Kituo cha Habari na Usaidizi wa Kuchukua Uamuzi

Kituo cha Habari na Usaidizi wa Kuchukua Uamuzi

Imetafsiriwa na/ Enas Abd El-Basset
Imehaririwa na/ Nourhan khaled

Kituo kilichoanzishwa mnamo mwaka 1985 , kilichopitia mabadiliko kadhaa,ili kuendana na mabadiliko ambayo jamii ya kimisri imepitia. Katika kipindi chake cha kwanza (1985- 1999), ilihusu  kuendeleza usanifu wa habari nchini Misri .Kisha kuanzisha Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari mwaka (1999 ) ikuwa hatua kubwa ya mabadiliko katika safari yake,ili kufanya kazi bidii kwa jukumu lake kama shirika la mawazo (think tank)  linalounga mkono juhudi za mtendaji wa maamuzi katika nyanja mbalimbali za maendeleo, na akifanya mazungumzo na jamii, na kujenga mitandao ya mawasiliano na raia wa Misri, ambayo inachukuliwa kuwa lengo la maendeleo na lengo lake kuu .

Hatua za Maendeleo ya Kituo Hiki:
  Hatua ya Usanifu wa Habari
(Kuanzia kipindi cha 1985 hadi  1999 ) 
Kituo hiki kilishughulika kuunda usanifu wa habari katika kipindi hiki ambacho kinahakikisha  kasi ya mtiririko wa maelezo na habari , na pia  kuchangia katika michakato ya maendeleo ya teknolojia nchini Misri .

Hatua ya Usaidizi wa Kuchukua Uamuzi na Upatikanaji wa Habari 
(Kuanzia kipindi cha 1999 hadi 2005 ) 
Hatua hii iliyopitia mabadiliko makubwa katika hali ya jukumu la kituo hiki ili kuwa na utaalamu zaidi katika uwanja wa usaidizi wa uamuzi kwa kutoa njia za kisayansi na za vitendo na mchakato unaosaidia kushughulikia masuala mbalimbali ya maendeleo,tangu wakati huo, inajenga maono ambayo maudhui yake ni  kuweka kituo hiki maalumu katika uwanja wa kusaidia kufanya uamuzi katika masuala mbalimbali ya kina ya maendeleo ya pamoja na upendezi wa kujenga jamii ya maarifa .
Hatua ya Mapatano ya kiakili ya Baraza la Mawaziri
Kuanzia 2005  hadi sasa……
Katika kipindi hiki – kama kituo cha mawazo cha Baraza la Mawaziri la Misri – Kituo kilihakikisha kwa kuunga mkono juhudi za anayechukua uamuzi kuhusu masuala ya kina ya maendeleo, na kujenga jamii ya maarifa na habari, kwani Kituo kinachangia katika hatua mbalimbali za sera za umma ,kuanzia na kushiriki katika kutambua masuala na kupanga vipaumbele vyake, kupitia hatua ya kuchangia kusaidia uamuzi kwa kutoa njia mbadala na mapendekezo mbalimbali kwa kuzingatia utaalamu na majaribio wa kimataifa, hadi kufikia hatua ya kurudisha nyuma ambapo  kituo hufuatilia  maoni na kutathmini athari zinazotokana na kutekeleza sera na maamuzi.

Jukumu la Kituo Hiki 
Kituo kinashughulika kwa kutimiza kundi ya wajibu na majukumu mbalimbali na hii inaendana na matakwa na mahitaji ya anayechukua uamuzi,na wakati huohuo inapatana na mahitaji  ya  wananchi na hali ya mabadiliko ambayo Wamisri walikuwa wakipitia ,na majukumu haya ni :

Msaada wa habari
Kituo kinatilia manani  kuiwezesha jamii ya maarifa kwa kutoa habari sahihi na ya kisasa ili kusaidia anayechukua maamuzi , na pia kwa upande mwingine  kutoa jamii ya wanufaika (wananchi, jamii yenyewe, ...) maarifa, habari za hali ya juu na  maendeleo,  katika maudhui hiyo, yafuatayo yanafanywa:
• Kuendeleza nyenzo za mawasiliano na jamii ya wanufaika ( Majukwaa ya kielektroniki , kurasa za mitandao ya kijamii, na Programu za kielektroniki).
• Utajiri wa maudhui ya maarifa ambayo yanapatikana mara kwa mara kwa kutoa matoleo tofauti ya kituo .
• Kuzingatia kuongeza ufahamu wa jamii kwa kuzindua kampeni na vifaa mbalimbali vya ufahamu.

Kusaidia Uundaji wa Sera za Umma
Kituo hiki kinashughulika waziwazi kwa kutoa habari na maarifa ambayo inawezesha anayechukua uamuzi kufanya hatua na taratibu zinazofaa zitasaidia juhudi za maendeleo na utekelezaji wa mipango ya mageuzi ya jumla, kwa njia ya:
• Kushughulikia masuala mbalimbali ya maendeleo kwa utafiti na uchambuzi wa kina, na kutoa njia mbadala bora, suluhisho na mapendekezo.
• Kutoa maoni na matukio yaliyo muhimu ili kukabiliana na changamoto mbalimbali.
• Kutumia vifaa mbalimbali vya uchambuzi ili kumsaidia anayechuka uamuzi na kujenga viashiria vilivyojumuishwa na mifano ya kawaida ili kuchambua mahusiano kati ya vigezo na kutambua njia mbadala zinazopatikana.
• Ufuatiliaji na utafiti wa maendeleo na wa matukio yote ya hivi karibuni  kwenye nyanja za ndani na kimataifa kwa vipimo tofauti, na kutoa mapendekezo muhimu kwa kuzingatia utaalamu na majaribio wa kimataifa.
• Kuunda jukwaa la kuwasiliana na masuala na vitu vinavyoibuka kwa kufanya mfululizo wa mikutano na vikao na wataalamu ; kubadilishana maono na mawazo na kutoa mapendekezo muhimu.

Kuchanganya kwa Kijamii 
Kituo daima hujitahidi kukuza mawasiliano ya mara kwa mara na wananchi kama washirika na watendaji katika kusaidia juhudi zote za maendeleo nchini, kwa kupendezwa na kujua mwelekeo na maoni yao kuhusu masuala kadhaa yanayotokea, kwa kutumia vifaa na njia mbalimbali za ufuatiliaji ambayo Kituo kina, pamoja na :
• Ufuatiliaji wa vyombo vya habari na uchambuzi wa masuala mbalimbali na maudhui yanayotokea na vyombo vya habari na kutoa picha kamili juu yake ili kusaidiza anayechukua uamuzi.
• Ufuatiliaji wa matukio yote, maendeleo, changamoto na mafanikio yaliyopatikana kupitia timu za ufuatiliaji zilizoko katika mikoa mbalimbali ya Jamhuri.
• Uchunguzi na utafiti wa maoni ya umma unaokusudiwa kuchunguza mwelekeo wa maoni ya umma kuhusu masuala ya kipaumbele .
• Mfumo wa malalamiko ya serikali, ambapo malalamiko ya wananchi hushughulikiwa na Kuwasiliana na mamlaka husika ili kupata suluhisho.
• Vituo maalumu vya uchunguzi vinavyochunguza masuala maalumu na kutambua mwelekeo wa mabadiliko kuhusu hiyo .

Kuunga Mkono Jitihada za Mabadiliko ya Kidijitali 
Kituo hiki kinashughulika kushirikiana na mamlaka husika katika kuunga mkono mwelekeo wa nchi kuelekea mabadiliko ya kidijitali kwa kuzingatia uzoefu wake mengi katika uwanja huu, kwa kutoa kundi la suluhisho la teknolojia na huduma za kitaalamu,ambapo kinasimamia maendeleo ya kundi la mifumo, tovuti na programu za teknolojia za kisasa ambalo linachangia kuboresha  muundo wa kiteknolojia wa taasisi za serikali, pamoja na kutoa huduma za kituo cha data na ushauri wa kiufundi, na pia huduma za kimawasiliano na kutoa mifumo ya ulinzi na usalama.

Kuboresha Mfumo wa Kukabiliana Na Matatizo Na matatizo
Kituo hiki kinasimamia utawala wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mgogoro, matatizo na Kupunguza hatari, na katika muktadha huu inafanya kazi kulingana na kundi la kazi ambayo ni pamoja na: . 
• Kuandaa mikakati na mipango ya kitaifa ili kupunguza hatari za tatizo.
• Kuongeza ufahamu wa jamii na kutekeleza mipango ya mafunzo na mafunzo ya uwanjani katika usimamizi wa shida na tatizo.
• Kuchangia kuboresha ufanisi wa taasisi za serikali, na kuimarisha uwezo wake wa kukabiliana na matatizo na tatizo .
• Kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kikanda na mamlaka mbalimbali maalumu ya kimataifa.
• Kuzingatia utumiaji bora wa njia mbalimbali za kiteknolojia za kisasa ili kufuatilia matukio na maendeleo kwa kuendelea kupitia uanzishaji wa chumba cha operesheni kuu na chenye vifaa vya teknolojia ya kisasa.
Kituo cha habari na usaidizi wa kuchukua uamuzi wa Baraza la Mawaziri kina watafiti (421) wa kitaalamu katika nyanja nyingi; kati yao (80) ni watafiti wa kisiasa, (64) ni watafiti wa uchumi, (18) ni watafiti wa takwimu, na (37) ni watafiti wa usimamizi wa biashara. Kwa pamoja na (18)watafiti wamehusishwa katika maeneo mengine ya kimataifa kama vile jamii ya kisiasa, falsafa, saikolojia, sayansi, mazingira, usimamizi wa mgogoro na wengine.Katika mfumo wa maendeleo ya kibinafsi ya watafiti wa kituo hiki, watafiti (224) kati ya jumla ya (421) walipata shahada ya uzamili katika maeneo maalumu, wakati watafiti (41) walipata shahada ya udaktari, na watafiti (39) walipata diploma maalumu za kiufundi. 

Yote haya yamefanya kituo hiki kuwa na jukumu kubwa katika utengenezaji wa sera za umma,kuimarisha uwezo na ufanisi wa juhudi za maendeleo, na kuiwezesha jamii ya maarifa.Kituo hiki kilipata kutambuliwa kikanda na kimataifa kwa jukumu lake muhimu kama taasisi ya mawazo, hivi karibuni matokeo ya “Programu ya Vituo vya Mawazo na Jamii za Kiraia (Think Tanks and Civil Societies
Program, TTCSP) ya Chuo Kikuu cha Pennsylvania, USA” iliyotangazwa mnamo Februari 2021; ambapo Kituo cha Habari na usaidizi wa kutoa maamuzi kilichaguliwa kuwa:
Ni miongoni mwa kituo 20 bora zaidi za mawazo duniani
zinazohusika/zinazokabiliana na janga la COVID-19 la 2020 (hakuna mpangilio maalumu wa orodha) .
Na nafasi ya 21 kati ya vituo (64) vya mawazo ulimwenguni yote kama mmiliki wa wazo bora au mfano mpya aliouendeleza wakati wa 2020, kwa kuzingatia kwamba hakuna kituo kingine cha mawazo cha Misri kilichoainishwa kulingana na kiwango hiki. Katika nafasi ya 14 kati ya jumla (101) katika Afrika na Mashariki ya Kati kwa mwaka 2020.
Kituo hiki kilishinda tuzo kadhaa, ni :
• Mashindano ya silaha ya serikali yenye ujanja (2021 ).
• Ushuhuda wa kujitolea kwa ubora (2020).
• Tuzo ya Stevie ya (2020).
• Tuzo ya mpango bora au programu ya usimamizi wa maarifa (2011).
• Tuzo ya Utafiti Bora kutoka mkutano wa Utafiti wa Kiuchumi la Kuwait (2006).
• Nafasi ya pili katika uwanja wa kukusanya habari (2005). 
• Mashindano ya uwepo wa serikali kwenye mtandao (2005).
• Tuzo ya Mohammed bin Rashid Al Maktoum ya Usimamizi wa Kiarabu (2003).
• Tuzo ya Stockholm ya Changamoto (1999).
• Tuzo ya kwanza kutoka kwa jumuiya ya mifumo ya habari za mjini na kikanda (1997).
• Tuzo ya Mradi wa (G7) wa ubunifu wa ulimwenguni (1997).
• Medali ya dhahabu ya mwaka (1996) kwenye maonesho ya kimataifa ya mtandao. 
• Tuzo ya Shirika la Kimataifa la mipango ya mjini (1996).
• Mashuhuri 100 wa jarida la ulimwengu wa kompyuta (1995).
• Tuzo ya kwanza ya Shirika la Frank Edelman la Usimamizi (1995).

Na si ajabu, kwamba nafasi wa hivi karibuni wa kituo hiki ni matokeo ya uwekezaji mzuri katika utajiri wa kweli wa kudumu ambayo ni timu ya watafiti na wataalamu wa kituo hiki cha ndani, pamoja na mtandao wa wataalamu wa nje .

Vyanzo:
Tovuti ya kituo cha habari na usaidizi wa kuchukua uamuzi.

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy