Chuo cha Mafunzo cha Kitaifa ni mshirika wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa 2021

Imefasiriwa na / Mervat Sakr
Chuo cha Kiaifa cha Mafunzo ya Vijana, kilichoanzishwa Agosti 2017, kwa Agizo la Rais, na mwanzo halisi wa kazi ya Chuo kilikuwa Julai 2018, nacho ni kituo kilichokabidhiwa viongozi watendaji waliohitimu ambao wanafanya kazi katika vyombo vya utawala vya serikali, kufanya kazi na kushindana katika ngazi ya kimataifa ndani ya Taasisi za serikali ya Misri, tena inafanya kazi ya kutoa fursa kwa vijana kuwa na jukumu la kuongoza, kwa kuwawezesha, na kuwapa mafunzo kwa njia sahihi, hii inafanyika kwa mfano wa nchi kubwa Duniani, ambazo zina taasisi zinazofanana katika suala hili, kuchukua "Mabadiliko na kuunda Mwanamume wa Nchi" kama kauli mbiu yake.
Shughuli za mafunzo katika Chuo hicho zimegawanyika katika sekta kadhaa, kuna Shule ya Rais ya Sekta ya Kuwezesha Uongozi, ambapo programu 5 muhimu ziko nayo, na kuna Programu ya Rais ya Sekta ya Kuwawezesha Vijana kwa Uongozi, iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri mwaka 2016, na ilikuwa nguzo kuu ya wazo la kuanzisha Chuo hicho.
Shule ya Rais ya Uongozi pia ina Programu ya Rais ya Watendaji Wanaohitimu kwa Uongozi, ambayo inahusika na kundi kubwa la umri, kuliko Mpango wa Rais wa Kuwezesha Vijana kwa Uongozi, kwani inashughulikia kundi la umri kutoka miaka 30 hadi 45, na ilizinduliwa kutoka ndani ya Chuo baada ya kuanzishwa kwake.
Kwa upande mwingine, kuna Mpango wa Rais wa Kuwawezesha Vijana wa Afrika kwa Uongozi, ambao ulikuja kujibu mamlaka ya Rais katika Jukwaa la Vijana wa Kiarabu na Afrika huko Aswan 2019.
Chuo kinahusika na kuanzisha ushirikiano na taasisi na mashirika ya kimataifa ili kufaidika na utaalamu wake, muhimu zaidi ni ushirikiano wa kimkakati na Shule ya Kitaifa nchini Ufaransa "ENA", Kituo cha Mafunzo ya Usalama cha Geneva, na kutoka kwa mavuno ya 2020 kusaini ushirikiano wa kimkakati na Kituo cha Kitaifa cha Maendeleo ya Rasilimali Watu nchini Korea Kusini, ambayo ni moja ya vituo 6 muhimu zaidi vya ubora ulimwenguni ambavyo nchi kama Malaysia, Japan na Urusi hukimbilia kufuzu na kutoa mafunzo kwa makada wanaofanya kazi katika vifaa vyao vya utawala, pamoja na itifaki na Shirika la Maendeleo la Uholanzi ambayo ni pamoja na moja ya vyuo vikubwa vilivyobobea katika maendeleo ya mitaa.
Ni vyema kutaja kuwa Chuo kina wenzake katika nchi nyingi kubwa, haswa Ufaransa, Malaysia na Korea Kusini, kwani kuna taasisi kadhaa katika nchi nyingi zilizoendelea zilizokabidhiwa makada wa umma waliohitimu kutoka serikalini.