Programu ya Kimawazo ya Julai ya Kwanza | Omba sasa

Programu ya Kimawazo ya Julai ya Kwanza | Omba sasa

Taasisi ya Afrika ya maendeleo na kujenga uwezo, kwa kushirikiana na Harakati ya Nasser kwa Vijana, kwa kuzingatia juhudi zao za kuimarisha na kufufua kumbukumbu ya kitaifa, yajiandaa kuzindua programu ya Kimawazo ya Julai ya kwanza, sambamba na sherehe za watu huru wa maadhimisho ya miaka 71 ya Mapinduzi tukufu ya Julai, na miaka 5 tangu kuanzishwa kwa Harakati ya Nasser kwa Vijana, hiyo inakuja kuanzia Julai 23 hadi Julai 26, kila siku kwa muda wa siku nne, kuanzia saa moja hadi nne usiku, katika makao makuu ya kihistoria katika Jengo la Immobilia, huko Downtown.

 Pamoja na uwezekano wa kushiriki karibu kupitia (Programu ya Zoom / Video Conference) kwa wana wote wa nchi za Kiarabu, tukijua kuwa ufunguzi utakuwa Julai 23, saa nne asubuhi hadi sita adhuhuri kwenye kaburi la kiongozi Gamal Abdel Nasser, ambapo shada la maua litawekwa kwenye kaburi, na njia ya usafiri itapatikana kutoka kwa kaburi hadi jumba la makumbusho ili kuanza shughuli za programu na kikao cha ufunguzi hapo.

Imepangwa kuwa programu inaonesha usomaji wa kina ili kutazama Mapinduzi ya Julai, mkabala wake wa mageuzi na maendeleo, na mafunzo yaliyopatikana kutokana na mambo kadhaa yanayohusiana na elimu, utamaduni, na haki ya kijamii, kwa mahudhurio ya wataalamu na wasomi muhimu zaidi wa Misri.

Hiyo inakuja kama njia mojawapo ya kujenga uwezo wa  kada za vijana na wanafunzi ambao Taasisi ya Afrika inauzingatia sana kupitia programu zake, matukio ya kiutamaduni na mikutano ya kiakili mara kwa mara.

Pia, ikumbukwe kuwa mshiriki katika programu ya Kimawazo ya Julai ya kwanza atapata cheti cha kukamilika kwa kozi hiyo, ila lazima kuhudhuria siku nne zilizopangwa kwa programu.

Ili kujiandikisha, tafadhali bonyeza hapa