Mshauri Abdulwahab Abdulrazak.. Mwenyekiti wa Baraza la Seneti la Misri

Mshauri Abdulwahab Abdulrazak.. Mwenyekiti wa Baraza la Seneti la Misri

Imefasiriwa na / Osama Mostafa

Mshauri Abdulwahab Abdulrazak amezaliwa mnamo Agosti 1948, katika Mkoa wa Minya, na alipata Shahada ya kwanza ya Sheria mnamo 1969, kwa daraja nzuri, kutoka Chuo Kikuu cha Kairo.

  Mwanzoni mwa miaka ya sabini ya karne iliyopita, Mshauri Abdulwahab Abdulrazak aliteuliwa katika Ofisi Kuu ya Hisabati, kisha akateuliwa kama Msaidizi wa Mwendesha Mashtaka Mkuu, na kisha akateuliwa kuwa "Abdulwahab" Mwakilishi wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa daraja la kwanza, na Naibu katika Baraza la Nchi, na Mshauri Msaidizi wa daraja (b) na daraja (a).

Mnamo 1987, ameteuliwa kuwa Mshauri katika Baraza la Nchi, na baadaye alishika nafasi ya Mshauri katika Tume ya Wanachama wa Mahakama Kuu ya Katiba.

Mnamo 1988, alifanya kazi kama Mshauri katika Tume ya Wanachama wa Mahakama Kuu ya Katiba, na kisha alipelekwa nchini Kuwait kufanya kazi kama Mshauri katika Idara ya Fatwa na Sheria katika Baraza la Mawaziri kuanzia 1992 hadi 1998.

Mshauri Abdulrazak aliteuliwa kuwa Naibu wa Mwenyekiti wa Mahakama Kuu ya Katiba  mnamo 2001, tena akashika nafasi ya Mwenyekiti wa Mahakama Kuu ya Katiba, akimfuatilia Mshauri Adly Mansour kuanzia Julai mosi, 2017 hadi Julai 31, 2018.

Mnamo Machi 2020, Mshauri Abdulwahab Abdulrazak aliongoza chama cha "Mustaqbal Watan" na alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Seneti mnamo Oktoba ya mwaka huo huo.