Mfumo wa Udhibiti wa Kiafrika

Mfumo wa Udhibiti wa Kiafrika

Mfumo wa Udhibiti wa Afrika unaojulikana kama  AGA ni jukwaa la mazungumzo kati ya wadau mbalimbali waliopewa dhamana ya kukuza utawala bora na kukuza demokrasia Barani Afrika, nao umetokana na Sheria ya kimsingi ya Umoja wa Afrika inayoashiria malengo husika ya kukuza na kulinda haki za binadamu na watu kijumla, kuimarisha taasisi na Utamaduni wa Kidemokrasia, tena kuhakikisha Utawala Bora na Utawala wa Sheria”, na lengo kuu ni kutekeleza maadili ya pamoja ya Umoja wa Afrika na haswa Mkataba wa Afrika kwa Demokrasia, Uchaguzi na Utawala, na mfumo wa AGA uko na sehemu nne kuu zikiungana nazo ni : Sheria na Vigezo, Taasisi na wengine wenye maslahi, Taratibu na shughuli za mawasiliano, na Kurahisisha Utawala wa Kiafrika.