Video | Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Vijana huko Nigeria asifu Harakati ya kimataifa ya Nasser kwa Vijana

Kiongozi hodari, Balozi "Egbe Sokubo", Mkuu wa Baraza la kitaifa la Vijana nchini Nigeria, alitoa pongezi zake za dhati kwa Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana katika Kumbukumbu wangu ya nne ya kuanzishwa kwake, na hiyo ilitokea katika mkutano wa video pembezoni mwa Kongamano la Kwanza la Ushauri kwa Vijana waafrika, lililofanyika huko Ufalme wa Morocco, sambamba na sherehe za watu huru za Kumbukumbu ya sabini ya Mapinduzi Matukufu ya Julai, Kwa mahudhurio ya kundi la viongozi vijana katika kiwango cha bara la  Afrika, na kwa maandalizi ya Muungano wa Vijana wa Afrika,pamoja na Ufadhili wa  Mfalme Mohammed VI bin Al-Hassan, Mfalme wa Morocco ndugu.

Mwanzoni mwa mazungumzo hayo," Egbe Sokubo" alielezea fahari yake kwa viongozi wa vijana wa Nigeria wanaoshirikiana na Harakati ya kimataifa ya Nasser kwa Vijana, na aliwapendelea kwa pongezi na Salamu, na akakamilisha salamu zake kwa viongozi wote wa vijana wa harakati ya Nasser katika nchi zote za ulimwengu, akiashiria kwamba Harakati ya kimataifa ya  Nasser  kwa Vijana, ni Jukwaa la upainia linalounganisha mabara (Asia, Afrika, Ulaya, Australia na Amerika ya Kusini), ikilenga kuunda Raia wa ulimwengu mzima mwenye sifa za ndani, na ana uwezo wa kuendeleza nchi yake, na kusonga mbele kuelekea kuboresha kiwango cha mazingira yake ya ushawishi, akichangia kikubwa katika kuwekeza nguvu na ujuzi wa wenzake na kuwawezesha, akisisitiza kuwa hilo ndilo linalotarajiwa na bara kama siku zijazo ambapo vijana wake wanaamini umuhimu wa umoja na mshikamano wao ili kufikia Afrika. tunayoitaka. 

Kwa upande wake, "Hassan Ghazali", Mwanzilishi wa Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana, alisisitiza kuwa Harakati hiyo ni moja ya njia za kuwezesha “Hati ya Vijana wa Afrika,” mfumo huo wa kisheria wa uwezeshaji wa vijana, sambamba na ramani ya Umoja wa Afrika ya kuwekeza vijana, pamoja na kazi yake ya kuwekeza nguvu zao kwa ajili ya  kuhakikisha malengo ya Ajenda ya Afrika 2063, pia, inakusanya makundi ya watu wengi kuelekea hilo, ikieleza kuwa Harakati  hiyo inashughulikia kufafanua ajenda za maendeleo,na mikataba ya kikanda na kimataifa, na kusanya makundi ya jamii ya kiafrika , ili kupata kibali na msaada , na kisha kusonga mbele kuelekea katika kuyatekeleza kwa haraka zaidi. na kwa urahisi, ikijumuisha (Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika) na Mkakati wa Ushirikiano wa Umoja wa Mataifa (Kusini - Kusini). 


Mwishoni mwa hotuba yake, Ghazali alisema kuwa Marehemu Kiongozi "Gamal Abdel Nasser" alitaka kuunga mkono viunganishi vya urafiki kati ya Misri na Nigeria baada ya uhuru mwaka 1960, iliyosababisha kuanza kwa uwakilishi wa kidiplomasia na kufunguliwa kwa Kituo cha Utamaduni cha Misri huko Kano, na kukuza mahusiano kati ya watu hao wawili, akisisitiza nia ya Misri ya kuimarisha ushirikiano na upande wa Nigeria katika nyanja zenye maslahi kwa pamoja, nazo ni pamoja na mafunzo na kujua ujuzi wa kidijitali, mashindano ya pamoja na maendeleo ya michezo, mafunzo na usaidizi wa maendeleo ya miradi, na programu za kubadilishana vijana kati ya nchi hizo mbili.