Mwaliko kwa watafsiri na watafiti katika uwanja wa masomo ya kiafrika kwa ajili ya kushiriki katika jarida la habari la kielektroniki "Afrika Yasimulia "

Mwaliko kwa watafsiri na watafiti katika uwanja wa masomo ya kiafrika kwa ajili ya kushiriki katika jarida la habari la kielektroniki "Afrika Yasimulia "

Imefasiriwa na / Nourhan Khaled

Kulingana na umuhimu wa Utamaduni wa Kiafrika na utambuzi wa mafanikio yake katika ustaarabu wa binadamu, Kituo cha Kitaifa cha Tafsiri, kikiongozwa na  Dkt. Karma Sami kimeshatoa toleo kwanza la jarida la kielektroniki "Afrika Yasimulia " inayolenga kusambaza ufahamu wa jamii na kitaifa kwa ngazi zote za utamaduni wa kiafrika kama  fasihi, sanaa na sayansi mbalimbali , na habari hizo inatangazwa katika tovuti za mitandao ya kijamii. 

Na kituo hicho kinaelezea mwaliko kwa watafsiri na watafiti katika masomo ya Kiafrika ili kushiriki katika matoleo yajayo kwa kazi zao za tafsiri za uteuzi kutoka matokeo ya kifasihi Kiafrika sawa ya kijadi  au kisasa yanayodokeza vipengele vingine vingi vya kiutamaduni na ustaarabu wa kiafrika ya zamani yenye thamani na pia kutoa maonesho ya vitabu vya kudokeza fikra za Kiafrika ubunifu katika nyanja mbalimbali za kuandika kwa Kiarabu sawa ya kuhusu lugha za Kiafrika za kitaifa au kuhusu lugha za kimataifa kama Kiingereza, na Kifaransa, sharti iwe lugha asilia ya kitabu hicho , na mwishoni kusambaza muhtasari za tasnifu na tafiti katika nyanja mbalimbali za kiutamaduni Kiafrika, pamoja na mahojiano na watu wasomi muhimu na mashuhuri.
Kazi zote zinapelekwa kupitia baruapepe ya Kituo:
Info@nct.gov.eg