Osama Al-Gohary..Mkuu wa Kituo cha Habari na Kukuza Maamuzi cha Baraza la Mawaziri la Misri

Osama Al-Gohary..Mkuu wa Kituo cha Habari na Kukuza Maamuzi cha Baraza la Mawaziri la Misri

Imefasiriwa na / Aya Nabil


Katika muktadha wa maagizo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kwa kutoa nafasi za uongozi kwa vijana wenye ujuzi na vipaji, na kusukuma vipengele vya vijana; kuchukua nafasi muhimu za uongozi, kwa ajili ya kuchangia katika kubadilisha mawazo, kuchochea uvumbuzi na kuboresha utendaji, Dkt. Mustafa Madbouli, Waziri Mkuu  mnamo Septemba 2019, alitoa uamuzi wa kumteua Profesa Osama Al-Gohari, Msaidizi wa Waziri Mkuu, kufanya kazi za Mkuu wa Kituo cha Habari na Kukuza maamuzi ya Baraza la Mawaziri, kwa muda wa mwaka mmoja, unaoweza kufanyiwa upya.


Vyeti vya kisayansi:

Ana shahada ya Uzamili katika masoko ya kimataifa, kutoka Chuo Kikuu cha Hult, Marekani, 2012.

 Ana shahada maalumu ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uingereza, 2009.

 Ana Diploma ya Uzamili katika Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka Chuo Kikuu cha Marekani huko Kairo, 2008.

Uzoefu muhimu zaidi wa kisayansi:

Mtafiti katika Ofisi ya kiufundi ya Waziri wa Mafuta na Madini mwaka 2007. 

Alishiriki katika kazi nyingi za utafiti kuhusu sekta ya mafuta na gesi.

 Alishiriki miongoni mwa vikundi vya kazi na nyumba za kimataifa za utaalam kuandaa tafiti  juu ya mustakabali wa sekta  ya mafuta nchini Misri. 

Mhadhiri katika uwanja wa uuzaji wa kielektroniki na tabia ya watumiaji - Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Misri (MIU) 2000-2015 . 

Mapema ya mwaka wa 2009, amefanya kazi katika Ofisi ya Kiufundi ya Waziri Mkuu. 

Mchambuzi wa kwanza na kiongozi wa timu, Ofisi ya Kiufundi ya Waziri Mkuu wa Misri tangu Aprili 2016.

Msaidizi wa Waziri Mkuu. Tangu Aprili 2019.  

Osama Al-Gohary ndiye mwenye umri mdogo zaidi miongoni mwa waliotwaa Uenyekiti wa Kituo cha Habari na Kukuza Maamuzi tangu kuanzishwa kwaka 1985 , ambapo alichukua jukumu la kuongoza kituo hicho akiwa na umri wa miaka 38 hadi sasa.


Vyanzo

 Tovuti ya Kituo cha  Habari na Kukuza Maamuzi cha  Baraza la Mawaziri la Misri.