Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa aongoza ujumbe wa Mtandao wa Vijana wa Sudan katika mkutano na Mfumo wa Juu wa Umoja wa Afrika

Imetafsiriwa na: Toka Mosaad Yusef
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

Mnamo tarehe Jumanne, Julai 16, katika hatua muhimu ya kuimarisha jukumu la vijana katika kufikia amani na mabadiliko ya kidemokrasia, Muhannad Orabi, mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, aliongoza ujumbe wa Mtandao wa Vijana wa Sudan kumaliza Vita na kuanzisha Mpito wa Kidemokrasia ya Kiraia, katika mkutano na Mfumo wa Juu wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Mkutano huo uliongozwa na Mohamed Ben Chammas, Mwenyekiti wa Mfumo wa Juu wa Umoja wa Afrika.

Muhannad Orabi aliwasilisha dira ya mtandao huo juu ya jukumu la Umoja wa Afrika katika kuunganisha Sudan, kushughulikia mgogoro wa sasa na kufikia suluhisho kamili la mgogoro. Pia alisisitiza umuhimu wa vijana na wanawake kushiriki katika majadiliano na kujumuisha maono na ajenda zao, ili kuhakikisha ushiriki mpana na ufanisi wa sekta zote. Alitoa wito wa kuwezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu ili kupunguza mateso ya wale walioathirika na shinikizo kwa pande zinazozozana kulinda wafanyakazi wa misaada.

Kwa upande wake, Mohamed Ben Chammas alisisitiza kuendelea kwa juhudi za mashirika ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na vyombo vingine vya kikanda, na kufanya mashauriano na Wasudan wote ili kupata njia iliyokubaliwa. Alielezea umuhimu wa kuratibu na Mtandao wa Vijana wa Sudan na vyombo vingine vya vijana, ikiwa ni pamoja na maono yao katika michakato ya mazungumzo inayoendelea, na kuhakikisha ushiriki na uwakilishi wa vijana katika hatua inayofuata. 

Pia ametoa wito kwa Mtandao wa Vijana wa Sudan kushirikiana na vyombo vingine vya vijana kuwashinikiza watoa maamuzi kusitisha vita na kuanzisha kipindi cha mpito cha kidemokrasia. Alisisitiza kuwa vyombo vya vijana vinaweza kuchukua jukumu kubwa katika kuanzisha hasara za vita na kuongeza ufahamu wa madhara yake, ndani ya mfumo wa kuratibu juhudi mbalimbali za kukomesha. 

Benchammas alisema kuwa Umoja wa Afrika unapanga mkutano wa vijana wa Sudan mwishoni mwa Agosti katika mji mkuu wa Kenya, huko Nairobi, kushauriana nao kuhusu suluhisho zilizopendekezwa na Umoja wa Afrika.