"Rasilimali za Maji na Maendeleo Endelevu" katika jedwali la mazungumzo ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

"Rasilimali za Maji na Maendeleo Endelevu" katika jedwali la mazungumzo ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
"Rasilimali za Maji na Maendeleo Endelevu" katika jedwali la mazungumzo ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
"Rasilimali za Maji na Maendeleo Endelevu" katika jedwali la mazungumzo ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
"Rasilimali za Maji na Maendeleo Endelevu" katika jedwali la mazungumzo ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
"Rasilimali za Maji na Maendeleo Endelevu" katika jedwali la mazungumzo ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
"Rasilimali za Maji na Maendeleo Endelevu" katika jedwali la mazungumzo ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Leo jioni, Alhamisi, Wizara ya Vijana na Michezo imehitimisha matukio ya siku ya tisa ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, kwa kikao cha mazungumzo kuhusu “Rasilimali za Maji na Maendeleo Endelevu” kwa ushiriki wa Dkt. Abbas Sharaki, Profesa wa Jiolojia na Rasilimali za Maji kwenye Chuo Kikuu cha Kairo, Dkt. Jihan Abdel Salam, Profesa wa Uchumi katika Kitivo cha Mafunzo ya Juu ya Afrika, Chuo Kikuu cha Kairo, Bi.Amira Sayed ambaye ni mwandishi wa habari katika Egyptian Gazette na mwakilishi wa Misri katika Bunge la Kimataifa la Maji kwa Vijana, na kilisimamishwa na Bw.Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.

Dkt. Abbas Sharaki, Profesa wa Jiolojia na Rasiliamali za maji katika Chuo Kikuu cha Kairo, wakati wa hotuba yake kwenye kikao cha mazungumzo ya mwisho ya matukio ya siku ya tisa ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, alionesha uzoefu wa Misri katika kukabiliana na ukame na uhaba wa maji, akiashiria kuwa kuna baadhi ya ukweli na changamoto za maji zinazoikabili nchi ya Misri, zinazochangia wengi wao wanakabiliwa na changamoto zinazokabili nchi za Afrika, akisisitiza kuwa nchi za Afrika hazina bahati ya kiasi cha maji, na hapa Misri tunaona kuwa zaidi ya 80% ya Rasiliamali zetu za maji huvukiza, kwani Misri inashikilia ngazi ya kwanza ulimwenguni katika uhaba wa mvua.

Katika hotuba yake, "Sharaki" alishughulikia vyanzo vya maji vya Misri, ambavyo Mwenyezi Mungu aliviwakilisha kwa maji ya Mto Nile, ambayo Misri inaishi na inategemea kama msingi, na ni maji ya mara kwa mara  yasiyoongezeka, yanayosababisha mateso kwa serikali kwa kuzingatia changamoto zinazoikabili katika mfumo wa kutoa mahitaji ya maji ya Wamisri, na akaonesha sababu za Kujenga Bwawa la Juu ili kufaidika kiwango kidogo cha maji kinachokuja Misri na mengi yake huenda kwenye Bahari ya Mediterania, licha ya kuzungumzia jinsi Misri inavyoshughulika kwa kuzingatia hisa yake ndogo ya maji na ongezeko la watu wake na utekelezaji wa miradi mingi mipya katika wakati huo huo, na alielezea njia maarufu zaidi za matumizi mabaya ya maji na aina ya uchafuzi wa maji, mabadiliko ya tabianchi na athari zake kwa Misri, ambapo aliiona kuwa nchi yenye ushawishi mdogo kuliko nchi nyingi Duniani, akielezea kuwa Misri ndiyo nchi pekee ambayo maji yake yote yanatoka nje ya mipaka, na kuna kanuni za ulimwengu kwa mito ya kimataifa.

Mwanzoni mwa hotuba yake, Dkt. Jihan Abdel Salam, Profesa wa Uchumi katika Kitivo cha Mafunzo ya Juu ya Afrika, Chuo Kikuu cha Kairo, alielezea furaha yake kuwa katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, akiashiria kuwa usalama wa maji kama dhana inamaanisha uwezo wa mtu binafsi ili kupata kiwango cha chini cha maji kinachofaa kwa matumizi yake, na unaohusiana na usalama wa taifa na vipimo vyake vya kiuchumi vinavyohusiana na usalama wa maliasili, na “Abdel Salam” aliongeza kuwa usalama wa maji sio tu mahitaji ya mtu binafsi, bali unahusiana na usalama wa taifa, na Bwawa la Al-Nahda ni suala la usalama wa taifa la Misri, kwani Misri inategemea maji ya Mto Nile kimsingi kama moja ya vyanzo vyake muhimu vya maji, na alisisitiza kuwa bila maendeleo na bila watu nchi hazitaishi, na usalama wa maji ndio uhai, maendeleo, utulivu na mwendelezo wa serikali. Pia, aligusia mifumo ambayo Misri ilitekeleza katika mgogoro wa Bwawa la Al-Nahda, na jukumu la Misri katika maendeleo ya nchi za Afrika na miradi iliyofanya katika muktadha huu, pamoja na kuzungumzia changamoto zinazokabili usalama wa maji nchini Misri, ikiwa ni pamoja na ongezeko la watu na athari zake katika kupungua kwa upatikanaji wa maji kwa kila mtu, licha ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kiasi cha maji nchini Misri na Duniani kote.

Katika hotuba yake, Bi.Amira Sayed, mwandishi wa habari katika Egyptian Gazette na mwakilishi wa Misri katika Bunge la Kimataifa la Maji kwa Vijana, aliishukuru Wizara ya Vijana na Michezo kwa mwaliko wa kuhudhuria kikao hicho muhimu, na kusifu utofauti na utajiri wa masuala ya Udhamini, na aligusia ufafanuzi wa Bunge la Vijana Ulimwenguni kama chombo cha vijana kinachojumuisha wataalamu na wasio wataalamu katika faili ya maji ili kuwa uhusiano kati ya wataalamu na wasio wataalamu na kati ya watoaji wa maamuzi na maoni ya umma. Na Bunge lilifanya kikao cha mashauriano kwa kupitia miaka mitatu mfululizo na kina kamati zaidi ya moja na mabunge ya ndani zaidi ya moja katika ngazi ya nchi zote. Vilevile, kuna maandalizi ya kuzindua Bunge la Afrika, na pia Bunge liko kwa nguvu zote katika maandalizi ya mkutano ujao wa kilele wa tabianchi. Na Sayed aligusia umuhimu wa diplomasia ya vijana na jukumu la vijana katika diplomasia ya maji, ambapo shinikizo la mara kwa mara la Rasiliamali za Maji zilizopo, lilisababisha mahitaji ya kuimarisha diplomasia ya maji, inayowakilisha vijana sehemu muhimu ya jukumu la diplomasia ya maji, kwa kuzingatia umuhimu wa ushiriki wa vijana katika kufanya maamuzi, ambapo suala la maji ni sehemu hawawezi kutenganishwa na usalama wa taifa na hivyo ni lazima wawepo katika kufanya maamuzi.

Kwa upande wao, washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, wakati wa kikao cha mazungumzo kilichofanyika ndani ya matukio ya siku ya tisa ya Udhamini huo kuhusu suala la Rasiliamali za Maji na Maendeleo Endelevu, waliibua maswali na mijadala kadhaa juu ya suala hilo muhimu la kila mtu katika nchi mbalimbali na mabara ya Dunia, wakisisitiza umuhimu wa usalama wa maji kama usalama wa taifa wa nchi na watu.

Kwa upande wake, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Bw.Hassan Ghazali, amegusia umuhimu wa mada ya kikao hicho cha mazungumzo kuhusu usalama wa maji ambao  ndio usalama wa taifa unaopaswa kulindwa na kuusimamishwa kwa umakini na hekima kubwa kwa sababu umuhimu wake mkubwa kwa mustakabali wa watu na nchi, akiashiria kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuhamisha uzoefu wa Misri ya kale katika kujenga taasisi za kitaifa pamoja na kufanya kazi katika kuunda kizazi cha viongozi wa vijana  kutoka nchi zisizofungamana zenye maoni sanjari na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza mwamko wa jukumu la Harakati ya kutofungamana.