Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ni mfadhili na msaidizi wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Wizara ya Mambo ya Nje  ya Misri ni mfadhili na msaidizi wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Wizara ya Mambo ya Nje ndiyo chombo kikuu cha Nchi chenye jukumu la kuanzisha, kuendeleza na kukuza mahusiano ya Misri na nchi zote za Dunia, pamoja na taasisi na vyombo vya kikanda na kimataifa, pia Wizara hiyo ina jukumu la kupendekeza na kutekeleza sera ya nje ya nchi, pia yachangia kuhifadhi Amani,Usalama na maslahi ya nchi, na hivyo vikitegemea kanuni za Katiba, Sheria na Sera kuu ya nchi.

Haswa ina jukumu la kupendekeza na kutekeleza sera ya nje, pia kusimamia mahusiano ya nje katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na zingine. Pia ina jukumu la kusoma na kuchambua hali za kisiasa zinazohusiana na sera ya nchi zingine na kiwango cha athari zake za sasa na baadaye katika sera ya serikali, pia kufuatilia maendeleo yake na kutathmini kwa kuzingatia sera ya nje ya Misri.

Wizara ya Mambo ya Nje yaendelea na harakati zake maalum kupitia duru za sera za kigeni za Misri katika ngazi ya pande mbili na pande nyingi, basi mwaka huu unashuhudia juhudi kubwa za kushauriana na kuratibu na ndugu wa Kiarabu kukuza nafasi za ushirikiano katika sekta zenye kipaumbele, na vile vile kuimarisha mifumo ya hatua za pamoja za Waarabu katika kukabiliana na changamoto tofauti zinazoshuhudiwa na eneo hilo. Pengine kubwa zaidi kutoka hayo ni uungaji mkono kwa suala la Palestina na uungaji mkono wa wananchi ndugu wa Palestina, ambapo inalaani vikali mashambulizi ya Israel dhidi ya Msikiti wa Al-Aqswa na kukataa kabisa vitendo vyovyote haramu vyenye lengo la kudhoofisha haki thabiti na halali kwa watu ndugu wa Palestina, haswa mashambulizi yaliyofanywa kwa watu wa kitongoji cha "Sheikh Jarrah", yakizingatiwa ukiukwaji wa sheria za kibinadamu za kimataifa.

Wizara ya Mambo ya Nje pia inajali kuunga mkono mwingiliano wa dhati na wa vitendo na washiriki wa kimataifa na mifumo ya kikanda na kimataifa na vikao husika na haki za binadamu, na hivyo kwa ajili ya kufafanua sera na misimamo yetu ya kitaifa kuhusu masuala ya haki za binadamu, na kuanzisha mipango inayoelezea maslahi ya Misri ya kitaifa na yanaendana na Ajenda na vipaumbele vya nchi zinazoendelea na nchi za Afrika kwa upande wa kimataifa, pia inatoa umuhimu mkubwa kwa kuimarisha mshikamano wa kimataifa ili kusaidia mwenendo wa maendeleo kwa kuzingatia malengo ya maendeleo ya kimataifa.

Kwa upande wa mahusiano ya Misri na Asia, suala la maendeleo limechukua kipaumbele cha juu cha sera za kitaifa za Misri na nchi za Asia kwa ndani na nje, na Asia kwa Misri ni kama uwanja mpana wa mawasiliano ya ustaarabu na kiutamaduni, basi kuna dondoo muhimu ya utamaduni  kati ya Misri na nchi nyingi za Asia zilizowakilishwa katika kuwepo kwa mikataba ya kiutamaduni na baadhi ya nchi hizo.

Misri na washiriki wake wa Asia pia wako kwenye mahusiano mapya katika ushirikiano wa kiuchumi, ambapo Asia ni mshiriki wa tatu wa kibiashara wa Misri baada ya Ulaya na Marekani, na ushirikiano huo unatokana na manufaa ya pande zote, na kubadilisha ushirikiano huo kutoka uhusiano kati ya serikali tu ukawa uhusiano unashughulikia misingi maarufu  pia watu wenyewe na nguvu zote za jamii ya kiuchumi, haswa wafanyabiashara.

Inapaswa kuashiria juhudi za sera ya nje ya Misri kuelekea bara la Afrika, ambapo iko moyoni mwake,ina nia ya kuunga mkono juhudi zote za ushirikiano wa kiuchumi katika nchi zote za bara, pamoja na kusaidia na kukuza programu za mafunzo na ukarabati na vijana kubadilishana programu na kuwawezesha kushiriki katika uongozi na kuunda maamuzi na kuwasaidia kushiriki na kuwakilisha nchi zao Kwa nje, kulingana na imani ya uongozi wa kisiasa katika kiunganishi kikubwa kati ya mustakabali ya Misri na mustakabali ya nchi za Afrika.

Ama kuhusu kiwango cha mahusiano ya Misri pamoja na nchi za Amerika ya Kusini, yanapata umuhimu wake kutokana na hali ya upatanisho wa kihistori, tukitazama ukaribu wa historia, na tabia ya juhudi zinazofanana katika maelezo mengi ya kujenga mataifa mawili yanayoinuka, nayo ni mahusiano ya kina ya chimbuko cha zamani sana hadi enzi za hayati Rais Gamal Abd El Nasser.

Misri inahangaika kuunganisha udugu na urafiki kati ya watu wa Misri na watu wa Amerika ya Kusini katika nyanja za kiutamaduni, kijamii, kisanaa, elimu, utalii, uchumi na michezo, na kuendeleza mahusiano ya kirafiki na udugu kati ya vijana wa Jamhuri ya kiarabu ya Misri na vijana wa nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini, na kuhimiza ushirikiano kati ya taasisi za wanawake nchini Misri na nchi tofauti za Amerika ya Kusini katika nyanja mbalimbali za shughuli za kiutamaduni, kijamii na kiuchumi kupitia kuhimiza mipango na miradi mingi iliyopitishwa na Wizara na inafanya juu chini kwa kuzizindua kabisa wakati huu.