"Salim Ahmed Salim" Mtaalam wa Mahusiano ya Kidiplomasia ya AFRO-ASIA na KILATINI

"Salim Ahmed Salim" Mtaalam wa Mahusiano ya Kidiplomasia ya AFRO-ASIA na KILATINI

Imefasiriwa na / Aya Nabil

Mwanadiplomasia mkongwe mwenye ushawishi mkubwa katika diplomasia ya kimataifa, anayejulikana kama lulu ya siasa ya kigeni; kwa kuwa mtu muhimu katika diplomasia na mahusiano ya kimataifa, mtu pekee kutoka Afrika aliyetikisa ulimwengu kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mnamo 1981, naye mwanasiasa anayeheshimiwa zaidi nchini Tanzania, tena huyo alikuwa sababu ya kupoteza sera shindwa.

Salim Ahmed Salim alizaliwa mnamo Januari 23, 1942, katika Usultani wa Zanzibar (baadaye Tanzania) kwa baba mwenye asili ya Oman anayeitwa Sheikh Ahmed Salim na mama Mwafrika – Mtanzania. Salim alipata elimu yake katika Kitivo cha Lumumba huko Zanzibar, akaendelea na masomo yake ya shahada ya kwanza katika Kitivo cha St. Stephen’s, Chuo Kikuu cha Delhi, akapata digrii ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Columbia cha Mahusiano ya Kimataifa huko New York,akawa mwanaharakati wa wanafunzi mnamo miaka ya 50 ya karne ya 20 kama mwanzilishi na naibu wa Mkuu wa Muungano wa Wanafunzi wa Zanzibar.

Alipata shahada za heshima za Uzamivu kutoka vyuo vikuu kadhaa katika taaluma mbalimbali kama vile Sheria, Falsafa, Masuala ya Kimataifa na Sayansi ya Utu,alizipata mwaka wa 1980-1998:

Mwakani 1998: Uzamivu wa Sheria, Chuo Kikuu cha Cape Town, Afrika Kusini.

Mwakani 1996: Uzamivu wa Falsafa, masuala ya Kimataifa, Chuo Kikuu cha Bologna, Italia.

Mwakani 1995: Uzamivu wa Sanaa katika Masuala ya Kimataifa, Chuo Kikuu cha Khartoum, Sudan.

Mwakani 1991: Uzamivu wa Sheria ya Kiraia, Chuo Kikuu cha Mauritius.

Mwakani 1983: Uzamivu wa Sayansi za Utu, Chuo Kikuu cha Maiduguri, Nigeria.

Mwanasiasa Salim Ahmed Salim alianza kazi yake katika uandishi wa habari, akiwa mhariri mkuu wa Gazeti la Zanzibar Daily. Na  mwanachama mashuhuri wa Shirika la Waandishi wa Habari la Zanzibar, aliingia katika ulimwengu wa kidiplomasia na kuchukua nafasi nyingi za kitaifa, Kiafrika, na kimataifa. Alianza kazi yake ya kidiplomasia kama balozi wa Tanzania kwa Misri mnamo 1961, jambo lililomfanya kuwa Mtanzania mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya nchi hiyo katika nafasi hiyo, pia aliteuliwa kuwa balozi wa nchi kama China, Cuba, Trinidad na Guyana.

Alifanya kazi kama mkurugenzi wa masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania mnamo 1968, kisha akateuliwa kuwa balozi wa Jamhuri ya Watu wa China mnamo 1960-1970. Akawa mwakilishi wa kudumu wa nchi yake katika Umoja wa Mataifa huko New York katika miaka ya 1970-1980, wakati huo alikuwa pia Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kamishna wake mkuu huko Barbados, Jamaica, Trinidad na Tobago.

Alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo 1976,  aliongoza kikao cha 34 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mnamo 1979, na pia aliongoza vikao vya dharura vya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa nusu ya kwanza ya mwaka wa 1980. Mnamo Septemba 1980, aliongoza Kikao maalum cha 11 cha Mkutanomkuu wa Umoja wa Mataifa.

Pia alishika nafasi ya Uenyekiti wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Ukoloni wakati wa 1972-1980, na wakati wa Uongozi wake alikuwa na mchango unaojulikana kama "Mkali" katika kuondoa ukoloni katika Angola, Msumbiji, Guinea-Bissau, Cape Verde, Sao Tome, Principe, na Zimbabwe.

Baada ya kuacha Umoja wa Mataifa mwaka 1980, alirejea Tanzania na kushika nafasi nyingine, akiongoza diplomasia ya Tanzania kutoka  nafasi yake ya Waziri wa Mambo ya Nje 1980-1984, na kisha kuwa Waziri Mkuu 1984-1985, na Waziri wa Ulinzi 1986-1989.

Uzoefu wake wa kidiplomasia ulimwezesha kuchaguliwa kama Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Afrika, na ndiye pekee – kati ya Katibu Wakuu wake -  aliyehudumu kwa mihula mitatu mfululizo, kisha akachaguliwa kama mjumbe maalum wa Umoja wa kiafrika ili kutatua mgogoro wa Darfur Magharibi mwa Sudani. Inaashiriwa kuwa alifanikiwa katika jaribio la China la kupata kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa hivyo China ilimpa nishani ya Heshima mnamo 2019, ambayo mtoto wake alipokea.

Salim Ahmed Salim aliongoza mikutano mingi ya kimataifa, makongamano, semina na warsha chini ya uangalifu wa Umoja wa Mataifa, Shirika la Umoja wa kiafrika, Harakati Zisizofungamana na mashirika mengine Duniani kote.

Alipata tuzo nyingi na nishani za kitaifa, Kiarabu na Kiafrika, ikiwa ni pamoja na: Nishani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1985), Nishani ya Mille Collins ya Rwanda (1993), Nishani ya Afrika ya Libya (1999), na Nishani ya Nileen ya Sudan (2001). Alitunukiwa huko Tanzania mnamo Oktoba 2014 kwa kutoa tuzo ya “Wana wa Afrika”, ambayo hupewa kwa watu ambao wamefanya huduma kubwa kwa Bara, kwa kutambua jukumu lake la "kuelimika na kuongeza" Barani Afrika.

Vyanzo