Vijana na Michezo: ufadhili wa Mheshimiwa Rais kwa Udhamini wa Nasser kwa mwaka wa pili mtawalia

Vijana na Michezo: ufadhili wa Mheshimiwa Rais kwa Udhamini wa Nasser kwa mwaka wa pili mtawalia

Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta.Ashraf Sobhy, alisisitiza uongozi wa kisiasa nchini Misri, ukiongozwa na Rais Abd El Fatah El-Sisi, una nia ya kuimarisha na kuwawezesha vijana waafrika kupitia udhamini wa kuwezesha unaotolewa na Misri pamoja na udhamini wa kiufundi  unaotolewa na Mashirika na Wizara za Misri, linalochangia katika kupatikana upeo wa maendeleo na kuhamisha Taaluma na Tamaduni katika nyanja na Taaluma mbalimbali.

Waziri wa Vijana na Michezo alielezea umuhimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na kupata kwake kwa ufadhili wa Rais kwa mwaka wa pili mtawalia, ambao ni mwendelezo wa juhudi za serikali ya Misri kutekeleza jukumu lake lililokabidhiwa katika kuimarisha nafasi ya vijana ndani, kikanda, Barani na kimataifa kwa kutoa aina zote za usaidizi, uwezeshaji na mafunzo, pamoja na Kuwawezesha katika nafasi za uongozi na kufaidika na uwezo na mawazo yao pia, na hilo lililopitishwa na kutangazwa na Rais El Sisi wakati wa shughuli za Jukwaa la Vijana Duniani katika matoleo yake yote.

Baada ya sifa nyingi za kimataifa na mafanikio makubwa ya toleo la pili, toleo la tatu, lililopangwa kufanyika Juni ijayo 2022, lilipata ufadhili wa kusifiwa kutoka kwa Mheshimiwa Rais kwa mara ya pili mtawalia.

Inatajwa kwamba kundi la kwanza la udhamini wa Nasser kwa Uongozi ulilifanyika Juni 2019 chini ya ufadhili wa Waziri Mkuu wa Misri, Dokta. Mustafa Madbouly, uliwalenga viongozi vijana wenye taaluma mbalimbali na zinazofaa za utendaji ndani ya Jamii zao , Toleo la pili la udhamini  huo ulipatwa  ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, na kupanuliwa likijumuisha viongozi wa vijana kutoka mabara ya Asia, Amerika ya Kusini .