Jeshi ni Shule inayojumuisha maafisa wakuu, maafisa wadogo na askari.. na Shule hiyo inaelezea sura ya nchi, ndio maana inaunganisha wananchi
Imefasiriwa na / Fatma Mahmoud
Ndugu Zangu:
Nawashukuru kwa mwaliko huu uliotuwezesha kukutana kwenye mahali huko, na ambao ulitupa fursa ili kuona mioyo ionekane nyusoni.
inawezekana Madhalimu na watu wenye nia mbaya kujaribu waletee ugomvi kati ya watu wa nchi hiyo ili kutenganisha kati ya ndugu na wananchi, lakini mimi leo ninapokuwa pamoja nanyi , sikuona kuwa mimi ni mgeni kwenu , bali nahisi kuwa kama naishi katika hali niliyoishi zamani mnamo mwaka 1938 wakati nilipokutana na makundi na aina ya watu mbalimbali .
Jeshi ni Shule inayojumuisha maafisa wakuu, maafisa wadogo na askari, na Shule hiyo inaakisi hali ya nchi kwani inawaleta pamoja wananchi, na hisia hizo ndizo ninazohisi sasa hivi ninapokuwa pamoja nanyi .
Hapo zamani , walijaribu kuwatenganisha watu wa nchi na kuwagawanya katika makundi, kwa hiyo Je ,wanaweza leo kutenganisha damu, mioyo, au hata hatima , na ardhi?!
Jambo linalotuunganisha kwa kweli ni " lengo" vilevile, mioyo inatuunganisha na damu inatuunganisha, na hiyo ndiyo maana ninayohisi leo.
Maadui wa mapinduzi hawatafanikisha kuwagawanya watu wa nchi hii katika makundi na madhehebu kama walivyokuwa wakifanya zamani kwa kusambaza roho ya uchoyo na chuki, basi nchi hivi karibuni imeshabadilika na mapinduzi hayo yamekuja kama hatua ya maana katika historia yake ambapo yalikuwa mwanzo wa enzi inayoundwa kwa upendo na ushirikiano kwa maslahi ya mtu mmoja na watu wote ambapo kila mtu kipindi hiki hajifikirii yeye mwenyewe, bali anaifikiria nchi yake kama ya kitu chochote .
Tuko na njia ndefu, na mapinduzi hayo si mapinduzi ya jeshi, lakini ni mapinduzi yenu nyinyi , mapinduzi ya nchi, na si mapinduzi ya Gamal au Salah, au mtu fulani; kwani watu huondoka, na mapinduzi ni mapinduzi ya raia ambayo yanafanya juu chini ili kufikia malengo yao ya juu.
Ndugu Zangu:
Shida ni nyingi na kubwa, nanyi mliona mnamo mwezi uliopita maadui katika ndani na nje ya nchi wakitega kuwadanganyeni kwa maneno ya kuvutia , kwa hivyo, inapaswa mioyo na roho zisafishwe ili tuweze kujenga nchi tunayoishi.
Jukumu hili si jukumu dogo, kwani kila mtu lazima afikirie nchi yake na mtoto wake na kaka yake anapojifikiria mwenyewe .
Na hisia hii lazima ionekane kwenye kila mahali, na nilihisi hayo yote nilipokuwa jeshini,pia nilihisi utu wa mmisri , kujitolea kwake na uaminifu wake , ambapo Katika vita vya Palestina, nilimwona mwanajeshi akipigana wakati alikuwa hana lengo isipokuwa uaminifu wake , na alikuwa anakufa kwa ajili ya uaminifu huu na utu huu . vilevile , tuliweza kwa utu huu , kukaa ili kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii kwa lengo la kuifanya Misri kuwa nchi kubwa.
Leo, nyinyi ni walinzi wa usalama, kwa hiyo mna jukumu kubwa, na mlipata fursa ya kuwasiliana na makundi yote.
Ndugu Zangu:
Mapinduzi hayo ni mapinduzi ya kina, si mapinduzi ya juu juu, na malengo yake hayafikiwi ghafla au kwa uchawi, lakini kwa kazi, kwa umoja na kwa upendo ambapo Ubomoaji ni rahisi, lakini ujenzi unahitaji kazi, jasho na bidii ya kila mmoja. inawezekana ujenzi kuwa kwa maadili badala ya nyenzo, lakini tunaweza kuanzia ujenzi wa nyenzo baada ya hayo , na sisi -Ndugu Zangu-, lazima tuishi katika nchi huru na yenye ukarimu, na lazima sote tuungane ili kufikia malengo hayo.
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Klabu ya Konstebo.
Mnamo Aprili 15, 1954.