Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" watembelea Maktaba ya Alexandria kama sehemu ya matukio ya siku ya 12 ya Udhamini huo.

Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" watembelea Maktaba ya Alexandria kama sehemu ya matukio ya siku ya 12 ya Udhamini huo.

Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa " katika toleo lake la pili, uliandaa ziara ya Maktaba ya Alexandria siku ya Jumamosi, ikihudhuriwa na Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , kama sehemu ya matukio ya siku ya 12 ya Udhamini huo, unaoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo ya Kimisri ikiongozwa na Dkt.Ashraf Sobhy, kwa ushirikiano na Taasisi ya kitaifa kwa mafunzo na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kimisri, tena Taasisi kadhaa za kitaifa na hayo yote pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, pia utakaofanyikwa hadi katikati ya Juni ijayo kwa kauli mbiu ya " Ushirikiano wa Kusini-Kusini" kwa ushiriki wa vijana viongozi bora zaidi kutoka  mabara ya Asia, Afrika na Amerika Kusini.

Washiriki wa Udhamini huo walitembelea Maktaba ya Alexandria katika siku ya 12 ya Udhamini huo na waliweza kujifunza historia ya maktaba hiyo na urithi mkubwa wa tamaduni zote, kama vile kuzungumza na maafisa wa maktaba na kutembelea sehemu mbalimbali za maktaba hiyo na kuona sanaa ya ukutani inayowakilisha historia ya Misri ya zamani, amani ya jamii, uvumilivu wa dini, pamoja na misikiti na kanisa mashuhuri ya Misri, na kwa upande wao Watu wa maktaba ya Alexandria pia walitoa maonesho ya kihistoria juu ya Misri na matukio mbalimbali na tamaduni zilizopita, na washiriki hao pia walizuru makumbusho ya Marehemu Rais Mohamed Anwar Al-Sadat,Bingwa wa Vita na Amani, tena wameona mambo ya Kale ya Kiongozi marehemu huyo na mavazi yake rasmi ya kijeshi.

Washiriki wa Udhamini huo, katika toleo lake la pili walielezea furaha yao ya kutembelea Mkoa wa Alexandria, kuona maeneo yake muhimu, na kutembelea Maktaba ya Alexandria kama chanzo cha elimu, wakikazia upendo wao kwa Misri, watu wake, na utajiri wa tamaduni zake za kihistoria. Baada ya ziara yao katika maktaba, washiriki walipiga picha kadhaa kwa furaha kubwa kutokana na uzoefu wao mzuri.

Kwa upande wake, Hassan Ghazali, Mratibu mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  alielezea kuwa Udhamini huo ni moja ya njia za kufikia lengo la nane la Maoni ya Misri 2030, ambalo ni kufikia na kuimarisha nafasi ya uongozi ya Misri, ambapo Ajenda ya kitaifa ilihakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo yanahusiana na malengo ya kimataifa kwa upande mmoja na ajenda ya kikanda haswa Ajenda ya Afrika 2063 kwa upande mwingine, basi baada ya Misri kufanikiwa katika kurejesha utulivu wake na kuboresha mahusiano yake na nchi za nje, lengo la kukuza nafasi ya Misri na uongozi wake katika ngazi za kikanda na kimataifa imekuwa ni lazima ili kuchochea maendeleo kamili, hilo ndilo linaloweza kufanikiwa kwa njia nyingi ikiwa ni pamoja na kusaidia kuboresha ushirikiano wa kikanda na kimataifa, hivyo ndivyo ilivyokuja kuwa kauli mbiu ya Udhamini huo "Ushirikiano wa Kusini-Kusini" kama mojawapo ya njia hizo.

"Ghazali" aliongeza kuwa Udhamini huo unalenga kuhamisha uzoefu mkubwa wa Misri katika kuzingatia na kujenga taasisi za kitaifa na kuunda kizazi kipya cha viongozi wa mabadiliko vijana wenye maoni yanayofanana na mwelekeo wa Rais wa Misri katika nchi mbalimbali kwa njia ya kuingiliana, pamoja na kushirikisha viongozi  vijana wenye athari kubwa ulimwenguni kote kupitia mafunzo, ujuzi na mitazamo ya kimkakati.