojiano ya Camp David mwaka 1979.

Nabil  Fahmy alifanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Nje katika idara kadhaa, kama  mipango ya kisiasa na kama mshauri wa kisiasa wa Waziri wa Mambo ya Nje Amr Moussa mnamo miaka ya 1990 kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Misri nchini Marekani kwa miaka kadhaa mnamo kipindi cha 1999 hadi 2008, pia kabla ya hapo alifanya kazi kama Balozi wa Misri nchini Japan.

Baada ya Balozi Fahmy kurudi Kairo mwaka wa 2008, alishika wadhifa wa Mwenyekiti wa Kituo cha Taasisi ya Montrey cha Mafunzo ya Kuzuia Kuenea kwa Nyuklia katika Mashariki ya Kati na Baraza  ya Ushauri ya Kamati ya Kimataifa ya Kuzuia Uenezaji wa Nyuklia na Kuondoa Silaha, tena  aliteuliwa kuwa Mkuu wa Shule ya Mahusiano ya Umma katika Chuo Kikuu cha  Marekani mjini Kairo.

Fahmy alichukua jukumu kubwa kama mwanadiplomasia katika juhudi nyingi za kuleta amani katika Mashariki ya Kati, na vile vile katika ngazi za kimataifa na kikanda katika masuala ya upokonyaji silaha, ambapo alikuwa mjumbe wa ujumbe wa Misri katika Umoja wa Mataifa, na alichaguliwa kama Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kwanza ya Upokonyaji Silaha na Masuala ya Usalama wa Kimataifa katika kikao cha 44 kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1986, na kuongoza kamati ya maandalizi ya wajumbe wa Misri walioshiriki katika mchakato wa amani Mashariki ya Kati mwaka 1993, na ujumbe wa Misri kwa kikundi kazi cha kimataifa kuhusu usalama wa kikanda na udhibiti wa silaha unaotokana na Mkutano wa Amani wa Madrid mnamo Desemba 1991.

Fahmy aliandika vitabu kadhaa ambavyo vilishughulikia sana siasa za Mashariki ya Kati, Maendeleo, kuleta Amani, Usalama wa kikanda, na Upokonyaji Silaha.