Kairo... Mkutano wa pili wa kilele wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote

Kairo... Mkutano wa pili wa kilele wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote

Mkutano wa Pili wa nchi zinazofungamana upande wowote ulifanyika Oktoba 5, 1964, ukiwa na mahudhurio ya wafalme na marais 58, lakini mahudhurio ya Waziri Mkuu wa Congo Tshombe yalikuwa  mgogoro kwa wengi wa washiriki wa mkutano huo; wengi wao walikataa kuketi pamoja naye;kwa sababu Tshombe anatuhumiwa kumuua Lumumba, Shujaa wa Harakati za ukombozi wa taifa nchini Congo, pia alimuua Hammarshulid, katibu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, na Rais wa Algeria Ahmed Ben Bella alimweleza, akisema: "Tshombe ni Mfuasi wa Ukoloni  na anaegemea upande wowote tunaopinga."

Rais wa Yugoslavia Tito, Mwenzake wa Algerai Ahmed Ben Bella  na Gamal Abd El Nasser walikutana nyumbani kwa Rais wa Jamhuri wakishauriana pamoja, Mwishoni waliamua kupeleka wito kwa Rais wa Jamhuri ya Congo Kasavubu kumwambia  wakieleza utashi wa kutohudhuria Tshombe, na  kumkaribisha Rais binafsi kuiwakilisha nchi yake, kwa lengo la kuuepusha mkutano huo na matatizo yasiyo ya lazima yanayozuia mwenendo wake wa kawaida.

Na ingawa kuna nchi ambazo hazipendi mahudhurio ya Tshombe, Lakini kulikuwa na nchi tatu za Kiafrika zilizounga mkono mahudhurio yake, nazo ni (Senegal – Nigeria – Liberia). Zikisema kwamba kusisitizia suala  hilo ni kama kuingilia masuala ya ndani ya Congo.