Davidson Nicol... Daktari Mwafrika aliyekabiliwa na ubaguzi kutokana na rangi yake

Davidson Nicol... Daktari Mwafrika aliyekabiliwa na ubaguzi kutokana na rangi yake

Imeandikwa na / Cripso Diallo

Imefasiriwa na / Mervat Sakr

Utengano  ( Decolonization) sio juu ya kusimama dhidi ya muktadha wa maarifa ya Magharibi kwa ujumla au kupendekeza nadharia ya njama ya Magharibi, bali ni kufikia uhuru wa lengo na haki kwa maarifa juu ya watu hapo awali waliodhulumiwa na kutengwa kiutamaduni na kihistoria katika kiwango cha mafanikio ya mtu binafsi na ya pamoja.

Wote wanafahamu kuwa Frederick Banting na John McLeod wanasifika kwa kugundua matibabu ya kisukari na insulini mwaka 1921, lakini wachache wanaofahamu Davidson Nicol, Daktari Mwafrika ambaye alikabiliwa na ubaguzi kwa sababu ya rangi yake baada ya kupata udhamini kwa ugumu na alifikia Uingereza kupata Uzamivu na kisha kufanikiwa kufikia hatua ya kwanza ya njia, jinsi ya kutengeneza na kuunda muundo wa insulini ya binadamu badala ya wanyama, na kuchambua kuvunjika na upinzani wa insulini katika mwili wa binadamu, hiyo ilikuwa hatua muhimu iliyosababisha mafanikio katika matibabu ya ugonjwa sio tu unaolenga viwango vya sukari ya damu, lakini pia hushughulikia matatizo yanayohusiana na moyo, hatimaye kusababisha kupunguza vifo vya wagonjwa wa Kisukari.

Davidson Nicol alizaliwa mnamo Septemba 14, 1924, katika mji wa Freetown, Sierra Leone. Mwaka 1943, Nicol alisafiri kwenda Uingereza na kwenda Chuo Kikuu cha Cambridge kusoma Sayansi asilia. Kisha akawa Mwafrika wa kwanza kuhitimu kwa heshima ya darasa la kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge, kisha ametoa barua kwa Shule ya Matibabu ya Hospitali ya London ili kuwa Daktari wa Moyo. Kwa mtazamo wa kwanza kwa sababu ya jina lake, Kitivo kilidhani alikuwa yeye ni mtu mweupe, lakini walipogundua kuwa yeye ni Mwafrika na mweusi walikataa kumruhusu aende Chuo Kikuu. Baadaye, profesa katika Chuo Kikuu cha Ibadan alimsaidia kujiandikisha katika Kitivo ya matibabu, na tayari alipata Uzamivu wake na kisha akaanza kufundisha katika kitivo. Mwaka 1957 alirudi katika Chuo Kikuu cha Cambridge na kuchaguliwa kuwa mshirika. Mnamo kipindi hiki, alichambua kuvunjika na upinzani wa insulini katika mwili wa binadamu na kisha kugundua jinsi ya kuunda muundo na utengenezaji wa insulini ya binadamu, na uzi huu, ambao wanasayansi waliufuata mwaka 1984 kwa kutumia uhandisi wa maumbile, ulitengenezwa na insulini ya binadamu, ambayo ina sifa ya insulini ya wanyama, ambayo watu walilazimika kujipa sindano za kila siku za zilizotengenezwa na nguruwe au ng'ombe, kwa nguvu ya ufanisi wake na ukosefu wa madhara.

Hajajali wala hajakasirika kwa sababu jina Davidson Nicol limezama au kupuuzwa katika ukanda wa vyuo vikuu vya Magharibi au mara chache hupatikana kwenye kurasa za majarida makubwa ya sayansi ya kimataifa na asili. Lakini janga kubwa liko katika ukweli kwamba uzalishaji wa maarifa unaingiliana kwa ukamilifu na muktadha ambao hutoa kiwango cha ubinafsi kwa watu wengi kutoka Kusini mwa Dunia ambao hawaoni katika ukombozi wa kielimu  unaotokana na uchunguzi na utafiti ili kuonesha mifano kama Davidson Nicol au maslahi katika mazingira ya ndani ni kitu kikubwa. Nkwazi Nkuzi Mhango katika kitabu chake "Kuondoa Ukoloni: Kuondoa Athari na Sumu Zilizomo katika Simulizi ya Ubaguzi wa rangi Barani  Afrika. (Decolonization: Getting rid of the Traces and Toxins Inherent in the Racist Narrative Dominant on the African Continent)" ambapo anawasilisha jinsi Waafrika wanavyoingiza maarifa na mawazo potofu katika shughuli zao wakati na baada ya kuangamizwa kwa ukoloni, na jinsi dhana hizo zinavyoonyeshwa katika masomo ya kitaaluma au yasiyo ya kitaaluma katika utafiti na maono yao wenyewe.