Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa watangaza orodha ya awamu ya kwanza kwa Wamisri wanaoomba kushiriki katika toleo la tatu la Udhamini

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa watangaza orodha ya awamu ya kwanza kwa Wamisri wanaoomba kushiriki katika toleo la tatu la Udhamini

Imetafsiriwa na: Al-Sayeda Tarek 
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ulitangaza orodha ya awamu ya kwanza ya kufuzu kwa Wamisri, kuomba kushiriki katika Udhamini wa Nasser katika toleo lake la tatu chini ya kauli mbiu "Vijana wa Harakati kutofungamana na Upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini", umeopangwa kufanyika Mei 31 hadi Juni 17, 2022, chini ya ufadhili wa Rais Abdel Fattah El-Sisi. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, orodha ya awamu ya kwanza inachukuliwa kuwa kundi la viongozi wa vijana, wawakilishi wa vyombo vya utendaji, viongozi kadhaa wa vyama vya wanafunzi katika ngazi ya Jamhuri, pamoja na wanaharakati wa asasi za kiraia, wataalamu wa vyombo vya habari, waandishi wa habari, wajasiriamali wa kijamii, pamoja na watafiti katika vituo vya utafiti wa kimkakati na mawazo. 

Ikumbukwe kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika toleo lake la tatu, umeopangwa kufanyika Juni 2022 chini ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri kwa mara ya pili mfululizo, na ushiriki wa viongozi wa vijana wa 150 kutoka nchi za 79 kutoka nchi zisizofungamana na upande wowote duniani kote, kulingana na Mkakati wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini wa Umoja wa Mataifa, Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, pamoja na Dira ya Misri 2030, Kanuni za Bandung, na Harakati kutofungamana na upande wowote kama kumbukumbu muhimu zaidi na nyaraka ambazo udhamini huo unategemea mwaka huu.