Bweni la Ujumbe wa Kiislamu.. Mji wa Mabalozi

Bweni la Ujumbe wa Kiislamu.. Mji wa Mabalozi
Bweni la Ujumbe wa Kiislamu.. Mji wa Mabalozi
Bweni la Ujumbe wa Kiislamu.. Mji wa Mabalozi
Bweni la Ujumbe wa Kiislamu.. Mji wa Mabalozi
Bweni la Ujumbe wa Kiislamu.. Mji wa Mabalozi
Bweni la Ujumbe wa Kiislamu.. Mji wa Mabalozi

Imetafsiriwa na/ Rahma Rajab 
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
 
Al-Azhar Al-sharif inawakilisha uislamu ulio sahihi na wa wastani. Wanafunzi wanakujia kutoka ulimwenguni kote ili kufaidika na elimu zake, na kujifunza mawazo sahihi ya kiislamu, maadili mema bila ya miimamo mikali  au mapambano, wanarudi nchi zao kama wasomi wanapokea ujumbe mwema wa kiislamu kama walivyojifunza kwenye Al-Azhar.

Kwa hivyo, Al-Azhar inatilia manani kupatikana makazi  kwa wanafunzi hao kwenye mabweni ya ujumbe wa kiislamu ambayo ni mojawapo ya ukanda wa  Al-Azhar, tangu  uanzishaji wa Al-Azhar inazingatia wanafunzi wanaokuja kutoka nje kwa uangalifu ambapo inazingatiwa vituo vikubwa zaidi na umuhimu vya kuvutia wanafunzi kutoka ulimwenguni kote ili kupata elimu.

Kwenye mtaa wa El-darasa, mashariki mwa mjini Kairo huko nchini Misri, karibu na makao makuu ya Al-Azhar na kwenye bustani ya Al-khaldin, uko mji wa Al-Fandaka na utalii mzima, unayopatikanishwa na Al-azhr Al-sharif ili kuwa dira ya wanafunzi wa elimu za kiislamu kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu, wanaotakia kujifunza kwenye chuo kikuu cha Al-Azhar.

Wazo la kuanzisha bweni la ujumbe wa kiislamu lilirejelea enzi ya mfalme Farouk , alipopendekezwa na sheikh ya Al-Azhar wakati huo, kuanzisha mji unaokusanyika wanafunzi wa Al-azhr, ambapo idadi ya wanafunzi waliokuja kutoka nje ya nchi imezidi na maeneo ya Al-azhr yamekuwa  madogo, jambo ambalo limewafanya kuanzisha bweni la ujumbe wa kiislamu ni jambo lililokuwa lazima kufanywa, imepokelewa misaada mengi ili kuuanzishwa,kisha agizo la kifalme limetolewa la namba 34 la mwaka 1952, kwenye Mei 6,1952 ili kuanzisha “ bweni la Farouk 1 kwa jumbe za kiislamu”, kwa kiwango cha paundi elfu 20  kimeainishwa ili kuuanzishwa, na Mwanamfalme Mohamed Abd El-mneim ametawala uwenyekiti wake.

Kufuatia mapinduzi ya julai,1952, mradi umesimamisha, kisha wazo linazukia mara tena, jambo ambalo limelifanya Baraza la Mawaziri kutoa uamuzi kwenye Novemba, 1954 ili kuanzisha bweni la chuo kikuu kwa wanafunzi wote wanaikujia Al-Azhar, ardhi iko karibu na Al-Azhar imeainishwa ili kuuanzishwa, na serikali imeuhesabi kile unachokihitaji kutoka pesa ya kujenga, samani, makazi, lishe na usimamizi.

Bweni hilo limeepoanzishwa umepokea takribani wanafunzi wa kiume na wa kike elfu tano, wanafunzi wa kiume wanakaa ndani ya bweni kubwa hilo na wanafunzi wa kike wanakaa kwenye bweni ndogo ambayo iko mbele ya bweni kubwa, wakati huo walikuja kutoka nchi arobaini, wanafunzi walianza kukaa kwa mara ya kwanza kwenye septemba 15,1959 baada ya ilifunguliwa na hayati Rais Gamal Abd El-Nasser pamoja na Mhe. Sheikh ya Al-Azhar Mahmoud Shaltot wakati huo.

 kinachovutia zaidi bwenini ni uzito wa mfumo, utulivu na usafi wa barabara , pamoja na nafasi kubwa za kijani zilizojaa miti na maua ili kufanya mahali kuwa na asili njema na kumfanya mtu kujisikia faraja ya kisaikolojia .

Bweni lili kwenye ardhi ambayo ukubwa wake ni elfu 163 mita, miongoni mwake elfu 42 mita kwa bustani na barabara, na elfu 84 mita kwa majengo ya makazi na mambo ya matumizi ya pamoja, imeshajengwa majengo ya makazi 43 mita, kila jengo lina ghorofa tatu, na limegawanyika kwa sehemu mbili, sehemu ya Kwanza ina majengo 35 kwa wanafunzi wa uume, sehemu ya pili ina majengo 8 kwa wanafunzi wa kike , na iko barabara ya msingi kati yao, na bweni la ujumbe wa kiislamu lina wanafunzi wa uume na wa kike kutoka nchi 105 pasipo na tofauti au ushabiki wowote, ambapo dini nzuri ya kiislamu inawafanya pamoja kwa maana zake za kuungana na uvumilivu.

Bweni hilo linajumuisha klabu za kijamii, wakati mwingine,wanafunzi wanakutana ili kusoma magazeti ya kila siku, majarida ya asubuhi na ya kila wiki, na  kutazama programu za runinga, vilevile lina migahawa inayotoa vyakula kwa wanafunzi wanaokuja kutoka nje ya nchi.

Mji una msikiti mkubwa , ukubwa wake ni zaidi ya mita mraba 1500, hufanyikiwa mihadhara,semina na vituo vya kuhifadhia na kusoma  quran tukufu, vilevile bweni hufanya tafiti za kimaktaba miongoni mwa wanafunzi, na semina za kukutana kwenye matukio ya kidini na ya kitaifa zilihudhuriwa na wataalamu wakuu wa sheikh za Al-azhr.
Maktaba inajumuisha vitabu vingi vya kidini, pamoja na makundi mengine ya vitabu vya kiutamaduni, kijamii na kisayansi.
Bweni linatoa huduma kadhaa kwa wanafunzi wake ambapo limetoa ruhusa kwa baadhi ya wafundi wanatoa huduma zinazohitajika na  wanafunzi kufungua baadhi ya maduka kama: kinyozi, ushonaji na hata maduka ya kuosha nguo.

 kila msimu wa Hajj,  wake mzuri zaidi , bweni hilo linachagua wanafunzi wake walio bora zaidi waliotambuliwa na wima, uchamungu na ubora wa kisayansi ili kufanya hajji kwa gharama yake.

Mnamo mwaka 1967, usimamizi wa bweni umeanzisha sanduku la kuhudumia wanafunzi kutoka nje, wanafunzi wote kwenye bweni wanaweza kulishiriki na kulingana na ushiriki huo, mwanafunzi yeyote au anayekaa bweni, anaweza kupata mkopo kutoka pesa za sanduku na kuulipa kwa sehemu ndogo, vilevile sanduku linatoa misaada kwa wanafunzi walio maskini, na linalipia mambo mengine kama shughuli za kiutamaduni na za kijamii.
 
Bweni linaendelea kufikia malengo yake ya kupatikana njia za kistarehe kwa mwanafunzi kutoka nje ili waweze kusoma kwa bidii, kukuza uhusiano na kuondoa utofauti baina ya watu wa ulimwengu wa kiislamu ambapo inawakusanya umoja wa itikadi na undugu wa kidini hata ikiwa wanazungumza lugha tofauti au wanaishi mahali mbalimbali, na pia kupinga ubaguzi unaotofautisha watu kwa wakubwa na watumwa ambapo watu wote kwenye uislamu ni mmoja, hakuna mtu bora zaidi ya mtu mwengine, ila ya uchamungu wake, na bweni linafanya kupatikana kwa utulivu wa kisaikolojia na uangalifu wa kiafya kwa wanafunzi kutoka nje kupitia uangalifu wa kiutamaduni, wa kijamii na kichezo ili kusahihisha tabia. Pamoja na kuwapa sehemu tofauti za elimu za kidini ili warudi nchi zao kama wahubiri na mabalozi kwa uislamu.

Na kwa uzingatie wa Rais Abd-Elfatah Elsisi kwa kuangalia idadi inayozidi ya wanafunzi kutoka nje, ameamua kuainisha ardhi 170  mjini mpya ili kuanzisha mji mpya wa ujumbe wa kiislamu ambao utakuwa mji mwenye vitu vyote ili kuhudumia wanafunzi kutoka nje na utapokea kila mwaka zaidi ya wanafunzi elfu 40 wanaotaka kusoma kwenye Al-azhr kutoka ulimwengu kote.

Mnamo aprili, 2016, sheikh Al-Azhar na mfalme wa Saudi Arabia Salman Bin Abd El-aziz walianzisha awamu ya pili ya bweni la ujumbe wa kiislamu, baada ya awamu yake ya kwanza imetekelezwa kupitia ziara yake kwa Al-Azhar na taasisi zake.

Kuna sehemu nyingine mjini Alexandria ili kupatikana makazi na chakula kwa wanafunzi wa nje wanaoikaa, na pia uangalifu wa kimaisha, kijamii, kiutamaduni, kichezo na kitiba, kunaendelea sasa kuanzisha bweni la tatu la jumbe mkoani Qina, pembezoni mwa Misri kwa sababu ya idadi kubwa zaidi ya wanafunzi kutoka nje wanaofaidika na uangalifu tofauti, vilevile kurejea kuendeleza majengo kadhaa bwenini mwa ujumbe mjini kairo ili kupanuza ukubwa wake, kuuzidishia majengo mengine.

Kwa hivyo, wahitimu wa chuo kikuu cha Al-azhr na wana bweni  la ujumbe wa kiislamu kutoka nchi tofauti za kiafrika, kiarabu na kiislamu ni nguvu imara kwa Misri, walikuja kwa nchi ya Al-azhr wakitakia elimu, na walirudi kwa nchi zao kama wahubiri, wataalamu wa kidini, mawaziri na viongozi wa serikali , hakuna nchi haziwana wanafunzi wa Al-Azhar, wanapenda sana Al-Azhar Al-sharif ambayo ni kituo kikubwa cha uislamu wa wastani mwema , na pia misri nchi ya utulivu kwa elimu na utamaduni wanayoupata.

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy