Kumbukumbu ya Miaka 71 ya Mapinduzi Tukufu ya Julai | Ushiriki sasa

Kumbukumbu ya Miaka 71 ya Mapinduzi Tukufu ya Julai | Ushiriki sasa

Katika tukio la maadhimisho ya miaka 5 ya kuanzishwa kwa Harakati ya Nasser kwa Vijana, tena sambamba na maadhimisho ya miaka 71 ya Mapinduzi ya Julai 23, na jukumu lake kubwa la kihistoria katika kusaidia harakati za ukombozi za kitaifa za Afrika na nchi za ulimwengu wa tatu, na kuunga mkono ujenzi wa mfano wa hali ya kisasa ya kitaifa, tunafurahi kupokea makala yenu, maoni na mitazamo pia kwa kuchapishwa kwenye tovuti rasmi ya Harakati ya Nasser kwa Vijana.

Unaweza kuzungumzia mada yoyote yafuatayo kama mada ya makala:

- Athari za Mapinduzi ya Julai juu ya kina cha Kiarabu na utaifa wa Kiarabu.

- Uhusiano wa kiongozi Gamal Abdel Nasser na viongozi wa Kiarabu, na uhusiano wa Mapinduzi ya Julai na mapinduzi ya Kiarabu, ambapo maadhimisho ya 71 ya Mapinduzi ya Julai mwaka huu yanaambatana na Mwaka wa Vijana wa Kiarabu.

Mapinduzi ya Julai na athari zake kwa Jumuiya ya kimataifa.

- Jukumu la kiongozi  marehemu Gamal Abdel Nasser na mipango yake ndani na kimataifa.

- Jukumu la Mapinduzi ya Julai katika kuunga mkono harakati za ukombozi wa kitaifa za Afrika.

- Jinsi Mapinduzi ya Julai yalivyochangia Umoja wa Afrika.

- Jukumu la Kiongozi Gamal Abdel Nasser katika ukombozi wa watu wa Global South(Ulimwenguni Kusini)

Pia, unaweza kuzungumzia mada nyingine kutoka kwa mtazamo wako na kutoka kwa mazingira wa jamii yako.

Hatimaye, peleka makala yako pamoja na (picha mwafaka ya makala - picha ya kibinafsi - jina lako kamili) kupitia baruapepe rasmi ya tovuti ya Makala na Maoni:

‏Articles@nasseryouthmovement.net